Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.08.2023

Crystal Palace wanapanga kumsajili mchezaji huru wa Ubelgiji Eden Hazard kwa kumpa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, 32, mkataba wa mwaka mmoja huko Selhurst Park licha ya majeraha yake. (Football TransferS)

Brentford wameweka bei ya pauni milioni 80 kwa mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27, huku Arsenal na Tottenham zikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo mwezi Januari mara baada ya kutumikia marufuku yake ya miezi minane kwa kukiuka sheria za kucheza kamari. (tIMES - usajili unahitajika)

Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano na Real Sociedad kuhusu mkopo wa msimu mzima kwa beki Kieran Tierney, 26. (The Athletic - Usajili unahitajika)

The Gunners wameafikiana na Monaco ada ya euro milioni 45 (£38.6m) pamoja na nyongeza kwa mauzo ya mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun, 22. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Manchester United wanakaribia kufikia kandarasi ya mwaka mmoja na Jonny Evans, 35, katika hatua ambayo inaweza kuibua shaka juu ya mustakabali wa beki mwenza Harry Maguire, 30, Old Trafford. (Telegraph - usajili unahitajika)

Klabu ya Albania ambayo haikutajwa jina ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 21, baada mchezaji huyo na United kufikia uamuzi wa kuondoka Old Trafford baada ya uchunguzi wa ndani. (Talksport)

Tottenham wanavutana na Nottingham Forest kuhusu ada ya kumsajili Brennan Johnson, huku klabu hiyo ya East Midlands ikionyesha kuwa haiko tayari kumruhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuondoka kwa kitita cha pauni milioni 40. (Standard)

Chelsea pia wana nia ya kumsajili Johnson na mchezaji huyo anafikiriwa sana Stamford Bridge. (Football London)

Fulham wamemchunguza beki wa Uingereza , 29, kwa lengo la kumsajili kutoka Tottenham baada ya kiungo huyo kuachwa nje ya kikosi cha mkufunzi wa Spurs Ange Postecoglou kwa mechi mbili za kwanza za Ligi ya Primia. (Sky Sports)

Manchester City wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pili kwa Wolves kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes, 24, baada ya dau la kwanza la takriban pauni milioni 47 kukataliwa. (Telegraph - usajili unahitajika)

Lakini City wako tayari kuachana na dili la Nunes ikiwa hawaamini kuwa litawapa thamani ya pesa. (Standard)

Barcelona watamsajili Joao Cancelo kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Manchester City siku chache zijazo lakini hakutakuwa na chaguo la kumnunua beki huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 aliyejumuishwa kwenye mkataba huo. (Marca kwa Kihispania)

Everton wanajadiliana na Udinese kumhusu mshambuliaji wa Ureno Beto, 25, lakini klabu hiyo ya Serie A haitamuuza endapo kifungu chake cha pauni milioni 30 cha kumuachilia hakitafikiwa. (Liverpool Echo)

Kiungo wa wa timu ya taifa ya Morocco Sofyan Amrabat, 27, aliachwa nje ya kikosi cha Fiorentina kwa mechi ya Ligi ya Europa Conference dhidi ya Rapid Vienna baada ya Manchester United na Liverpool kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Sky Sports)

Sheffield United iko kwenye mazungumzo na klabu ya Ufaransa Troyes kuhusu mpango wa kumnunua winga wa Guinea-Bissau Mama Balde, 27. (L'Equipe - kwa Kifaransa).

Dau la Burnley la euro 20m (£17.2m) kwa winga wa PSV Eindhoven Johan Bakayoko limekataliwa na klabu hiyo ya Uholanzi, ambayo imedai zaidi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 20. (Fabrizio Romano)