Mkutano wa Alaska: 'Kushindwa kwa Marekani na kufaulu kwa Putin'- The Washington Post

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Alaska unaendelea kutawala vichwa vya habari katika magazeti ya Uingereza, Marekani na Urusi.
Katika nakala yake ya Washington Post, mwandishi Max Boot amechukulia mkutano huo kama "kushindwa" kwa Marekani.
Alisema kuwa mkutano wa Ijumaa kati ya Trump na Putin "haukuwa mbaya zaidi, lakini haukuwa mzuri pia, isipokuwa kwa mtazamo wa Kremlin." Mwandishi anaulinganisha mkutano huo na mikutano ya awali iliyofanyika miongo minane iliyopita kati ya marais wa Marekani na mwenzake wa Urusi.
Alibainisha kuwa mkutano wa kilele wa Alaska haukuwa kama mkutano wa kilele wa Helsinki wa 2018, wakati Trump "alipojidhalilisha mwenyewe na nchi yake kwa kukubali hakikisho la Putin kwamba Urusi haikuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016, akipuuza ripoti ya mashirika ya ujasusi ya Marekani ambayo yalithibitisha kinyume."
"Jambo bora zaidi ambalo linaweza kusemwa kuhusu mkutano wa Alaska ni kwamba unaweza hata kuwa mbaya zaidi," alisema.
Lakini mwandishi huyo amesema, "Kama mkutano wa kilele wa Alaska haukuwa janga, basi hakika ulishindwa kutimiza malengo," na akatoa maoni kwamba Putin "aliibuka mshindi wazi katika makabiliano yake ya hivi karibuni na rais wa Marekani."
Alidokeza kuwa "Ushindi wa Putin ulikuwa wazi tangu mwanzo, wakati vikosi vya Marekani vilipopomuwekea zulia jekundu dikteta aliyeshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa uhalifu wa kivita uliotekelezwa mnamo 2023, ambaye hawezi kusafiri kwenda nchi nyingi kwa kuhofia kukamatwa."
Wakati Putin alimsifu Trump na kusema hangewahi kuivamia Ukraine kama angekuwa rais, mwandishi anahoji je ni, "Kwanini Putin ameongeza mashambulizi yake ya ndege zisizo na rubani na makombora tangu kuapishwa kwa Trump?"
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Aliamini kwamba Putin "alifanikiwa kumdanganya" Trump baada ya kuahirisha kuweka vikwazo kwa Urusi ambavyo alikuwa ametishia kabla ya mkutano huo, na kwamba marais hao wawili hawakukubaliana kusitisha mapigano.
Kauli ya Trump kwamba alikuwa amejiunga na ombi lake la kusitisha mapigano na kukubaliana na Putin kuhamia moja kwa moja kwenye mazungumzo ya "makubaliano ya amani ambayo yangemaliza vita" ilitafsiriwa na mwandishi kama "kupunguza shinikizo kwa rais wa Urusi kusitisha mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Ukraine."
Lakini aliona dokezo la Trump, "ambaye ana mtazamo wa kuyumba kwa vita hivi," kwamba angetoa dhamana ya usalama wa Marekani kwa Ukraine kama sehemu ya suluhu ya amani, kama ushindi mkubwa kwa Kyiv iwapo hilo litatokea.
Kwa kuzingatia mtazamo wa Trump wa kuyumba kwa vita vya Ukraine, ni mapema mno kukata tamaa. Trump aliashiria kwa viongozi wa Ulaya baada ya mkutano huo kwamba yuko tayari kutoa dhamana ya usalama wa Marekani kwa Ukraine kama sehemu ya suluhu ya amani. Ikiwa ni kweli, huu utakuwa ushindi mkubwa kwa Kyiv.
Kuimarisha hadhi ya Urusi kama dola kubwa"

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika The Telegraph, afisa mstaafu wa Jeshi la Uingereza Richard Kemp aliandika nakala akitoa wito kwa Ulaya kumwogopa Putin, ambaye "ameanzisha hadhi ya Urusi kama taifa lenye nguvu kubwa"
Mwandishi alisema kuwa mkutano wa Trump na Putin "ulikuwa sawa," kwa sababu vita nchini Ukraine "haviwezi kusimamishwa licha ya zaidi ya miaka mitatu ya juhudi za Magharibi."
"Licha ya vikosi vya Ukraine kuzuia mashambulizi ya Urusi mapema katika vita, ushujaa wao katika mapigano, na mashambulizi yao ndani ya Urusi, Putin bado anaamini kuwa anaweza kuhimili mapigo yoyote ambayo Kyiv itatoa na kwamba anaweza kupata eneo zaidi, wakati vikosi vyake vinaendelea kusonga mbele katika eneo lenye utajiri wa madini la Donbas, ambalo linawakilisha mhimili mkuu wa kijeshi wa Urusi, " mwandishi anaandika.
Alibainisha kuwa Putin "hangependa kuendelea kuipigania Donbas ikiwa angeweza kuipata kwa njia zingine," na akamwambia Trump kwamba "vita vinaweza kumalizika ikiwa Ukraine itajiondoa kutoka asilimia 30 ya Donetsk ambayo vikosi vyake vilikuwa bado havijaichukua."
Lakini Zelenskyy "atasitasita" kukubaliana na matakwa ya Putin, akisema kwamba kuacha kwa hiari eneo lolote la Ukraine kutahitaji kurekebisha katiba, kifungu hicho kilisema.
Mwandishi alisema Zelensky "lazima asawazishe hili na tathmini yake ya kiwango ambacho vikosi vya Ukraine vitaweza kushikilia eneo lao ikiwa vita vitaendelea, na gharama inayowezekana ya vita.
"Tathmini hii italazimika kujumuisha matarajio ya Magharibi ya uwezekano wa amani, na iwapo zitaendelea kuunga mkono juhudi za ulinzi za Ukraine, na kiwango ambacho kitaiwezesha Ukraine kuwa na ufanisi peke yake," alielezea.
Mwandishi alibainisha kuwa Putin "hakutoa chochote kama malipo ya kupata kile anachokihitaji." Anaamini kwa Putini usitishaji wa mapigano kabla ya "makubaliano" haikuwa na maslahi kwake, na usitishaji mapigano amba ni , kipaumbele kwa Magharibi, "haukuchukuliwa kwa uzito" huko Alaska.
Mwandishi anaamini kwamba "licha ya mapungufu ya kijeshi ambayo yamedhihirika tangu kuanza kwa vita, nguvu ya Urusi haiwezi kupuuzwa," akibainisha kuwa "teknolojia za hali ya juu za Magharibi na mbinu za kijeshi hazitoshi kuishinda nguvu ya Putin ."
"Urusi imejifunza masomo ya vita vya kisasa, ikirekebisha vikosi na mikakati yake ya kukabiliana na ndege zisizo na rubani na ubunifu mwingine wa uwanja wa vita kwa njia ambayo Magharibi haijafikia," mwandishi anasema.
Alibainisha kuwa Urusi "inaendelea kudumisha viwango vya kushangaza vya uzalishaji wa silaha, ikiongeza uzalishaji wake na vifaa kutoka Iran, Korea Kaskazini na China." Kinyume chake, Magharibi "imeshindwa au haitaki kuendana na kasi."
Alisema vita vitaendelea isipokuwa Zelenskyy atakapokubali matakwa ya Putin, wakati "Ulaya wameridhika kutazama hatima ya Ukraine—na yao wenyewe."
''Vikwazo" nchini Urusi kumaliza vita
Huko Urusi, Elena Davlekanova aliandika Makala katika The Moscow Times yenye kichwa "Kwa nini ni vigumu sana kwa Putin kumaliza vita vya Ukraine?"
Mwandishi alisema kuwa mkutano huo, ambao haukuleta Ukraine karibu na amani ya kudumu, uliwezesha "kurudi kwa Urusi kutoka baada ya kutengwa kwake kwa kidiplomasia kwa miaka mingi.
Mwandishi anaamini kwamba "Lengo la kimkakati la Putin tangu mwanzo halikuwa kuambatanisha eneo la Ukraine kama bali ni kuanzishwa tena kwa msimamo wa Urusi kama nguvu ya kimataifa na mamlaka kubwa barani Ulaya."
Lakini alisema, "Urusi inapata shida kutenda kama nguvu kubwa na uchumi wa kawaida, kulinganishwa na Italia. Kwa hivyo, suluhisho lake la mwisho ni mradi wa nguvu na silaha zake za nyuklia."
Kwahivyo, kwa Rais wa Marekani kumkaribisha Putin huko Alaska na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov kuvaa fulana yenye mandhari ya Usovieti ilitimiza lengo kuu la Kremlin vizuri. Leo, kuonyesha Urusi kama Dola ya ulimwengu katika ulimwengu ulioundwa na ushindani mkubwa wa nguvu kumerejea kwenye mazungumzo mazito ya kisiasa, mwandishi anabainisha.
Alizungumzia kuhusu "jambo lingine muhimu linalochochea vita: kusita kwa nchi za Magharibi kuweka vikwazo vikali kwa Urusi na kuvitekeleza kikamilifu kufuatia uvamizi wake na kuinyakua Crimea, jambo lililoipa Kremlin muda wa kuelekeza biashara yake." Alibainisha kuwa mapato ya mauzo ya nje ya Urusi yanazidi viwango vya 2015, licha ya vikwazo vya kimataifa.
Matokeo yake , "uchumi wa Urusi umebadilika na sasa unaanza kupungua baada ya miaka mitatu ya ukuaji usio endelevu unaochochewa na matumizi ya serikali. Itaweza kujishikilia kwa muda kabla ya kuanguka," mwandishi alisema, akiongeza kuwa "vikwazo vya pili kwa nchi zinazofanya biashara na Urusi na bei ya chini ya mafuta ndio suluhisho la mwisho la kuhakikisha amani "
Alibainisha kuwa "kikwazo kingine cha kumaliza vita ni masilahi ya kifedha ya wale ambao wamejikusanyia utajiri kutoka kwanjia tata za kijeshi na kiviwanda na urekebishaji wa uchumi wakati wa vita, ambao umeunda tabaka la wanaonufaika ."














