Sologamy:Unajua kuna umuhimu wa 'kujioa'mwenyewe?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo 2011, wanawake 10 huko Bilbao, Uhispania, walikusanyika ili kutangaza hadharani kujipenda kwao na kujioa wenyewe.
Ilianza kama kitendo cha kufurahisha, cha uasi dhidi ya ndoa ya kitamaduni, lakini kwa kweli, walikuwa wakiingia kwenye jambo ambalo tayari linaendelea ulimwenguni. Inaitwa sologamy.
Ndoa ya kitamaduni sio tena lengo kuu kwa baadhi ya wanawake. Badala yake, wanachagua kujitolea kujipenda wenyewe kabla ya wengine.
Je, kujipenda huku kumepitiliza au ni mabadiliko mapya ya kushangaza kwenye hadithi ya zamani?
Huyu ni May, anakaribia kula upya kiapo chake chake cha harusi. Ameishi katika ndoa kwa miaka 11, siri ni ‘kujioa’ mwenyewe.
‘’Nilijiahidi kujisikiliza na kila siku kujiuliza nataka nini na kujipatia kitu hicho. Niliacha kutafuta nje kitu ambacho tayari ninacho ndani yangu’’
Huenda hujawahi kusikikia neno kujioa mwenyewe kwa kiingereza sologamy.
Ukweli ni kwamba neno hili halipo katika lugha rasmi ya Kihispania.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hadi siku ya harusi ndipo tuligundua tunafanya kitu muhimu, anasema May.
''Nilifikiri najipenda, kwamba kila wakati najitunza, lakini ule wakati nilijiahidi mwenyewe mbele ya watu mia moja, kwamba nitajipenda, nitajitunza na kujipatia kipaumbele niligundua kwa hakika sikujipenda.
''Kujipenda na kujiheshimundio mwanzo mpya kwa kila mtu bila kujali jinsia’’ ,anasema Neus Tur Bujosa mtaalamu wa masuala ya jinsia.
Bi Bujosa pia anasema kuwa mwanamke haifai kuwa kizingiti akiongezakuwa wanaume tayari wamelelewa kujipenda lakini – ''sisi wanawake hatuoni umuhimu wa kujipenda vile tunavyoonyesha upendo kwa wengine''.
Profesa wa Saikolojia, Esperanca Bosch Fiol wa chuo cha UIB anasema kujipenda kunasaidia kwanza kutupatia nafasi duniani na pili kuwa na uamuzi mzuri wakati linapokuja suala la kuamua ni nani anastahiki upendo wetu na ni nani hafai.
Nchini Uhispania, wenzi wa ndoa wa jinsia tofauti bado wanaongoza.
Sasa watu hawaona sana na idadi ya wanaotalakiana inaongezeka isopokuwa kwa wanawake kama Juncal ambaye aliamua kuolewa mara mbili kwa mume wake na kujioa mwenyewe.
‘’Nilaimua kujioa mwenyewe kwa sababu binti yetu mdogo ndio mwanzo alikuwa amezaliwa, na mara nikajipata sina muda wa kujipenda. Niligeuka kuwa mama na mke na upendo wote nimeelekeza mtoto na baba yake,’’ anasema Juncal Alzugaray Zurimendi.
Mume wake Sergio Ibarguen Garay anasema Juncal alipomwambaia anataka kujioa mwenyewe kwanza nilipatwa na mshangao kwa sababu sio jambo la kawaida.
''Lakini nilifahamu kuwa yeye ni mtu binafsi na ikiwa hajipendi huenda hafurahii mazingira yanayomzunguka basi hilo litaniathiri mimi,watoto wake na watu wanaomzunguka na hivyo ndivyo nilivyomuelewa mwanzoni.''.

Chanzo cha picha, MARRY YOURSELF VANCOUVER
Miongo kadhaa iliyopita ili kufungua akaunti ya benki au kupata leseni ya kuendesha gari wanawake walitakiwa wawe wameolewa kanisani lakini hili sasa limebadilika.
Licha ya hayo familia imeendelea kuwa nguzo ya jamii yetu na bado inachukuliwa kuwa hali ya asili ya watu.
Katika visa vingi ndoa za kawaida zimekuwa kama jela kwa baadhi ya wanawake. Hii ni kwasababu tumeambia lengo letu la kwanza ni kutunza familia.
Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu nchini Uhispania mwaka 2010 ndio ilikuwa mwisho wa kuatikana kwa data inayoangazia muda unaotumiwa na wanawake kufanya shughuli za nyumbani. Takwimu zilionyesha kuwa wanawake walikuwa wakitumia saa mbuli zaidi kufanya kazi za nyumbani ikilinganishwa na wanaume.
Sologamy ni nini?
Sologamy ni tendo la kujioa mwenyewe katika sherehe ya hadhara, pia inajulikana kama ndoa ya kibinafsi au ndoa ya mtu mmoja. Ingawa ndoa kama hiyo haina kibali au hadhi ya kisheria, sherehe hiyo ya mfano hutumiwa na wengi kama tendo la kusisitiza kujipenda na kujitegemea.
Sologamy ilianza lini
Mtindo huu kujioa mwenyewe ilianzishwa na Linda Baker, daktari wa meno kutoka Marekani, ambaye alijioa mwenyewe mwaka wa 1993.
Inachukuliwa kuwa tendo la kwanza la ndoa ya kibinafsi ambalo lilihudhuriwa na marafiki 75 wa Baker, ambapo bi harusi aliamua kufanya hivyo ''ili kujiheshimu katika ugonjwa na afya hadi siku ambayo ataaga dunia.''
Je Sologamy itabadili maisha ya ndoa?
Baadhi ya wataalamu wa masuala ya jinsia wanasema kujuioa mwenyewe hakutabadilisha chochote ni kisingio cha kujivinjari tu kwa wale wanaoamnua kukumbatia aina hii ya upendo na haina msingi wowote wa kusuluhisha hali zinazowakumba wanawake katika jamii.









