Kuzuka kwa vugu vugu la watu wasiofua nguo

Indigo Invitational

Chanzo cha picha, Getty Images

Bryan Szabo na wenzake wametumia muda mwingi kutazama picha za suruali ya jeans iliyovaliwa vizuri, ikiwa ni pamoja na nguo za zamani zilizofifia zilizo na kitambaa kilichopauka na ung'avu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuchanika kwenye eneo la goti.

Wamekuwa wakisifiwa sana mitandaoni, kwa kuwa waundaji bora wa suruale za aina hiyo. "Utengenezaji huu wa crotch ni mzuri sana!".

Shindano la Indigo limekuwa kwa muda sasa, ambapo watu kutoka kote duniani huvaa jeans kwa mwaka mmoja bila kufua. Lakini vuguvugu hilo sio la washindani wa jeans zilizo na muundo wa kuvutia duniani pekee.

Wao pia ni mabingwa wa kitu kingine: denim isiyofuliwa mara kwa mara. Kwa kuwa denim inakuwa laini sana ikifuliwa kwa sabuni, ndiposa baadhi ya watu wanapendelea kutofua aina hii ya nguo. Huu ni mkakati huo unafuatwa na kila mtu kutoka kwa wanachama wa vugivugu la no-wash hadi Mkurugenzi Mtendaji wa Levi's.

Indigo Invitational

Chanzo cha picha, Indigo Invitational

Kwa Szabo, mwenendo wa kutofua nguo zake ulianza wakati aliponunua jozi yake ya kwanza ya jeans ghafi ya denim mwaka 2010.

Akisafiri kutoka Canada hadi Ulaya, alibeba jeans yake kwa safari ya miezi sita. "Ilikuwa jambo la ajabu kwangu kwamba nilikuwa na jeans hizi za uvundo," anaiambia BBC Culture.

"Zilikuwa na harufu mbaya." Huko Budapest alikutana na mke wake mtarajiwa, na jeans ikawa gumzo katika uhusiano wao. "Jean zangu zilikuwa kwenye rundo mwishoni mwa kitanda," anakumbuka. "Ukiingia chumbani, unakaribishwa na uvundo[wake]... Nilikuwa na bahati sana kwamba mke wangu alikuwa ananipenda na licha ya mapungufu hayo."

Miongoni mwa washiriki wa shindano la Indigo, ambayo sasa inaingia mwaka wake wa tano, zaidi ya watu tisa kati ya 10 huchukua muda kufua suruali zao mara ya kwanza hadi wazivae mara 150 au 200, Szabo anakadiria.

Baadhi ya marafiki zake huchukuwa muda zaidi kabla ya kufuqa suruale zao, wakifuata kile anachokiita "falsafa ya kutofua kabisa".

Badala ya kuzifua, wavaaji wa jeans humebuni njia zingine za kutunza mavazi yao, kama vile kuzianika juani, Szabo anasema au kuzianika nje usiku kucha.

Szabo mwenyewe hufua surali zake, "Mara tu [mke wangu] anaposikia harufu ya jeans yangu, ananiambia, na bila kupoteza muda wanaingia kwenye shughuli ya kufua."

Mbuni Stella McCartney si shabiki wa kufua nguo mara kwa mara, ingawa bado "ni msafi sana"

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamitindo Stella McCartney si shabiki wa kufua nguo mara kwa mara, ingawa "ni msafi sana"
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sio wavaaji wa Jeans pekee ndio wanaopunguza kufua nguo. Mnamo mwaka wa 2019, wanamitindo Stella McCartney aligonga vichwa vya habari alipoelezea mwenendo wake wa kutofua nguo mara kwa mara: "Kimsingi, sio lazima kufua hasa kama hakuna sababu ya kufanya hivyo. Singebadilishi sidiria yangu kila siku na sio tu kuingiza vitu kwenye mashine ya kufulia kwa sababu vimevaliwa. Mimi mwenyewe ni msafi sana, lakini si shabiki wa kufua nguo mara kwa mara kusema, kweli."

Wengine hutathmini upya tabia zao za kufua nguo kutokana na wasiwasi wa mazingira au kupanda kwa gharama za umeme.

Mac Bishop, mwanzilishi wa kampuni ya nguo ya Wool & Prince, anaielezea Fast Company kwamba alibadilisha mtazamo wake juu ya "urahisi wa mavazi, ambayo ilihusishwa na watumiaji wa kiume - "hasa ​​wale ambao thawakupenda kufua nguo" - ilipoanza kutangaza chapa yake ya wanawake, Wool&.

Kulingana na karne nyingi za utangazaji wa nguo za kijinsia, wanawake hawangekubaliana na wazo la kutofua nguo zao, ilitoa nadharia, na utafiti uliounga mkono, kuonyesha kwamba, pamoja na wanawake, mazingira ni sababu nzuri zaidi ya kutofanya hivyo.

Mmoja wa wateja wa Wool&'s ni Chelsea Harry kutoka Connecticut, Marekani. "Nilikulia katika nyumba ambayo unaosha kila kitu baada ya kutumia mara moja," aliambia BBC Culture.

"Taulo baada ya kutumia mara moja, nguo yako ya kulalia unafua baada ya kuvalia mara moja."

Wakati wa majira ya joto Bi Harry aliishi na bibi yake, ambaye alimfundisha kuweka pajama zake chini ya mto wake anapoamka asubuhi na kuvaa tena usiku uliofuata.

Baadaye, alikutana na mume wake, ambaye, anasema, "aliona ugumu sana kufua nguo yoyote".