Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Wachezaji wa Tottenham kupunguziwa mishahara iwapo timu yao itashushwa daraja
Wachezaji wa Tottenham wanakabiliwa na kupunguzwa kwa mishahara kwa lazima ikiwa klabu hiyo itashushwa kutoka Ligi ya Premia hadi katika ligi ya Ubingwa. (The Athletic - Subscription Required)
Inter Milan wanavutiwa na mlinda lango wa Liverpool na Brazil Alisson, 33, huku Juventus pia wakimtaka. (La Repubblica - Subscription Required in Italy)
Manchester United wanamtaka nahodha wa Newcastle Bruno Guimaraes, 28, kuchukua nafasi ya kiungo Casemiro msimu huu wa joto - huku kiungo huyo wa kati wa United mwenye umri wa miaka 34 akimuidhinisha mchezaji mwenzake wa Brazil. (AS)
Beki wa Spurs Micky van de Ven hana nia ya kuongeza mkataba wake na klabu hiyo inayofanya vibaya huku Barcelona na Real Madrid wakimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24, kwa ajili ya uhamisho wa majira ya joto. (Nipe Sport),
Bayern Munich wataelekeza mawazo yao kwenye kandarasi mpya kwa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, baada ya mlinzi wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, kutia saini mkataba mpya mwezi uliopita. (Fabrizio Romano)
Liverpool, Arsenal na Barcelona zote zinamfuatilia beki wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 26 Alessandro Bastoni. (Caughtoffside)
Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili Leon Goretzka wa Bayern Munich mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto huku kiungo huyo wa kati wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 akitamani kucheza Ligi ya Premia licha ya kutakiwa na Inter Milan, Juventus na AC Milan. (Christian Falk vianBayern Insider)
Barcelona wako tayari kuilipa Manchester United ada wanayotaka kubadilisha uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa England Marcus Rashford kuwa wa kudumu. (Mirror)
Manchester City wanataka kumsajili tena Lukas Nmecha kutoka Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliachiliwa na City miaka mitano iliyopita bila kucheza Ligi ya Premia lakini anasakwa na Pep Guardiola. (Target)
Manchester United wamemuongeza mkufunzi wa Borussia Dortmund Niko Kovac, 54, kwenye orodha yao ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu. (Football Insider)
Real Madrid wako katika kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, kutoka Borussia Dortmund kutokana na uhusiano wao wa kirafiki na klabu hiyo ya Bundesliga. (AS - Spanish,
Kocha wa Arsenal, Nicolas Jover, anapokea bonasi kila timu inapofunga kutokana na hali mbaya ya mpira. (Times - Subscription Required)