Kwa nini Simu na 'Laptop' yako ni mgodi wa dhahabu

Chanzo cha picha, Royal Mint
Wakati taka za kieletroniki ( E-Waste) zikiongezeka, Sasa kampuni moja Uingereza inayoitwa Royal Mint imekuja na mbinu mpya ya 'kuchimba' madini ya thamani yaliyofichwa kwenye (Laptop) au kompyuta za mkononi na simu ili kupunguza utegemezi wetu wa malighafi.
Kwa miaka miwili, kampuni hii ya Royal Mint, ambayo ndiyo mtayarishaji rasmi wa sarafu za Uingereza, imekuwa ikisaka njia mpya ya ajabu ya kurejesha madini kutoka kwenye taka za elektroniki.
Kwenye maabara ndogo, Hayley Messenger, Mwanakemia aliyebobea katika madini endelevu ya thamani, anaeleza kwa nini hakuna nyaraka ama mahali palipoandikwa kuhusu hili: "Kila kitu ni siri!" Anasema.
Yeye na timu ya wanakemia na watafiti wengine wa kemikali, pamoja na kampuni ya Excir ya Canada, wamegundua njia safi na kujipa hakimiliki, ambayo wanadai kuwa inatoa 99% ya dhahabu kutoka kwenye saketi zinazopatikana ndani ya kompyuta ndogo na simu za zamani.
Baadaye mwaka huu, Royal Mint inafungua kiwanda kipya chenye thamani ya mamilioni ya dola ambacho kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 90 za majumba ya saketi kwa wiki, mara baada ya kufanya kazi kikamilifu, na kurejesha mamia ya kilo za dhahabu kila mwaka.

Chanzo cha picha, Royal Mint
Suluhisho la kemikali
E-waste (pia inajulikana kama vifaa taka vya umeme na elektroniki au WEEE) ndio mkondo wa taka unaokua kwa kasi zaidi ulimwenguni. Kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, wastani wa tani milioni 50 za taka za kielektroniki huzalishwa duniani kote kila mwaka, zikiwa na uzito zaidi ya ndege zote za kibiashara zilizowahi kutengenezwa. Lakini ni 20% tu za taka hizo husindikwa rasmi, na nyingi hutupwa na ama kupelekwa kwenye maeneo ya kuteketezwa.
Utafiti uliofanywa mwaka jana uligundua kuwa Uingereza ilishika nafasi ya pili kwa kuzalisha kiasi kikubwa cha taka za kielektroniki kwa kila mtu, huku Norway ikiongozana na Marekani ikiwa nafasi ya nane.
Kadiri mahitaji ya vifaa vya mkononi vinavyobebeka kama simu, Laptop na vifaa vya elektroniki yakiongezeka, ndivyo pia mlima wa taka za kielektroniki unavyoongezeka. Mnamo mwaka wa 2019, Jukwaa la Uchumi Ulimwenguni lilikadiria kuwa ifikapo 2050, uzalishaji wa taka za kielektroniki kwa mwaka utakuwa zaidi ya mara mbili na kufikia tani milioni 120.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kama malighafi zote muhimu, dhahabu ni rasilimali isiyo na kikomo, lakini 7% ya dhahabu ya ulimwengu kwa sasa iko kwenye vifaa vya elektroniki ambavyo havitumiki. Kutoa au kupata dhahabu kwneye vifaa vye eletroniki kwa kawaida huhusisha kusafirisha vifaa hivyo kwenda Umoja wa Ulaya au Asia ambapo taka za kielektroniki huyeyushwa kwa joto la juu sana katika mchakato unaotumia kaboni nyingi.
"Tunataka kurejesha madini ya thamani kadiri tuwezavyo kutokana na vitu ambavyo kwa sasa vimeharibika ama havitumiki," anasema Messenger. "Lengo letu ni kufanya hivi kwa uendelevu ndani ya Uingereza, kwa kutumia mchakato ambao ni mzuri kwa joto la kawaida huku tukitoa uzalishaji mdogo wa gesi chafu kuliko kuyeyusha."
Kwa sababu taka nyingi za kieletroniki zisizo za dhahabu huondolewa mwanzoni mwa mchakato, uchakataji wa kemikali hutumika tu kwa vipande vya taka zakieletroniki vilivyo na dhahabu, kama Baker anavyoeleza.
Malighafi inayotumiwa na Kampuni ya Royal Mint inajumuisha bodi za saketi, badala ya kompyuta nzima au simu nzima za rununu au mkononi. Mara tu dhahabu inapotolewa, mabaki ya taka zisizo za dhahabu zote hupelekwa kwenye sehemu tofauti kwa ajili ya matumizi mengine, kwa hivyo hakuna kitakachoharibika.

Chanzo cha picha, Carl Wilson
Ingawa kwa sasa, kiwanda cha kuchakata taka cha Royal Mint kinajishughulisha tu na kuchakata dhahabu kwa kiwango kidogo, matarajio ni huko baadae kuchakata na kurejesha madini mengine ya thamani kutoka kwa malighafi za saketi au kieletroniki.
Kate Hinton, anaongoza Shirika lisilo la kiserikali la katika Material Focus, linaloendesha kampeni ya Recycle Your Electricals, anadokeza kuwa kaya za Uingereza zinahifadhi vifaa vya umeme vya zamani vipatavyo milioni 527, ikiwa ni pamoja na kompyuta ndogo za zamani milioni 31, zenye uzito wa karibu tani 190,000.
Nchini Marekani, simu za mkononi au za rununu zenye thamani ya $60m (£47m) za dhahabu na fedha hutupwa kila mwaka. Ripoti ya mwaka 2022 ya Maabara ya Kitaifa ya Lawrence Berkeley ilionyesha kwamba zaidi ya vifaa vya kielektroniki bilioni moja vinaweza kutupwa kila mwaka nchini Marekani muongo mmoja kuanzia sasa - na kwamba vifaa hivyo vya kielektroniki vinaweza kuwa chanzo cha takriban nusu ya kiasi cha dhahabu ambacho kinachimbwa huko kwa sasa.
Kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo, madini yalitolewa kutoka kwenye simu milioni sita za rununu na karibu tani 72,000 za taka za kielektroniki na kutengeneza medali 5,000 za dhahabu, fedha na shaba.
Tani 155,000 za taka ndogo za umeme hutupwa kila mwaka, anasema Hinton, ambaye anataka kuona urejeshaji wa taka za kielektroniki unakuwa jambo la kawaida kwa kijamii.

Chanzo cha picha, Getty Image
Ubunifu unahitajika ili kufanya urejeshaji na kuzichakata upya taka za kielektroniki kuwa njia kuu, anasema Hinton. "Hasa kwa vifaa vidogo vya umeme, kama vile chaja, 'plugs' na nyaya ambazo zimejaa shaba. Ingawa Kampuni ya Royal Mint inafanya vizuri, dhahabu ni sehemu ndogo sana ya mengi yanayopatikana.
Fomula ya siri ya kemikali ya Royal Mint ina uwezo wa kurejesha madini mengine ya thamani kando na dhahabu, kama vile paladiamu, fedha na shaba kutoka kwenye taka za kielektroniki na katika siku zijazo, hizi zinaweza kutumika kutengeneza bidhaa zingine nyingi kando na vito.












