Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Ronaldo kucheza Brazil? Apokea nono

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mshambuliji wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo, 40, amepokea ofa kutoka kwa klabu ya Brazil ambayo haijafichuliwa, ambayo ingemruhusu nyota huyo wa Ureno kucheza Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa litakaloanza Juni. (Marca - kwa Kihispania)

Aston Villa inavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres, 25, na ipo tayari kutoa takriban euro milioni 50 (£42m) kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Mundo Deportivo)

Manchester United imewasilisha ofa ya euro milioni 65 kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, ambaye amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. (Fichajes)

Winga wa Lyon mwenye umri wa miaka 21 Mfaransa Rayan Cherki, anayewaniwa na Manchester United na Liverpool, amethibitisha kuwa ataondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu wa kiangazi. (Goal)

Manchester United pia inataka kumsajili kiungo wa Sporting na Ureno Pedro Goncalves, 26, msimu huu wa kiangazi. (Team talk)

Atletico Madrid ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtaka kiungo wa kati wa Aston Villa Muargentina Enzo Barrenechea, 23, ambaye anakipiga Valencia kwa mkopo. (Birmingham Mail)

Bayern Munich ina matumaini ya kusalia na winga wa zamani wa Manchester City Leroy Sane huku kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kumalizika mwezi ujao. (Bild - kwa Kijerumani)

Nottingham Forest ina nia kuwapa mkataba mpya wachezaji wawili wa Uingereza, kiungo Morgan Gibbs-White, 25, na winga Callum Hudson-Odoi, 24, haraka iwezekanavyo. (Football Insider)

Napoli inamsaka kiungo mshambuliaji mpya kwa ajili ya msimu ujao na inapanga kumsajili mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 25, au mshambuliaji wa Liverpool wa Uruguay Darwin Nunez, 25. (Calciomercato - kwa Kiitaliano).

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi