'Afrika mashariki inamaslahi zaidi DRC kuliko UN'- Evariste Ndayishimiye

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema kuwa Afrika Mashariki Ina maslahi zaidi ya usalama kuliko vikosi vya walinda amani wa umoja wa mataifa katika nchi ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ndayishimiye ambaye ni mwenyekiti ya jumuiya ya EAC amesema watafanya kila juhudi kurejesha Amani na utawala wa Sheria nchini DRC.

Ndayishimiye ameyasema hayo huku akijiandaa kutimiza miaka 3 tangu alipochukua uongozi wa taifa la Burundi baada ya kifo cha mtangulizi wake Hayati Pierre Nkurunziza.

Katika mahojiano na BBC mwandishi wetu Dinah Gahamanyi alimuuliza kwanza hali ilivyo kwa Sasa akilinganisha na miaka 3 alipochukua uongozi...