Simulizi ya utata ya Operesheni iliyowasomba maelfu ya watoto wa Vietnam kwenda Marekani

Baby lift

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati Kanali wa Jeshi la anga la Marekani Regina Aune aliposikia sauti ya mlipuko ndani ya ndege kubwa ya mizigo aina ya C-5, alijua kwamba alikuwa na sekunde chache tu za kuwafikisha mamia ya watoto hao mahali salama. ofisi.

"Nilijua tunaanguka," Aune, mwanamke wa kwanza kupokea tuzo ya Cheney kutoka kwa Jeshi la anga kwa "vitendo vya kishujaa na vya kujitolea" baada ya kuokoa watoto kadhaa licha ya kuvunjika, aliiambia BBC Mundo..

"Kitu ambacho hatukujua ni mahali gani, kwa sababu C-5 [ndege ya mizigo ambayo haina madirisha mengi. Tulichojua ni kile tulichoweza kuona kuwa ni uharibifu wa ndege hiyo."

Baby lift

Chanzo cha picha, US AIR FORCE

Maelezo ya picha, Kanali Aune

Ndege iliyopata ajali ya Lockheed C-5A Galaxy ya Jeshi la Wanaanga la Marekani - ambayo Kanali Aune alikuwa mmoja wa wasafiri siku ya Aprili 4, 1975 - inelezwa ilikuwa ya kwanza na safari ya kwanza ya operesheni iliyoitwa 'Babylift', juhudi kubwa za vikosi vya jeshi la Marekani baada ya mwisho wa Vita vya Vietnam za kuwasomba watoto kutoka Vietnam. Zaidi ya watoto 3,300 walihamishwa kutoka nchi hiyo ya Asia.

Nchi zingine kama Ujerumani Magharibi, Ufaransa, Canada nazo zilishiriki katika operesheni hiyo.

"Nimetoa maagizo kwamba dola milioni 2 zitengwe kwenye mfuko wa kimataifa wa misaada ya watoto ili kuwaleta yatima 2,000 kutoka Vietnam Kusini hadi Marekani haraka iwezekanavyo," Rais wa wakati huo Gerald Ford alitangaza Aprili 3, 1975 akiwa San Francisco.

Hata hivyo, ajali ya C-5 sio jambo pekee linalolalamikiwa kwenye Operesheni 'Babylift' ambayo iliathiri maisha ya mamia ya watu.

"Kulikuwa na upande mbaya mwingine wa operesheni hii kwamba sio watoto wote hawa walikuwa mayatima," Christian Appy, profesa wa Historia katika Chuo Kikuu cha Massachusetts, anaiambia BBC Mundo.

"Wakosoaji wengi walihoji kuwa kupeleka watoto hawa Marekani bila idhini ya wazazi wao ni sawa na kuwateka nyara."

Athari za ajali

Baby lift

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya ndege ya C-5 ambayo mstaafu Kanali Regina Aune alikuwa akisafiria, sekunde chache kabla ya kuanguka.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

C-5 ilipaa na kufika umbali wa futi 22,000 kabla ya kusikika mlio mkubwa. Kanali Aune anasema kwamba ilikuwa sauti ambayo kwa mtu yeyote aliye na mafunzo anaweza kutambua kwa urahisi.

"Unapoenda shule ya urubani, ya aina yoyote, lazima upate uzoefu wa aina hiyo ya suala kama hili," anafafanua.

"Tulijua vizuri kwamba kile ambacho kilikuwa kimetokea tu ni kitu kinachotokea kwa haraka."

"Kwa hivyo nikatazama chini na kuona Bahari ya China Kusini, ambayo kwa kweli sikupaswa kuiona, na huo ulikuwa mlango dharura punde niliweza kuona majimaji yanavuja kila mahali."

Ndege hiyo ilijibamiza mara mbili: kwanza, kando ya kwenye Mto Saigon, ikarushwa futi chache angani kabla ya kumalizia ajali ya pili mbaya iliyoua watu 138, wengi wao wakiwa watoto.

Aryn Lockhart anaiambia BBC Mundo kwamba anadhani alikuwa kwenye ndege hiyo, alipokuwa na umri wa mwaka mmoja tu.

"Nilichukuliwa nikiwa na umri wa mwaka mmoja, na wazazi wangu wanaamini sikuzote kwamba nilikuwa kwenye ndege hiyo ya kwanza," asema Aryn.

“Sina taarifa za familia yangu ya asili, sijui hata tarehe yangu ya kuzaliwa, yule mtawa aliyekuwa amenichagua kunilea kutoka kwa wazazi wangu alifariki katika ajali ya ndege, sina taarifa zozote kuhusu mwanzo wangu, na kufa kwako na taarifa zangu zilipopotea."

Baby lift

Chanzo cha picha, DICK LOEK

Maelezo ya picha, Watoto hawakupelekwa tu Marekani wengine walipelekwa kwa nchi washirika kama Canada

Kanali wa Jeshi la anga la Marekani Aune kwa upande wake anasema: "Jeraha nililolijua zaidi ni kuvunjika kwa mifupa kwenye mguu wangu," Aune aeleza.

"Na ni aina ya kitu cha kijinga unachofikiria, kwa sababu nilipoteza kiatu kwenye mguu wangu wa kushoto (mifupa iliyovunjika ilikuwa kwenye ule wa kulia)".

Katika simulizi yake, hakuwa na kumbuka kwa sababu ya umri wake.

Ni jambo ambalo, kwa mujibu wa maelezo yake, watu wengine wanasisitiza kuwa ilikuwa hivyo.

Watoto

Baby lift

Chanzo cha picha, SARAH BYNUM

Maelezo ya picha, Kwa SArah Bynum ni muhimu kujua alikotoka kabla ya kusonga mbele

Kuna aina mbili za watoto hapa. Wale ambao wanajeshi wa Mrekani walizaa na wanawake wa Vietnam wakati wa vita na wale ambao walikuwa ni yatima wenye asili ya Vietnam.

Mmoja wao ni Saran: “Nilikuwa na hasira nyingi ndani yangu, sikuwa na imani kuhusu sura za wanaume wala wanaume wenyewe kwa ujumla, maana nilisikia watu wengi wakisema vita ilikuwa ya kutisha na wanawake walijiuza, Inasikitisha sana," anasema.

"Niliwambiwa kwamba baba yangu alijua kwamba nilikuwepo. Ingawa hakujua kama ni msichana au mvulana, alijua kwamba alikuwa na mtoto huko Vietnam."

Baby lift

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miongoni mwa maelfu ya watoto waliosombwa kupelekwa Marekani walikuwa ni watoto wa Askari wa Marekani waliozaa na wanawake wa Vietnam

Kwa wengine kama Aryn, uzito wa siku za nyuma si mkubwa hasa kuhusu utambulisho wao na zaidi ni somo la udadisi mkubwa.

"Kwa namna fulani, nimeshakubaliana na hali, nmekubwalia kwamba mambo yalivyokuwa ndivyo hivyo hivyo yalivyo," anaambia BBC Mundo.

"Siku zote nilijua juu ya operesheni hii. Nadhani walezi wangu kila wakati walijitahidi kuhakikisha kuwa ninafahamu nilikotoka (asili yangu), nadhani ilipangwa hivyo ili niwe hapa."

Hiyo haimaanishi kwamba asili yake haukuwa imeamsha udadisi wake. Kwa kweli, huo ndio udadisi ambao Operesheni Babylift ilimtia nguvu hadi akafanikiwa kuwasiliana na watu kadhaa waliohusika nayo, akiwemo Kanali Aune.

Baby lift

Chanzo cha picha, JOINT BASE SAN ANTONIO

Maelezo ya picha, Aryn Lockhart anaamini alikuwa miongoni mwa watoto waliosombwa kwenye operesheni ya Baby Lift kutoka Vietnam na kupelekwa Marekani

"Baada ya muda tulikuwa karibu sana. Na kwa kweli tulikwenda mpaka Vietnam pamoja na tukaamua kuandika kitabu," Aryn anasema, akielezea kuwa operesheni hiyo ni kitu kinachomjia tena na tena katika maisha yake.

Madhara ya vita

Baby lift

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Ford alikosolewa kwa kutumia Operesheni hiyo kujijengea umaarufu wake

Mwanahistoria Christian Appy anaambia BBC Mundo kwamba, kihistoria, Operesheni 'Babylift' ni mwanzo wa mwisho wa mzozo ambao ungeweza kuepukwa.

Baby lift

Chanzo cha picha, GERALD FORD PRESIDENTIAL LIBRARY

Maelezo ya picha, Sio watoto wote waliosombwa wakati wa operesheni ya 'Baby lift' walikuwa yatima

"Marekani ndiyo ilikuwa chanzo," anaeleza.

"Kama Marekani isingeingilia kati kuunga mkono Ufaransa kuhusu Indochina baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Vietnam ingeunganishwa tena kama ilivyoanzishwa katika makubaliano ya Geneva ya 1954, chini ya serikali moja iliyochaguliwa kidemokrasia, na kuepuka vita vilivyoua watu milioni tatu."