Wanaanga wanakula nini wakiwa angani?

Tangu binadamu kufika mwezini mwaka 1972 chakula cha wanaanga kimeboreka kwa kiasi kikubwa kwa miongo kadhaa ili kuruhusu milo mbalimbali na yenye afya ambayo haitofautiani sana na milo iliyotayarishwa kwenye sayari ya Dunia.
Lakini umewahi kujiuliza wanaanga wanakula nini angani siku hizi?
Wanaanga Saba wa Mercury kama John Glenn walitumia lishe ya poda iliyokaushwa iliyogandishwa na kidonge kinachoweza kuliwa kupitia mirija.
Wanaanga wa Apollo walipiga hatua zaidi kwa kutumia maji moto na vyombo vya plastiki ambavyo vingeweza kufunguliwa ili kuwezesha kula kwa kijiko.
Siku hizi, zaidi ya bidhaa 100 kama vile samaki, pasta, nyama na chokoleti za brownies zinaweza kupatikana kwenye menyu ya Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), huku milo ikiweza hata kubinafsishwa kwa wanaanga binafsi.
Mwanaanga wa ESA Samantha Cristoforetti alikua mtu wa kwanza kutengeneza kahawa ya espresso angani mwaka wa 2015, naye mwanaanga wa Uingereza Tim Peake akitengeza mlo wa kwanza wa bacon kwenye kituo cha Kimataifa cha anga za juu, ambayo alipokea mwanzoni mwa misheni yake ya Principia mwaka huo huo.
Wanaanga walio katika safari ndefu ya kwenda Mars, Mwezini au sayari zingine watalazimika kukabiliana na viwango vya juu vya mionzi, kudhoofika kwa misuli, mifupa iliyovunjika, mafadhaiko na uchovu.
Lakini kuongeza kwa hili, wangeweza pia kukabiliana na matatizo ya kula.

Chanzo cha picha, NASA
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Kihistoria, wanaanga wamepungua uzani wa mwilli wakati wakiwa safarini," anaelezea Dk Scott Smith, mkuu wa maabara ya lishe ya biokemia ya NASA.
"Tunajua kwamba ikiwa unapoteza uzito wakati wa safarini, utapoteza nguvu ya mfupa na misuli zaidi, mfumo wako wa moyo na mishipa huharibika, na uharibifu mwingine wa mfumo wa mwili unakuwa juu."
Smith anaamini kuwa shida iko chini ya mvuto. “Wahudumu wengi wameripoti kuwa wanajisikia vizuri kwenye obiti, yaani wanakula mpaka wanashiba. Lakini wanapoteza uzito wa mwili. Tunafikiri hii inaweza kuhusishwa na ishara kutoka kwa ubongo inayoambia tumbo lako limejaa inaweza kuwa tofauti angani. kwa sababu chakula kinaweza kushtua tumboni kama inavyofanya duniani."
Mvuto sio tatizo pekee. Kwa safari ndefu kwenda Mars, kwa mfano, wafanyakazi wanaweza wasiweze kubeba chakula chote wanachohitaji, kwani hii ingechukua uzito na nafasi nyingi sana. Pia hawangeweza kutegemea usafirishaji wa kawaida kutoka duniani.
Tatizo hili linahitaji kusuluhishwa kupitia njia ya kukuza chakula katika anga za juu. Lakini kukua kwa mazao ni vigumu katika anga hizo.

Chanzo cha picha, ESA
"Joto baridi, viwango vya mionzi na nguvu ya chini ya uvutano inamaanisha kuwa aina fulani ya uzio inahitajika kukuza mimea, na virutubishi vya msingi, gesi na maji lazima vitolewe," anasema James Bevington wa Chuo Kikuu cha New South Wales, ambaye anaongoza timu ya wanasayansi wakijaribu jinsi ya kupanda mazao kwenye ISS.
"Kwenye Mwezi na Mirihi, unaweza kutumia vyanzo vya ndani kama vile barafu kwenye volkeno au chini kidogo ya uso kusambaza maji, hata hivyo kuyeyuka kwa barafu na kuunda nafasi ya joto kukuza mimea inachukua nguvu nyingi kwa hivyo unahitaji mfumo wa nguvu."
Uchunguzi pia unaonyesha kuwa nafasi inaweza kudhoofisha kinga ya mimea, kitu kinachoonekana na wanaanga pia.
Timu ya Bevington inazindua moduli ndogo ya ukuaji wa mmea wa 10x10x10cm kwenye dhamira ya ugavi wa SpaceX Falcon 9 kwa ISS tarehe 28 Juni 2018.
Wanasayansi wanapanga kukuza mazao yaliyobadilishwa vinasaba kama dhibitisho la majaribio ya dhana.
"Mwishowe, tunafikiri transgenics inaweza kuundwa ili kushinda baadhi ya changamoto za kukua mimea angani," anasema Bevington.
"Kwa mfano, unaweza kufikiria mmea ambao umeboresha kinga ukiwa angani, au mmea unaotoa vitamini ambayo ingekuwa vigumu kupata."
NASA pia inachunguza eneo hili kwa kutumia Mfumo wao wa Uzalishaji wa Mboga (Veggie), kitengo cha ukuaji wa mimea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Chanzo cha picha, NASA
Hata hivyo, mavuno ya mazao ni ya chini ikilinganishwa na mimea iliyopandwa ardhini, labda kwa sababu zunazootkana na kitu kinachofahamika kitaalamu kama Microgravity kinaweza kusababisha usambazaji usio sawa wa oksijeni na maji kupelekwa kwa mimea.
"Nadhani ni muhimu kufikiria juu ya kukuza mimea badala ya kukuza chakula cha kutosha ili kuendeleza wanadamu," anasema Bevington.
"Ni rahisi kulima nyanya chache katika katika shamba lako dogo, lakini kukuza shamba kubwa la kutosha ili kuondoa hitaji lako la kwenda dukani ni vitu viwili tofauti."
Wanasayansi wengine wanaliangalia tatizo hilo kwa mtizamo tofauti.
Timu kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Pennsylvania hivi majuzi walionyesha kwamba wanaweza kubadilisha kinyesi cha binadamu - mkojo na kinyesi - kuwa chakula.
Walilisha kinyesi bandia kwenye kiyeyezi kilichojaa bakteria, ambayo ilivunja mabaki ya viumbe hai katika mchakato sawa na kile kinachotokea kwenye matumbo yetu.
Utaratibu huu hutokea anaerobically (bila oksijeni) na kusababisha methane na carbon dioxide kuzalishwa.
Baada ya kuchujwa na kusafishwa, methane hiyo hulishwa ndani ya mtambo wa pili uliojaa bakteria ambao huzila.
Bakteria zinazokuzwa kwenye kinu cha pili huwa chakula cha wanaanga.
Ingawa wanasayansi hawakuonja bidhaa ya mwisho, inazingatiwa kwa matumizi ya binadamu.

Chanzo cha picha, NASA
"Viumbe vingine vyenye seli moja, kama vile hamira na mwani, vimetumiwa na wanadamu kwa maelfu ya miaka," anasema Lisa Steinberg, mtafiti aliyeongoza utafiti huo.
"Mlo wa kimsingi wa mimea umependekezwa kwa safari ya muda mrefu ya anga, ikiongezewa na vyanzo vya protini ikiwa ni pamoja na wadudu na pengine samaki.
"Vyakula vya bakteria tulivyounda vina protini na mafuta mengi, ambayo hayapatikani kwa wingi kwenye mimea ukilinaganisha na wanyama.
Kwa hivyo hii itakuwa nyongeza nzuri kwa lishe inayotokana na mimea."
Kwa hivyo badala ya pakiti za chakula ambazo hazina maji mwilini, wanaanga wa siku zijazo kwenye sayari ya Mars wanaweza kufurahia kula bakteria wanaolishwa kutokana na kinyesi, wadudu wanaotambaa mimea mingine maalum.
Ingawa inaonekana kuwa si ya kawaida hata kidogo, mradi tu wahakikishe wanakula chakula cha kutosha, lishe hii bora na yenye virutubisho inaweza kuwakimu nanakuwatosheza kiafya katika miezi kadha mirefu ya safari yao.














