Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nani alilipua Nord Stream? Ulaya inachunguza hujuma kubwa kwenye bomba kuu la gesi kutoka Urusi
Ulaya imeanzisha uchunguzi kuhusu hujuma kwenye njia tatu za bomba kuu la gesi kutoka Urusi.
Jeshi la wanamaji linashika doria katika Bahari ya Baltic inayovuja gesi ya Urusi, jeshi na polisi wanaimarisha ulinzi karibu na mitambo ya mafuta na gesi, na wanasiasa wanaahidi kuwawajibisha wale waliohusika na shambulio ambalo halijawahi kutokea kwenye miundombinu ya nishati ya EU.
Ni nani aliyelipua mistari mitatu ya Nord Stream kwa mara moja kwenye pwani ya Denmark na Uswidi, hatutajua katika siku zijazo. Ulaya inasema wana uhakika kuwa ni hujuma, kwani hata kukaribia eneo la milipuko kwa wiki ijayo hakutafanya kazi.
Siku ya Jumatano, siku ya tatu baada ya tukio hilo, gesi kutoka katika mabomba yaliyoharibiwa yalipasuka kwa nguvu sawa kutoka katika kina cha mita 80 hadi juu na kutoa mapovu juu ya eneo kwa kipemyo cha kilomita.
Nusu ya gesi inayopatikana kwenye mkondo uliokatika uliojazwa wa Nord stream tayari imeyeyuka, mamlaka ya Denmark na Uswidi ilisema. Uzito wa uvujaji hautapungua hadi mwishoni mwa wiki.
Meli za kivita za Ujerumani na Denmark hulinda eneo lililofungwa kwa usambazaji ndani ya eneo la maili tano za baharini.
"Mlipuko huo ulikuwa na nguvu sana, kwa hivyo itachukua muda kabla ya kuzama ndani ya maji huko," Waziri wa Ulinzi wa Denmark Morten Bedskov alisema katika mkutano na Jumatano. "Kwa kweli, inaweza kuchukua wiki moja au hata mbili kabla ya kila kitu kutulia hapo na tunaweza kuangalia eneo tu eneo hilo."
Alithibitisha hitimisho lililotolewa siku moja kabla na mamlaka ya nchi tatu za pwani kwamba milipuko mitatu kwenye nyuzi mbili za bomba la gesi ilikuwa hujuma. Sababu za asili za ajali hazijajumuishwa.
"Sio bahati mbaya. Kila kitu kilipangwa, kimepangwa kwa uangalifu," Bedskov alisema.
Nani anafaidika?
Urusi ilipoteza bomba kubwa na mpya zaidi la gesi kwenda Ulaya, ambayo, hata hivyo, haikupeleka gesi, kwani Ujerumani haikuthibitisha mstari mmoja, na Kremlin ilizuia mwingine katika duru iliyofuata ya vita vya gesi dhidi ya EU ikiwa ni katika jaribio la kutoa shinikizo na kuweka vikwazo kwa shambulio la Ukraine.
"Je, tunavutiwa na hili? Hapana, hatupendezwi. Tumepoteza njia za usambazaji wa gesi kwenda Ulaya," msemaji Dmitry Peskov aliambia mashirika ya habari ya Urusi.
Alikumbuka kuwa Marekani, ikiwa inaongoza duniani kwa nishati ya mafuta na gesi, inafaidika kutokana na kupunguzwa kwa usambazaji wa Urusi kwenye soko la Ulaya na kutokana na kupanda kwa bei ya gesi.
"Tunaona faida kubwa kutoka kwa wasambazaji wa gesi ya kimiminika wa Marekani, ambao wamezidisha usambazaji wao katika bara la Ulaya. Wana nia kubwa ya kupokea faida hizi kubwa," Peskov alinukuliwa na Interfax akisema.
Awali Marekani ilikuwa ikipinga Nord Stream 2. Vikwazo dhidi ya mradi huo viliwekwa na Donald Trump, lakini rais aliyefuata, Joe Biden, alivifuta.
Ikulu ya White House bado inazungumza kwa tahadhari juu ya milipuko kwenye mabomba ya gesi, ikidai kusubiri kwa ufafanuzi na kuahidi haitaipeleka Ulaya katika shida ya nishati.
Ulaya inaandaa "majibu magumu", NATO - ulinzi
"Uharibifu wowote wa makusudi wa miundombinu ya nishati ya Ulaya haukubaliki kabisa na utapata pingamizi la pamoja na kali," Joseph Borrell, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, aliwatishia wahujumu hao.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Denmark na kusema kuwa amejadili kuhusu hujuma ya mabomba ya Nord Stream na ulinzi wa miundombinu muhimu ya nchi za NATO.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Jeppe Kofod pia alitaja kutakuwa na majibu magumu na washirika wa Atlantiki, lakini aliahidi kuliangalia kwanza.
"Bado hatujui ni nani aliye nyuma ya hii. Na hatujui nia zao ni nini. Lakini kwa hali yoyote, hili ni shambulio la miundombinu yetu ya nishati katika maji ya kimataifa. Tunachukulia mambo kama haya kwa uzito mkubwa,” alisema.
Norway, msambazaji mkubwa zaidi wa gesi asilia kwa watumiaji wa EU, amechukulia kwa uzito zaidi kuhusu uvujaji huo.
Mamlaka ilisema Jumatano kwamba polisi na jeshi wameimarisha ulinzi kwenye majukwaa na mabomba. Na Equinor, kampuni kubwa zaidi ya Norway, imeongeza kiwango cha hatari na kuchukua hatua za ziada kwenye ardhi na nje ya nchi.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Uswidi ilikabidhi uchunguzi wa uharibifu huo kwa idara ya usalama wa taifa na ikaeleza hayo kwa kusema kwamba ni jinai kubwa ambayo angalau kwa kiasi fulani inaweza kuelekezwa dhidi ya maslahi ya taifa ya Uswidi na inaweza kufanywa na mamlaka za kigeni.
Je, inaweza kurekebishwa?
Mwendeshaji wa bomba la gesi la Nord Stream alipata ugumu hata kwa kukadiria matarajio ya ukarabati. Kremlin ilizungumza kwa ari ile ile.
"Hatuelewi nini cha kutengeneza bado. Tunawezaje kukadiria matengenezo ikiwa hatuelewi nini cha kutengeneza," Peskov alisema.
Wakati huo huo, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya bomba la gesi ya Ujerumani Gasunie Deutschland anasema yote hayajapotea.
"Kuna wataalam bora katika ajali kwenye mabomba, ardhini na chini ya maji, kuna usambazaji wa dharura wa mabomba," Reuters inamnukuu Jens Schumann. "Haya yote yanatia matumaini ya wastani kwamba hata hii inaweza kurekebishwa."
Matumaini haya yanakinzana na vyanzo vya gazeti la Ujerumani Tagesspiegel katika serikali ya Ujerumani.
Walisema Jumatano kwamba ikiwa ajali haitasafishwa haraka na maji ya chumvi yataingia kujaza bomba, Nord Stream inaweza kubaki na kutu chini ya Bahari ya Baltic.