Makamanda wa Urusi walijadiliana kutumia silaha za nyuklia nchini Ukraine - Marekani

Chanzo cha picha, RUSSIA DEFENCE MINISTRY
Viongozi wakuu wa kijeshi wa Urusi walijadili mwezi uliopita jinsi na lini wanaweza kutumia silaha za nyuklia vitani Ukraine maafisa wawili wa Marekani wameiambia CBS News.
Vladimir Putin hakuhusika katika mazungumzo hayo, waliambia mshirika wa BBC wa Marekani.
Ikulu ya White House ilisema imekua "ina wasiwasi" juu ya uwezekano wa matumizi ya silaha za nyuklia katika miezi michache iliyopita.
Lakini ilisisitiza kuwa Marekani haikuona dalili yoyote ya Urusi kujiandaa kwa matumizi hayo.
Hilo linathibitisha tathmini za awali za kijasusi za Magharibi kwamba Moscow imekuwa haisongezi silaha zake za nyuklia.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alishutumu Magharibi kwa "kusukuma mada hiyo kwa makusudi", ingawa muda wa majadiliano hayo ya ngazi ya juu ya kijeshi ya Urusi katikati ya Oktoba ni muhimu.
Kufikia mwishoni mwa Septemba Rais Putin alikuwa ameeneza matamashi yake ya nyuklia dhidi ya Magharibi, akizungumzia juu ya kutumia njia zote anazoweza kuilinda Urusi na ardhi ya Ukraine ambayo alikuwa amechukua.
"Huu sio upuuzi," alisema, akishutumu nchi za Magharibi kwa kuibua usaliti wa nyuklia na kujivunia silaha za Kirusi ambazo zilikuwa za kisasa zaidi kuliko silaha zozote za Nato.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Akijibu ripoti za vyombo vya habari vya Marekani kwamba Urusi ilijadili kutumia silaha za nyuklia, msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema: "Tumekua na wasiwasi kuhusu uwezo huo kwani miezi hii imepita."
Kadiri uwezo wa kijeshi wa Urusi kwenye medani ya vita ukipungua, vitisho vyake vya nyuklia vinaonekana kuongezeka.
Moscow imeishutumu Ukraine kwa kuandaa "bomu chafu", lililowekwa nyenzo zenye mionzi, ingawa Ukraine na nchi za Magharibi zinasema Urusi inajaribu tu kujenga kisingizio cha kuilaumu Kyiv ikiwa kifaa kama hicho kitatumika.
Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, alizungumza na viongozi wenzake wa Marekani, Uturuki na Ufaransa ili kuzungumzia njama hiyo ya Ukraine.
Hata hivyo, wakati wizara ya ulinzi ya Urusi ilipotoa picha kuelezea matokeo yake, serikali ya Slovenia ilisema haraka kwamba picha hizo zilikopwa kutoka kwa Wakala wake wa Kudhibiti Takataka za Mionzi na zilionyesha vifaa vya kugundua moshi vya 2010.
Katika wiki za hivi karibuni, mipango ya nyuklia ya Urusi imechunguzwa kwa karibu kutokana na hali ambayo inaweza kutumia silaha hizo , haswa silaha ya "kimkakati ambayo inaweza kutumika kwenye uwanja wa vita huko Ukraine.
Silaha ya kimkakati ya nyuklia ni ya kutumika katika mapigano, kinyume na silaha kubwa "za kimkakati" ambazo zimeundwa kusababisha uharibifu mkubwa.
Wakati Urusi ilifanya mazoezi ya kawaida ya nyuklia wiki iliyopita, ilikuwa chini ya hali ambayo ilikuwa ikilipiza kisasi shambulio la nyuklia la adui kwa silaha kubwa ya kimkakati. Bw Putin alikuwa na msimamo mkali kwamba mazoezi ya nyuklia ya Urusi yaliruhusu tu matumizi ya kujihami ya silaha za nyuklia.
Lakini siku ya Jumanne naibu mkuu wa baraza la usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, aliangazia kipengele kingine cha mazoezi ya Urusi - matumizi ya nyuklia katika tukio la tishio linalowezekana kwa serikali. Alidokeza kuwa malengo ya vita vya Ukraine ni kurejesha maeneo yote ambayo yalikuwa yake hapo awali, na kwamba yenyewe ilikuwa tishio lililopo.

Chanzo cha picha, EPA
Bw Medvedev huenda asisikizwe na rais, lakini maoni yake yanaonyesha imani ya Bw Putin kwamba kunyakua rasmi maeneo makubwa ya kusini na mashariki mwa Ukraine kumeyafanya kuwa eneo la Urusi, hata kama hayatambuliki kama sehemu ya Urusi na jumuiya ya kimataifa.
Na katika taarifa yake siku ya Jumatano, wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilikariri kuwa Moscow ilikuwa na haki ya kutumia silaha za nyuklia kujibu "uchokozi wa matumizi ya silaha za kawaida wakati usalama wa serikali uko hatarini".
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema kutakuwa na "matokeo makubwa" ikiwa Urusi itatumia mbinu ya kinyuklia katika uwanja wa vita nchini Ukraine. Aliwaambia wabunge hatabashiri juu ya matukio hayo .
Alipoulizwa wiki iliyopita na BBC kukanusha kwamba Urusi itatumia silaha za nyuklia nchini Ukraine, mkuu wa idara ya ujasusi wa kigeni SVR, Sergei Naryshkin, alisema Urusi ina wasiwasi mkubwa kuhusu matamshi ya nchi za Magharibi na kuushutumu uongozi wa Ukraine kwa kujaribu kupata silaha za nyuklia.















