Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili 20.11.2022
Chelsea itamfuatilia nyota wa Everton na England Jordan Pickford kwenye Kombe la Dunia huku mmiliki Todd Boehly akitafuta mlinda mlango mpya. (Sun on Sunday)
Mchezaji kinda wa Manchester United Alejandro Garnacho yuko mbioni kuongezewa mshahara mnono. Winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 18 anatarajiwa kulipwa £50,000 kwa wiki. (Star)
Chelsea wako tayari kwa fursa iwapo Manchester United itatekeleza mpango wao wa kukatisha mkataba wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37. (Sunday Mirror).
Kiungo wa kati wa Brighton na Scotland Billy Gilmour yuko tayari kuhamia klabu moja ya Ulaya kwa mkopo baada ya kukosa nafasi ya kucheza tangu ajiunge na klabu hiyo ya pwani ya kusini. (Sun on Sunday)
Chelsea wanafikiria kumnunua winga wa Aston Villa, Mjamaika Leon Bailey, 25, ambaye ni rafiki mkubwa wa kiungo Raheem Sterling. (Mail on Sunday)
Baba yake na nyota wa Brazil, Endrick anadai kuwa ni klabu moja tu ya Ulaya ambayo imefungua rasmi mazungumzo na Palmeiras kuhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 16 ingawa hawezi kuhama hadi atakapofikisha umri wa miaka 18. (90Min).
Mshambulizi wa Paris St-Germain Lionel Messi, 35, anaweza kuungana na kocha wake wa zamani Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City ikiwa atashindwa kutwaa Kombe la Dunia linaloanza leo akiwa na Argentina. (El Nacional)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefichua kwamba aliondoka Borussia Dortmund mapema kuliko ilivyopangwa ili kuisaidia klabu hiyo ya Ujerumani kumpata Thomas Tuchel kama mrithi wake. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester City, Bernardo Silva amesisitiza kuwa kutoelewana kwa Cristiano Ronaldo na Manchester United sio kikwazo katika kampeni ya Ureno ya Kombe la Dunia. (Guardian)
Mkufunzi wa zamani wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino ansema kwamba mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, 23, alitaka kuondoka katika klabu hiyo msimu uliopita ili kujiunga na Real Madrid. (Mirror)
Takriban maskauti 35 wa Manchester United kutoka duniani kote wamekutana mjini Manchester kaika mfululizo wa mikutano ya usajili ili kuwa na mbinu ya pamoja zaidi katika usajili. (Football Insider)
Liverpool wamepata msukumo katika kumsaka kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jude Bellingham huku kukiwa na ripoti kwamba wapinzani wao Real Madrid wana kikomo cha juu cha bei ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 19. (Liverpool Echo)
Kiungo wa kati wa Leeds na Poland Mateusz Klich, 33, ana raha Elland Road na anatazamiwa kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari. (Give Me Sport)
Bosi mpya wa Wolves Julen Lopetegui anataka kuleta timu yake ya kuajiri kabla ya dirisha la Januari. (Football Insider)