Ukiishi miezi 9 anga za mbali hivi ndivyo mwili wako utakavyobadilika

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, James Gallagher
- Nafasi, Health and science correspondent, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 3
Kutumia muda wako kuwa kwenye aga za juu na kuitazama sayari ya dunia kutokea juu ni uzoefu mzuri usio kifani ambao wengi wetu tunauota.
Hata hivyo, mwili wa mwanadamu unakuwa na mabadiliko fulani ili kukabiliana na mvutano uliopo kati ya anga na dunia. Kwa sababu mwili wa binadamu uliundwa kufanya kazi chini duniani. kuwa mazingira mengine kama anga ya mbali inaweza kuchukua miaka kadhaa mwili kurejea kikamilifu katika hali yake ya kawaida.
Wanaanga Suni Williams na Butch Wilmore wamerejea duniani wiki hii, baada ya misheni yao siku nane ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kugeuka misheni ya miezi mitatu. Wmeishi muda huo bila kutarajia.
"Anga ni mazingira magumu zaidi ambayo binadamu wamewahi kukutana nayo, na hatujakuwa kwneye nafasi nzuri zaidi ya mabadiliko ya kimwili ili kuweza kukabiliana na hali hiyo ngumu," Prof Damian Bailey, ambaye anasoma fiziolojia ya binadamu, katika Chuo Kikuu cha Wales Kusini, anasema.
Kuingia kwenye anga za juu hubadilisha hali ya mwili wa mwanadamu, na pale mwanzo mwanzo, mwili huweza kushtuka kutoka na ugeni wa mazingira.
"Unahisi kama uko likizo," mwanaanga Tim Peake, ambaye alienda kwa ISS mnamo 2015, anasema.
'Moyo wako unafanya kazi kwa urahisi. Misuli yako na mifupa yako pia inakuwa haina kazi kubwa ya kufanya. Unasafiri ndani ya kituo cha anga bila uzito, ni hali ya kushangaza."
Fikiria kutumia wiki kadhaa umelala kitandani bila kuinuka kabisa, hii ni moja ya mbinu ambazo wanasayansi hutumia kuchunguza athari za anga kutokuwa na mvutano na dunia, na hapo utaanza kuelewa athari zake. Kutokuwa na mvutano huu kunamaanisha kwamba mtu anakuwa anaelea tu, havutwi chini kudondoka wala haendi juu.
Nguvu za Misuli
Kwa misuli, ni suala la "kuitumia au uipoteze."
Hata kusimama tu kunatumia misuli mingi mwilini ili kuhakikisha mwili unasimama na kudumu wima. Lakini hilo haliwezekani ukiwa huko kwenye anga za mbali, ISS.
Nguvu ya misuli huchukua maana tofauti unapoishi kwenye mazingira ambayo kila kitu kinaelea, chepesi hakina uzito.
Kuzeeka kwa Haraka
Moyo na mishipa ya damu hupata unafuu ukiwa angani kwani havina kazi ya kupambana na mgandamizo wa dunia, lakini hiyo pia husababisha udhaifu.
Mifupa nayo huwa dhaifu na rahisi kuvunjika.
Kwa kawaida, mwili huwa na uwiano kati ya seli zinazovunja mifupa ya zamani na zile zinazojenga mifupa mipya. Lakini bila mvutano wa dunia, mchakato huu huvurugika.
"Kila mwezi, takriban 1% ya mifupa na misuli yao hutoweka (ukiwa angani), ni kama kuzeeka kwa kasi," anasema Profesa Bailey.
Hali hii huonekana wanaporudi duniani.
Mazoezi ya Lazima
Hii ndiyo sababu wanaanga huenda angani wakiwa katika hali bora kabisa ya kiafya.
Kila siku, wanatumia takriban masaa mawili kufanya mazoezi , wakitumia mashine ya kukimbia, baiskeli ya mazoezi na vifaa vya kuinua vitu vizito, ikiwemo vyuma vya mazoezi, ili kudumisha afya ya misuli na mifupa.
Sasa, Suni na Butch wataanza mpango mkali wa kufanya mazoezi ili kurejesha uwezo wao wa mwili.
"Itawachukua miezi michache kujenga tena misuli yao," anasema Dk. Helen Sharman, mwanaanga wa kwanza wa Uingereza.
Mifupa inaweza kuchukua "miaka michache" kurudi katika hali yake ya awali, lakini hata hivyo, "kuna mabadiliko madogo katika aina ya mfupa unaojengwa baada ya kurudi duniani ambayo huenda isirejee katika hali ya kawaida kabisa."
Lakini si misuli na mifupa pekee inayobadilika, anga huathiri mwili mzima.
Hata aina za bakteria wazuri waliomo mwilini, yaani microbiome nao hubadilika.

Chanzo cha picha, NASA
Mabadiliko ya Majimaji Mwilini
Majimaji mwilini pia hubadilika katika hali ya kutokuwa na mgandamizo.
Badala ya kuvutwa chini kuelekea miguuni kama ilivyo duniani, majimaji haya husafiri juu kuelekea kifuani na usoni.
Uso kuwa mviringo na kuvimba ni moja ya mabadiliko ya kwanza yanayoonekana.
Lakini hali hii pia inaweza kusababisha uvimbe kwenye ubongo na mabadiliko kwenye macho, yakiwemo neva ya macho, retina na hata umbo la jicho.
Hali hii, inayoitwa "ugonjwa wa macho unaohusiana na safari za anga," inaweza kusababisha kuona kwa ukungu na hata uharibifu wa macho wa kudumu.
Kuhisi Kizunguzungu
Kama hakuna mgandamizo, pia huvuruga mfumo wa vestibula, ambao husaidia kuhisi mwelekeo na kudumisha usawa wa mwili.
Katika anga za mbali, hakuna juu, chini au pembeni.
Hali hii inaweza kuwa ya kuchanganya unapoingia angani na pia unaporudi duniani.
Tim Peake anasema: "Awamu ya kwanza ya kuacha kuhisi kizunguzungu, kurejesha usawa wa mwili na kuwa na nguvu ya kutembea kawaida, huchukua siku mbili au tatu tu."
"Siku hizo za kwanza baada ya kurudi duniani zinaweza kuwa ngumu sana."












