Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je sheria za ngono za Indonesia 'zinamaanisha nini' kwa watalii?
Wanaofanya kazi katika sekta ya utalii nchini Indonesia bado wanaendelea kujaribu kujikwamua kutokana na athari mbaya za janga la Covid-19 . Na sasa bunge la nchi hiyo limepitisha sheria mpya ambazo baadhi wanahofu kuwa zinaweza kuwafukuza tena watalii – kwasababu kufanya ngono nje ya ndoa utakuwa ni ukiukaji wa sheria.
Sheria hiyo tata, ambayo wakosoaji wameiita "maafa" kwa haki za binadamu , pia inazuia wenzi wanaoishi pamoja ambao hawajaoana rasmi kuishi pamoja , na kudhibiti uhuru wa kisiasa na kidini. Kulikuwa na maandamano katika mji mkuu Jakarta wiki hii, na sheria hizo zinatarajiwa kupingwa mahakamani.
Sheria mpya ya uhalifu inatarajiwa kuanza kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu na itawahusu Waindonesia na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo, pamoja na wageni wanaoitembelea nchi hiyo.
Uchumi wa Indonesia unategemea pakubwa watalii kutoka Australia, ambayo ilikuwa chanzo cha kwanza cha utalii kabla ya janga la corona.
Maelfu ya watu husafiri kwenye kisiwa cha kitropikali Bali kila mwezi hali yahewa ya joto , huku wakijivinjari kwa bia za bei nafuu za Bintang na kushiriki katika shere za usiku kwenye baada na hoteli zilizopo ufukweni.
Ndoa za Bali ni ni za kawaida , na maelfu ya wanafunzi wa Australia wanaohitimu mafunzo yao husafiri kwa ndege kuelekea Bali kila mwaka kusherehekea kumaliza shule ya sekondari.
Kwa vijana wengi wa Australia, safari ya Bali huonekana kama kutoka umri wa utoto kuingia utu uzima. Wengine huenda pale mara chache kila mwaka kwa ajili ya likizo ya garama fupi.
Lakini mara tu baada ya taarifa kwamba sheria mpya zinakuwa halisi, baada ya uvumi kuzihusu wa miaka kadhaa, wasi wasi kuhusu safari zijazo ulianza kuwakumba Waastralia.
Kwenye kurasa za Facebook za utalii, watumiaji walijaribu kutaka kuelezea maana ya mabadiliko hayo nay ana maana gani kwa wageni watalii wanaoitembelea nchi hiyo.
Baadhi walisema kuwa wataanza kusafiri nav yeti vyao vya ndoa, huku wengine ambaoi hawajaolewa wakisema watakwenda kwingine kama sheria zinamaanisha kuwa hawataruhusiwa kulala chumba kimoja cha hoteli na mwenzi wao.
"Utatoa hongo ", alisema mmoja wa watumiaji katika kundi la usafirishaji la Bali Travel Community.
"Njia mojawapo ya kuangusha sekta ya utalii wa Bali," aliandika mwingine , huku wengine wakiafiki kuwa utakuwa ni "mkakato wa kutisha" ambao hautawezekana kuutekeleza.
Chini ya sheria mpya, wenzi ambao bado hawajaoana waliopatikana wakifanya ngono wanaweza kufungwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela na wale ambao watapatikana wakiishi pamoja wanaweza kufungwa kifungo cha hadi miezi sita gerezani.
Wakosoaji wanasema waandaaji wa likizo za mapumziko wanaweza kunaswa pia
"Tuseme mtalii Muaustralia ana mpenzi wake wa kiume au mpenzi wake wa kike ambaye ni mwenyeji ," Andreas Harsono, mtafiti wa ngazi ya juu katika Human Rights Watch aliliambia Shirika la utangazaji la Australia (ABC).
"Halafu wazazi wenyeji au wawaone kaka au dada waripoti wawaripoti katika polis iwa utalii . Itakuwa ni tatizo ."
Wageni wameambiwa wasiwe na hofu sana , kwasababu polisi watafanya uchunguzi tu pale ambapo mwanafamilia atakapolalamika – kama vile mzazi, mume au mke au mtoto wa mshukiwa wa kosa.
Lakini hilo pekee ni hatari, Bw Mr Harsono alisema, kwani linafungua mlango wa ya "utekelezaji wa baadhi ya sheria ".
"Inamaanisha kuwa haitatekelezwa dhidi ya watu fulani ,"aliiambia redio ABC.
"Halafu wazazi wenyeji au wawaone kaka au dada waripoti wawaripoti katika polis iwa utalii . Itakuwa ni tatizo ."
Wageni wameambiwa wasiwe na hofu sana , kwasababu polisi watafanya uchunguzi tu pale ambapo mwanafamilia atakapolalamika – kama vile mzazi, mume au mke au mtoto wa mshukiwa wa kosa.
Lakini hilo pekee ni hatari, Bw Mr Harsono alisema, kwani linafungua mlango wa "utekelezaji wa baadhi ya sheria ".
"Inamaanisha kuwa haitatekelezwa dhidi ya watu fulani ,"aliiambia redio ABC.
"Inaweza kuwa hoteli, inaweza kuwa watalii wa kigeni …hilo litawaruhusu maafisa wa polisi kuwatoa hongo au wanasiasa fulani kuitumia, kwa mfano tuseme, sheria ya kukufuru , kuwafunga wapinzani wao ."
'Waastralia hawatakiwi kuwa na hofu'
Huku wengi wa watumiaji wa mtandao wakiwa na maoni kuwa watu hawapaswi kuwa na hofu, bado kuna hisia za hofu miongoni mwao.
Waastralia wanafahamu fika ni jinsi gani mambo yanaweza kuwa mabaya unapojikuta miongoni mwa mamlaka za Indonesia – hata kwa makosa madogo
Msemaji wa wizara ya sheria ya Indonesia alijaribu kutuliza hofu kwamba hatari ni za kiwango cha chini kwa watalii kwasababu kila mtu atakayewasilisha malalamiko yake kwa polisi huenda uwezekano mkubwa akawa ni rai awa Indonesia "hiyo inamaanisha kuwa watalii wa Australia hawapaswi kuwa na hofu ," Albert Aries alinukuliwa akisema na wavuti wa habari wa Australia -WAToday.com.
Lakini Bali haiwezi kuhimili pigo jingine kwa sekta yake ya utalii. Kujikwamua kwake baada ya janga la Covid – 19 kumekuwa taratibu, na wafanyabiashara wengi na familia bado wanajaribu kurejesha kile walichokipoteza.
Mwaka 2019, idadi ya watalii wa Australia waliozulu kisiwa cha Bali ilirekodiwa kufikia watu milioni 1.23 , kulingana na taasisi isiyo ya kiserikali ya yenye makao yake Perth.
'Kusema ukweli ninategemea utalii'
Muongozaji wa watalii anayeitwa Yoman, ambaye alifanya katika Bali tangu 2017, aliiambia BBC kwamba athari za sheria mpya zinaweza kuwa ..mbaya sana’’ kote nchini Indonesia, lakini hasa katika kisiwa hicho cha mapumziko.
Nina wasi wasi sana, sana , kwasababu ninategemea kusema kweli utalii "," alisema.
Bali ina historia ya matukio – yanayotengenezwa na binadamu na majanga asilia kwa pamoja – hilo limewaathiri wageni wanaotembelea kisiwa hicho.
"Vita vya Ghuba, mashambulio ya mabomu ya Bali, milipuko ya volkano, Mount Semeru (volkano), Volkano ya Mlima Rinjani halafu Covid. Utalii wa Bali unaathiriwa kwa urahisi ," Yoman alisema.
Serikali ya Indonesia imeanzisha juhudi mbali mbali kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inarejea katika hali yake ya awali.
Wiki mbili tu zilizopita, ilitangaza kutoa kibali kipya cha usafiri (visa), kinachowaruhusu watu kuishi katika kisiwa hicho kwa miaka hadi 10.
Na bila shaka ni watalii kutoka Australi ambao wanaweza kuathiriwa.