Ngono, mauaji, na miili katika masanduku – ni wanaume gani waliohusika?

g

Chanzo cha picha, Albert Alfonso/Flickr

Maelezo ya picha, Yostin Mosquera (Kushoto), Albert Alfonso (Katikati) na Paul Longworth (Kulia) wanaonekana kama walikuwa wakivinjari wakati likizo
Muda wa kusoma: Dakika 6

Mauaji ya Albert Alfonso na Paul Longworth na Yostin Mosquera yalifichua ulimwengu hali ya juu wa maisha ya ngono , video chafu za wavuti na uundaji wa maudhui ya watu wazima. Lakini wanaume hao watatu walifahamianaje - na kwa nini Mosquera aliwaua?

Onyo: Makala haya yana maelezo ambayo yanaweza kuwafadhaisha baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na vurugu na maelezo halisi ya ngono.

Wanaume watatu wakifurahia safari ya mashua ya mwendo kasi katika mapumziko ya kifahari huko Colombia - selfie ya Albert Alfonso na Yostin Mosquera na Paul Longworth inawafanya waonekane kama marafiki bora.

Lakini ukweli halisi ulikuwa ni tofauti kabisa.

Nyuma ya tabasamu kulikuwa na uhusiano mgumu kulingana wa kingono , utawala na shughuli za kifedha, zote zilikuwepo pamoja na ushirikiano wa upendo na kujali.

Miezi minne baada ya picha hiyo kupigwa, Mosquera aliwaua wanaume wote wawili bila huruma katika gorofa yao ya London mnamo Julai 8, 2024, kabla ya kukatakata miili yao, na kusafiri zaidi ya maili 116 (kilomita 186) pamoja nao kwenye sanduku. Alimkodisha mtu aliyekuwa na gari kumpeleka Bristol, ambaye alimshusha karibu na daraja la jiji, ambapo Mosquera alipanga kuwatupa.

h

Chanzo cha picha, Albert Alfonso/Flickr

Maelezo ya picha, Paul Longworth (kushoto) na Albert Alfonso (kulia) walikuwa wameishi pamoja kwa miaka 20

Albert, 62, na Paul, 71, hapo awali walikuwa wamefunga ndoa ya kiserikali na wakati walikuwa wametengana, walibaki karibu na kuendelea kuishi pamoja.

Polisi waliwaelezea wanaume hao kama wasio na "familia kubwa, wala marafiki", badala yake walikuwa "wanategemeana sana kwa kila kitu".

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Albert alikuwa mwalimu wa kuogelea na alikuwa akifanya mazoezi ya kuwa mlinzi katika Gym ya Klabu ya Mode huko Acton, magharibi mwa London.

Alikulia Bidart, Ufaransa, na akapata mafunzo katika shule ya hoteli huko Biarritz kabla ya kuhamia Uingereza kusimamia hoteli.

Hapo awali alikuwa meneja mkuu katika 375 Kensington High Street – makazi ya kifahari magharibi mwa London.

Katika taarifa zilizosomwa kwa Mahakama ya Woolwich Crown, Mfanyakazi mwenzake wa zamani wa Albert walimtaja kama "mcheshi, mwenye mamlaka na motisha".

Ilikuwa katika jengo hili ambapo Albert alikutana na Paul, mfanyakazi ambaye alikuwa amestaafu hivi karibuni.

Walipendana sana kutokana na ukweli kwamba wote wawili walilelewa na familia ambazo sio za wazazi wao na mnamo Februari 2023 waliingia katika mahusiano ya kiraia, ingawa marafiki wa Paul waliiambia BBC kwamba "hakuwa wazi kuhusu ujinsia wake" na kumtaja Albert kama kaka yake.

Paul alielezewa sana na marafiki na majirani kama "mkarimu sana".

Kevin Dore, 74, kutoka Shepherd's Bush, alikuwa akinywa pombe na Paul na alimjua kwa zaidi ya miaka 20.

"Yeye ni mtu mzuri, mchangamfu, mkarimu," alisema.

"Daima adabu. Daima angekununulia kinywaji, mkae chini na uzungumze."

George Hutchison, ambaye pia alikuwa akinywa pombe na Paul, alisema: "Alikuwa mmoja tu mmoja wetu. Alikuwa mtu mzuri sana, hakuwahi kumdhuru mtu yeyote."

g

Chanzo cha picha, Albert Alfonso/Flickr

Maelezo ya picha, Mosquera alichapisha video za ngono zilizokithiri mtandaoni kwa kutumia majina bandia

Ingawa Albert alisemekana kuwa msiri juu ya maisha yake ya kibinafsi, kesi hiyo ilifunua ulimwengu wa ngono iliyokithiri ambao alilipia mara kwa mara, alishiriki na kushirikisha umma video mtandaoni.

Ilikuwa ni upande wa maisha yake ambao Paulo hakuwa na uhusiano wowote nao, ingawa aliufahamu na alionekana kuikubali.

Mosquera, raia wa Colombia, pia alikuwa akichapisha video zake nyingi mtandaoni akifanya vitendo vya ngono vilivyokithiri chini ya majina bandia.

Sasa ana umri wa miaka 35, aliishi Medellin, na alikuwa na kaka watano na dada mmoja, ambaye alikufa miaka michache iliyopita. Pia ana watoto wawili.

Albert na Mosquera walianza kuzungumza kupitia Skype kuanzia karibu mwaka 2012. Kufikia 2017, Albert alianza kumlipa Mosquera kwa video za ngono, ambazo ziliripotiwa kuwa mbaya zaidi baada ya muda.

Unaweza pia kusoma:

Hatimaye walikutana ana kwa ana mnamo 2023 wakati Mosquera aliposafiri kwenda Uingereza kwa mara ya kwanza.

Lakini inaonekana Albert alielewa vibaya uhusiano wao wa kimapenzi.

Wakati ilionekana Albert alikuwa ndani uhusiano huo kwa ajili ya ngono, Mosquera alikuwa ndani yake kwa ajili ya kupata pesa.

Mahakama ilimsikiliza Albert akielezea alivyokuwa ameweka maisha yake yote wazi kwa mtu ambaye uhusiano wake ulikuwa, kwa kweli, wa shughuli.

Taarifa za benki za Albert zinaonyesha kuwa alipokea zaidi ya £17,500 kati ya tarehe 2 Septemba 2022 na 12 Julai 2024 kutoka kwa kampuni inayoendesha tovuti ya ponografia iliyokithiri.

Kati ya Mei 2022 na Februari 2024, Albert alimtumia Mosquera jumla ya $7,735 katika malipo 72 - sawa na takriban £5,800.

Na kati ya Januari 2024 na 19 Juni 2024 Albert alimtumia £928 kupitia MoneyGram, ambayo hutoa huduma za kimataifa za kuhamisha pesa.

Kwa malipo hayo Mosquera alichapisha ponografia kwenye wavuti nne, pamoja na video na picha zaidi ya 100, kwa kutumia majina bandia.

Wateja walikuwa wameomba maonyesho ya ngono na kati ya tarehe 30 Juni 2022 na 12 Juni 2024 alipata $2,682.90.

g

Chanzo cha picha, Albert Alfonso/Flickr

Maelezo ya picha, Picha inayoonyesha Mosquera akifurahia eneo la utalii huko London

Lakini Mosquera aliiambia mahakama kuwa hakujua Albert alikuwa akishirikisha umma video zake mtandaoni hadi siku chache kabla ya kumuua - licha ya kukubali kwamba alitia saini fomu ya idhini mnamo 2023 ikimruhusu Albert kupakia picha zake mtandaoni ili apate faida ya kifedha.

Wakati Mosquera aliposafiri kwenda Uingereza mnamo Oktoba 2023 alikaa nyumbani kwa Albert London na usafiri huo ulikuwa umelipwa na Albert.

Mosquera aliiambia mahakama kwamba alibakwa "kila siku" na Albert na kwamba hakufurahia vitendo vya ngono vilivyokithiri, ambavyo alilipwa kuvifanya.

Wakati wa kukaa kwake, Mosquera alitembelea eneo la kitalii la Madame Tussauds, akasafiri kwa basi la wazi na akaenda safari ya mashua kwenye Mto Thames.

Kisha mnamo Machi 2024, Albert alimpeleka Paul hadi Colombia ambako walikaa Cartahenga - na Albert ambako alimlipia Mosquera aje kukutana nao.

Kevin Dore, mmoja wa marafiki wa Paul wa kunywa pombe aliiambia BBC walikuwa wamemuonya juu ya kusafiri kwenda nchini.

"Tulisema 'hapo ni mahali hatari Paul, usisumbuke huko'," Bw Dore alisema.

Mnamo Mei mwaka huo Mosquera alitengeneza video nyingine kali na Albert na ndani ya wiki chache alikuwa amerudi Uingereza, akikaa na wawili hao - tena kwa gharama ya Albert.

Wakati huu Albert alipanga tafrija ya wageni kwa Mosquera kwenye ukumbi wake wa mazoezi, akamweka ajiunge na kikundi cha Whatsapp cha timu ya mpira wa miguu ya kazi tano, na kumsajili kwenye kozi ya lugha ya Kiingereza ya wiki nne.

Wanaume hao watatu pia walisafiri kwenda Brighton kwa safari ya siku moja.

Lakini, katika siku chache kabla ya Mosquera kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow na wakati wa kukaa kwake, alikuwa akipata habari juu ya fedha za Albert na Paul, alitafuta sumu ya maiji maji ya viwandani na pia sumu nyingine hatari na kemikali zinazoweza kusababisha hatari kama vile saratani na magonjwa ya mishipa ya moyo.

Paul na Albert waliuawa mnamo tarehe 8 Julai.

h

Chanzo cha picha, Albert Alfonso/Flickr

Maelezo ya picha, Mosquera aliiambia mahakama kwamba alifanya tu vitendo vya ngono vilivyokithiri ili kupata pesa

Paul alipigwa mara kwa mara na nyundo, na kuvunjwa fuvu lake. Mwili wake ulifichwa chini ya kitanda, wakati Mosquera akingojea Albert arudi nyumbani.

Wakati wa kikao cha ngono kilichorekodiwa, Mosquera alimchoma kisu Albert hadi kufa, baada ya hapo aliimba na kucheza kuzunguka chumba.

Kisha akafikia kompyuta ya Albert katika jaribio la kutuma pauni 4,000 kwenye akaunti yake ya benki huko Colombia, na pia kutoa pesa zingine za kifedha.

Wakati hili liliposhindikana, alienda kwenye kituo cha pesa (ATM) kilicho karibu na akatoa mamia ya pauni kutoka kwa akaunti za Albert.

Mosquera alikata miili yao siku chache baadaye - akiweka vichwa vyao kwenye friji na kusafirisha sehemu zingine za mwili kwenye masanduku hadi Bristol.

Mauaji yasiyotarajiwa na ya kikatili ya Albert na Paul yaliishtua jamii yao.

Bw Dore alisema mauaji hayo yameuvunja moyo wake.

Mosquera alipatikana na hatia ya mauaji hayo mara mbili katika kesi katika mahakama ya Woolwich Crown na atahukumiwa mnamo mwezi wa Oktoba.

Ripoti ya ziada na Fiona Lamdin, Adam Crowther na Beth Cruse.