Waandamanaji wanaopinga kodi Kenya walishinikiza kanisa kuwa na msimamo

Vijana misa kanisani Kenya
Maelezo ya picha, Vijana wamiminika kanisa kuhudhuria misa ya kuwakumbuka waliouawa katika maandamano Kenya
    • Author, Barbara Plett Usher
    • Nafasi, Mwandishi BBC Africa
    • Akiripoti kutoka, Nairobi

Maandamano ya vijana nchini Kenya kupinga nyongeza ya ushuru kwa namna fulani imesaidia kanisa kuzinduka.

Yameitikisa taasisi yenye nguvu, katika nchi ambayo zaidi ya 80% ya idadi jumla ya watu, akiwemo rais mwenyewe ni wakristo.

Vijana wamelishutumu kanisa kwa kuegemea upande wa serikali na kuchukua hatua dhidi ya wanasiasa wanaotumia mimbari kama jukwaa la kisiasa.

Katika Jumapili moja ya hivi karibuni, viongozi wa kanisa katoliki, waliipokea changamoto hiyo.

Waliandaa misa maalum ya vijana kutoka makanisa ya ndani na maeneo yanayouzunguka mji wa Nairobi, kama njia ya kutoa heshima na kuwakumbuka wale waliouawa katika maandamano ya kupinga nyongeza ya kodi.

Mamia ya vijana walikusanyika katika kanisa la Holy Family Basilica kuwaombea waliofariki.

Wiki kadhaa tu zilizotangulia, misa ya Jumapili ilitatizwa kwa kelele kutoka kwenye madhabahu ya kanisa hilo.

Ni hatua ambayo haikutarajiwa kutoka kwa vijana – wanaofahamika kama Gen-Z.

Walikuwa wanahisi kuwa kanisa haliwaungi mkono.

Askofu Simon Kamomoe alijaribu kuwashawishi kuwa wamesikika.

“Ninajua vijana mara nyingine munahisi kanisa linawavunja moyo,” alisema.

“Tungependa kuahidi upya uwajibikaji wetu katika kuwatumikia. Huenda tumekosa…Mungu atusamehe kama kanisa ambapo mbele yake Mungu, hatujawaridhisha..”

Aliwasihi kuwana subira katika kutafuta malengo yao, waongozwe na kanisa na watubu madhambi yoyote yaliotekelezwa wakati wa maandamano.

“Hatutaki kuwapoteza, hatutaki kuwapoteza vijana wetu,” alisema kwa uwazi mkubwa.

“Maaskofu wa kikatoliki wana wasiwasi kuhusu kukipoteza kizazi hiki,” alisema, akiwaomba wadumishe amani na walinde maisha yao.

Misa hiyo iligubikwa kwa nyimbo za kiroho na kumalizika kwa shangwe wakati watu wakipunga hewani bendera za Kenya.

Baadhi ya waliohudhudira misa hiyo walisema ni hatua ya kwanza inayokaribishwa, lakini iliochelewa.

Unaweza kusoma
Vijana misa kanisani Kenya

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Takriban watu 39 waliuawa katika maandamano yalioanza Juni 25
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

“Ninahisi kuwa kwa mara ya kwanza kanisa linatambua kuwa vijana wanalichukulia suala hili kwa uzito,” ameeleza Yebo, aliyeshiriki maandamano kabla kuzuke vurugu na ambaye hakutaka kujulikana.

“Na ninahisi kuwa kanisa halijatuunga mkono. Hawajakuwa na msimamo kwa muda mrefu.

“Vijana wameendelea kusisitiza, wameleta matokeo zaidi ya kanisa kwa hali inayoshuhudiwa sasa ya mabadiliko ya uchumi.Tunamuona rais anawachukulia vijana kwa uzito kuliko hata kanisa.”

Mashirika yamakanisa yalishinikiza dhidi ya mswada wa fedha unaopendekeza nyongeza ya ushuru, lakini vijana waliomiminika barabarani kwa kiwango kikubwa ndio waliomshinikiza rais Ruto kurudi nyuma.

Na sio hilo tu.

Maandamano ya vijana sasa yanashutumu uhusiano kati ya ukristo na taasisi za kisiasa.

Mara kwa mara pembezoni mwa misa, wanataja shaka yao kuhusu viongozi wa makanisa wanaokwenda ikulu ya rais ikiwemo wakati wa maandamano.

Moja ya mambo walioyataka na waliopata ni kusitishwa kwa uchangishaji wa fedha maarufu kama harambee ambapo wanasiasa hutoa viwango vikubwa vya fedha kwa makanisa.

Misaada hii inaweza kununua ushawishi wa kisiasa Jumapili asubuhi.

Maandamano yalionuiwa kulistisha hilo yalipewa jina #OccupyChurch yaani makanisa yadhibitiwe.

Vijana misa kanisani Kenya
Maelezo ya picha, Baadhi ya vijana wanaamini kuwa viongozi wa makanisa wamekuwa na ukaribu sana na siasa

Baadhi pia walipinga rais Ruto kuhudhuria halfa iliodhaminiwa na kanisa. Lakini aliunga mkono msimamo wao.

“Kwenye suala la kupnga siasa katika mimbari ninaliunga mkono100%,” aliwaambia waandhishi habari katika mahojiano nao yaliopepeperushwa hewani moja kwa moja kitaifa.

“Hatustahili kutumia mimbari katika makanisa au katika sehemu nyingine ya kuabudu , kuendeleza siasa. Sio sawa.”

Siku kadhaa baadaye, aliwapiga marufuku viongozi wa serikali na watumishi wa umma kutoa misaada kwenye halfa za uchagishaji wa fedha na kumuagiza mkuu wa sheria kuunda mkakati utakaofanikisha utoaji misaada ya aina hiyo kwa njia yenye mpangilio na yenye uwazi.

Lakini rais mwenyewe amekuwa na utamaduni huu wa kutumia mimbari ya kanisa kama jukwaa la kisiasa.

Rais William Ruto Kenya

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Ruto aliutupilia mbali mswada wa fedha uliopendekeza nyongeza ya ushuru

“Ujumbe wake ulikuwa ukisukumwa ndani ya kanisa,” anasema reverend Chris Kinyanjui, katibu mkuu wa baraza la kitaifa la makanisa Kenya (NCCK).

“Kwahivyo, watu wanahisi kuwa wana serikali ya kikristo.”

Na mtazamo huo wa kikristo wa Ruto umefanya kuwa vigumu kwa wachungaji wengi kumwajibisha, Rev Kinyanjui amesema. Badala yake wanakuwa kama “washikadau wa utawala huu," amedai.

"Rais wetu anazungumza kwenye mimbari. Unajua hiyo ina maana gani? Hawezi kuhojiwa. Kwahivyo amekuwa kiongozi mwenye nguvu katika siasa Kenya na mizunguko ya makanisa.

Vijana maarufu Gen Z wanahoji na wanasema hatujui tofuati kati ya serikali na kanisa."

BBC imeiuliza serikali kutoa tamko lakini msemaji wa serikali amesema hawezi kutoa tamko kwa sasa.

Alikuwa anazungumza wakati kukifanyika mabadiliko katika baraza la mawaziri na idara ya huduma za usalama yalioidhinishwa na rais Ruto kufuatia maandamano nchini.

Shutuma kutoka kwa vijana nchini zinaweza kubadili namna mamlaka au nguvu inavyofanya kazi Kenya.

Wao ndio idadi kubwa ya idadi ya watu nchini na hawako katika mizunguko inayoweza kutabiriwa ya kisiasa.

Rais sasa anasikiliza, na kanisa pia linasikiliza.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Maryam Abdalla