Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Rashford atapunguziwa mshahara kwa kuhama Barca
Mshambuliaji Marcus Rashford afurahia kupunguziwa mshahara ili kupewa fursa ya kuhama Manchester United kwenda Barcelona, Arsenal wapania kumchukua Jakub Kiwior kutoka Napoli, AC Milan wakataa ofa ya Manchester City kwa Tijjani Reijnders.
Mshambulizi wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Aston Villa, yuko tayari kupunguza mshahara wake ili kuhamia Barcelona msimu wa joto. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona wanataka kumchukua Rashford kwa mkopo kutoka Manchester United mara ya kwanza lakini wakiwa na chaguo la kumnunua. (Sport - in Spanish)
Mlinzi wa Arsenal na Poland Jakub Kiwior, 25, atafuatiliwa tena na Napoli msimu huu lakini klabu hiyo ya Serie A inataka The Gunners kupunguza dau lao la £30m. (Calciomercato - in Italian)
Manchester United haitamfuta kazi kocha Ruben Amorim hata kama watapoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Tottenham. (Mirror)
Manchester City wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 180 kwa winga wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 22, na kiungo wa kati wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26. (Mirror)
AC Milan wamekataa ofa ya £50.4m kutoka kwa Manchester City kwa ajili ya Reijnders. (Teamtalk)
Bayer Leverkusen na beki wa kulia wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 24, amekubali kandarasi ya miaka mitano na Liverpool. (Talksport)
Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, amekataa ofa ya kandarasi mpya katika klabu ya Bayern Munich huku akihusishwa na vilabu vya Primia League na La Liga. (Sky Germany - in German)
Kipa wa Aston Villa Emiliano Martinez anaonekana kukaribia kuondoka katika klabu hiyo huku Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 32 akipokea ofa kutoka Saudi Arabia na timu mbili za Ulaya. (Mundo Albiceleste - in Spanish)
Martinez na familia yake wametua Birmingham lakini anataka kuhama ili kushinda mataji zaidi. (Ole - in Spanish)
Aston Villa wanamfuatilia Caoimhin Kelleher wa Liverpool kama mbadala wa Martinez lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea, Newcastle United na Bournemouth kumnunua mlinda lango huyo wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 26. (The I)
Kipa wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 24, pia anawindwa na Aston Villa. (Fabrizio Romano)
Mshambulizi wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr, 24, analengwa na vilabu kadhaa vya Saudi Arabia kwa ofa ya £210m (euro 250m) dau ambalo linaaminika kuwa mezani. (Fichajes - in Spanish)
Newcastle United wako tayari kutumia £150m kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi wakiwa na winga wa kulia, mshambuliaji na kipa ambaye ndio kipaumbele kwenye orodha ya kocha Eddie Howe. (Newcastle Chronicle)
Kocha wa zamani wa Al-Nassr Luis Castro alikataa fursa ya kuchukua mikoba ya Corinthians ya Brazil huku Mreno huyo, 63 ,akielekea katika Ligi ya Primia. (Foot Mercato - in French)