Mwani wa baharini ni tiba ya miujiza au uvumi tu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukitajwa na baadhi kama siri ya ngozi inayong'aa, kupunguza uzito kwa urahisi, na afya bora ya utumbo, mwani wa baharini au mwani wa miiba, unaofahamika kwa lugha ya kiingereza kama Sea Moss unaoliwa umekuwa maarufu miongoni mwa watu mashuhuri pamoja na watumiaji wa TikTokers.
Mitandao ya kijamii imejaa mapishi ya vyakula vyenye mwani wa baharini, vipodozi vya uso vya kutumia DIY, na video za #SeaMossChallenge zimesambaa ambapo washawishi humeza mdomo wa jeli ya mwali wa bahari wenye harufu mbaya.
Lakini je, kuna ukweli wowote nyuma ya madai ya umaarufu wa mwani kuwa bora, au kusaambaa tu kwa taarifa za uvumi kama uvumi mwingine?
Mwani wa baharini ni nini?
Mwani wa baharini pia hujulikama kama moss ya Ireland ni aina ya mwani mwekundu unaopatikana kwa kawaida kando ya mwambao wa miamba ya Ireland na sehemu nyingine za Atlantiki. Pia hukua katika maji ya joto ya Asia, Amerika Kusini, na Afrika.
Kulingana na Baraza la Kimataifa la uboreshaji wa vyakula (Intarnational Food Additives), wanadamu wamekuwa wakivuna na kutumia mwani wa baharini kwa takriban miaka 14,000, na kuna ushahidi wa matumizi ya mwani kama dawa China mapema kama 600 KK.
Mmea huu hutoa nyongeza inayoitwa carrageenan, ambayo watengenezaji wa chakula hutumia kama kimiminika cha kuongeza ukubwa katika bidhaa kama vile ice cream, maziwa ya chokoleti.
Kama mwani mwingine mwani wa bahari una virutubisho vingi, ikiwa ni pamoja na chuma, magnesiamu, iodini na vitamini, ambayo huchangia afya njema kwa ujumla, kulingana na Shirikisho la masuala ya Lishe la Uingereza.
unapatikana kwa wingi mtandaoni katika hali yake mbichi na kavu, lakini bidhaa maarufu zaidi kwenye mitandao ya kijamii ni vidonge, poda, jeli, na gummies.
Soko la kimataifa la moss wa bahari linatarajiwa kuzidi dola bilioni 3 ifikapo 2032, likiztokana na mahitaji makubwa nchini China, kulingana na data za Utafiti wa Soko la Polaris.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ngozi nzuri?
Katika makala kuhusu kudhibiti psoriasis, hali sugu ya ngozi , nyota wakipindi cha masiha halisi cha televisheni Kim Kardashian alishirikisha umma taarifa kwamba anakunywa mwani wa baharini kama sehemu ya lishe inayotokana na mimea.
Lakini sayansi inasema nini?
Mwani wa baharini una vitamini A na E, ambazo, kulingana na taasisi ya Kitaifa wa Afya ya Uingereza (NHS), ni muhimu kwa afya ya ngozi. Pia ina antioxidants, kama vile polyphenols, ambayo ina athari "zilizowekwa vizuri za kupambana na uvimbe wa mwilini (inflammation)", kulingana na NHS.
Leah de Souza-Thomas ni mwanasayansi aliyehitimu wa matibabu anayeishi Uingereza na mwanachama wa Nutritionist Resource, hifadhidata ya wataalamu wa lishe na wataalamu wa lishe waliohitimu. Anasema kwamba kuna "ushahidi mdogo wa moja kwa moja kwamba ulaji wa mwani wa baharini huboresha hali au muonekano wa ngozi."
Uchunguzi unaoonyesha faida za mwani wa baharini kwa ngozi umezingatia matibabu ya juu, kama vile creams, badala ya matumizi, aliiambia BBC.
Kupunguza uzito wa mwili
Utamaduni wa lishe upo sana kwenye TikTok. Mnamo 2022, utafiti wa Chuo Kikuu cha Vermont nchini Marekani ulibainisha video bilioni 9.7 zilizo na kampeni ya kupunguza uzito wa mwili za za mtandaoni -hashtag #weightloss.
Watumiaji wameutaja mwani wa baharini kama chakula bora ambacho husaidia kupunguza uzito, lakini Bridget Benelam, msemaji wa Wakfu wa Lishe wa Uingereza, anasema hakuna ushahidi wa kupendekeza kwamba mwani wa baharini unapaswa kuchukuliwa kuwa chakula bora.
"Tunajua kidogo sana juu ya faida maalum ambazo ulaji wa mwani wa baharini unaweza kuwa na afya ya binadamu," aliiambia BBC.
Mwani una nyuzinyuzi nyingi, ambazi zinaweza kukusaidia kuhisi umeshiba, kulingana na Richelle Isaacs, mtaalamu wa lishe ya tiba asili aliyesajiliwa nchini Uingereza.
Lakini anaongeza kuwa "hakuna ushahidi wa kutosha kwamba unachangia kupoteza uzito."

Chanzo cha picha, Getty Images
Bora kwa utumbo
Mwani, ikiwa ni pamoja na mwani wa baharini , una kiwango kikubwa cha polysaccharides, aina ya kabohaidreti ya prebiotic ambayo ni ya manufaa kwa utumbo.
"Prebiotics ni kama mbolea kwa vijidudu vya utumbo wetu," inaeleza Jumuiya ya Dietetic ya Uingereza. "Kimsingi ni vyakula vinavyolisha bakteria wetu wazuri."
Shule ya Harvard ya Afya ya Umma inabainisha kuwa utumbo wenye afya unahusishwa na faida nyingine, ikiwa ni pamoja na kinga iliyoimarishwa, afya bora ya ubongo, na inaweza hata kupunguza hatari ya ugonjwa wa kisukari.
Bi de Souza-Thomas anakubali kwamba mwani wa baharini umeonyesha "matumaini" kwa afya ya utumbo, lakini aliiambia BBC kwamba "utafiti zaidi unahitajika ili kuelewa kikamilifu jukumu lake."

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatari zinazowezekana
Kuna baadhi ya hatari zinazohusiana na ulaji wa mwani wa baharini, ambazo wataalam walizungumzia na BBC waliangazia.
Una viwango vya juu vya iodini, ambavyo vinaweza kusababisha matatizo ya tezi ikiwa unautumia sana.
"Haupaswi kuzidisha kiasi kilichopendekezwa kwenye kifurushi," Benelam alisema.
Aliongeza kuwa, kama unaweza kunyonya metali nzito kutoka kwa maji, kulingana na mahali ulipopandwa.
Mamlaka ya Usalama wa Chakula ya Ulaya inashauri kwamba mkusanyiko wa metali katika mwili unaweza kuwa na athari mbaya za muda mrefu.
Hata hivyo, Bi de Souza-Thomas anaamini kwamba mwani unaweza kuliwa kwa kiasi kidogo kama sehemu ya lishe bora.
Lakini unaweza kuwa sio tiba ya miujiza watumiaji wa Tiktok wanavyodai.
"Mwani wa baharini unafikiriwa vyema kama nyongeza, badala ya mbadala, kwa lishe anuwai iliyo na mboga mboga, matunda, nafaka ambayo haijachakatwa, protini bora, na mafuta yenye afya," anaongeza de Souza-Thomas.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












