Israel na Wahouthi: Je, makabiliano yao yamefikia kiwango hatari?

Chanzo cha picha, EPA
Katika jibu la hivi punde la Israel dhidi ya kuendelea kwa mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya Tel Aviv, Israel imepanua shabaha yake katika mkoa wa Hodeidah wa magharibi mwa Yemeni, ikilenga kile ilichosema kuwa ni maeneo na vituo vinavyotumiwa na wanamgambo wa vuguvugu hilo lenye mafungamano na Iran kwa madhumuni ya kijeshi.
Maeneo mapya yaliyolengwa ni pamoja na "vituo vya umeme vya Al-Hali na Ras Katneeb, pamoja na matangi ya mafuta katika bandari ya Ras Issa, na maeneo karibu na bandari ya Hodeidah," kulingana na shirika la habari la Saba linaloendeshwa na Houthi.
Idadi ya awali ya hasara za binadamu ilikadiriwa kuwa watu watano waliofariki na wengine 44 kujeruhiwa, wakati vyanzo vya Houthi havikufichua hasara ya nyenzo, ambayo inaaminika kuwa dola milioni kadhaa, sawa na ilivyotokea katika mashambulizi ya awali.
Makumi ya ndege za kivita zilishiriki katika uvamizi huu, kwani mamlaka ya Israeli ilikuwa na nia ya kuchapisha sehemu za video za wakati wapiganaji hawa walipotoroka kwenye moja ya vituo vyake vya anga.
Kuchapisha picha hizi kando ya matukio ya mioto mikubwa iliyosababishwa na uvamizi wake inaonekana kuwa kitendo cha kimakusudi na kilichokadiriwa ndani ya mfumo wa vita vya kisaikolojia, na kutuma ujumbe kwa Houthis kwamba wanapaswa kufikiria uwezekano wa matukio yaleyale kutokea tena katika maeneo mengine muhimu ndani ya eneo la kijiografia linalodhibitiwa na Houthis kaskazini magharibi mwa Yemen.
Kwa hakika, hii inaweza kuwa pana na kuharibu zaidi na kudhuru uwezo wa Wahouthi wenyewe.
Hata hivyo, kutokana na kile Wahouthi walichojifunza kutokana na shambulio la awali la Israel dhidi ya Hodeidah Julai mwaka jana, huenda waliweza kuhifadhi mafuta ya akiba katika maeneo mengine kando ya ghala zile zile za mafuta na vifaa vingine ambavyo Israel ililenga Jumapili alasiri kwenye bandari ya mafuta ya Ras Isa ambayo ilikuwa bandari kuu ya kusafirisha mafuta yaliyozalishwa katika maeneo ya mafuta ya jimbo la Marib kaskazini-mashariki
Isipokuwa uharibifu wa ghala za mafuta katika bandari ya Ras Isa, maeneo mengine ambayo Israeli ilichagua kulipua, kama vile uwanja wa ndege wa Hodeidah, ambao haujatumika tangu kabla ya vita nchini Yemen, na vile vile vituo vya umeme vya Hali na Ras Katneeb, hakika havitakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa vita unaoendeshwa na Wahouthi, au kutafakari moja kwa moja juu ya juhudi zao za vita.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini kilicho wazi, kulingana na ripoti kutoka Hodeidah na maeneo mengine yanayodhibitiwa na Wahouthi, ni kwamba kulengwa hivi karibuni kwa akiba ya mafuta kutaongeza mateso ya idadi ya watu na maisha ya kila siku kwa ujumla, na kusababisha shida kubwa ya mafuta na ongezeko kubwa la mahitaji, kwa bidhaa zinazotokana na mafuta, na kwa bei ya juu, ambayo itawaelemea raia wa nchi hiyo ambayo imesambaratishwa na vita kwa muongo mmoja.
.Swali la msingi hapa linahusiana na hatua zinazowezekana za kuongezeka kwa vita ikiwa Israeli na madola ya Magharibi yatajibu kwa ukali zaidi mashambulizi ya Houthi dhidi ya Israeli na kwenye njia za kimataifa za meli katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden.
Kwa kuzingatia matamshi ya Israeli, kuna uwezekano mkubwa kwamba Israeli itatoa, angalau katika siku zijazo, jibu la moja kwa moja na la haraka kwa shambulio lolote la Houthi dhidi ya Israeli.
Kuhusu mashambulizi ya Houthi kwenye njia za meli za baharini, msimamo wa Marekani kuhusu suala hili ulionyeshwa na zaidi ya afisa mmoja wa kijeshi na kisiasa huko Washington, kwamba "Marekani itaimarisha uwepo wa vikosi vyake katika eneo hilo, na itajibu kwa nguvu shambulio lolote la Houthi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Faida na hasara
Katika pande zote mbili za mzozo wa ndani nchini Yemen, idadi kubwa ya watu wanapinga kushambuliwa na Waisraeli au Wamarekani na Waingereza katika eneo la nchi yao, na wanaamini kuwa kituo chochote muhimu cha kiraia ambacho kinalengwa kinaidhuru tu moja kwa moja na sio Wahouthi. Zaidi ya hayo, vituo hivi ni vya Wayemen wote na si ya Wahouthi, hata kama waasi hao watajaribu kuzitumia kwa maslahi yao na madhumuni ya kijeshi yanayohusishwa na kile kinachoitwa "Mhimili wa Upinzani" unaoungwa mkono na Iran.
.Wakati huo huo, vyama kadhaa vya kisiasa vya Yemen vinathibitisha kwamba kulaani kwao mashambulizi ya Israel dhidi ya miundombinu ya raia huko Hodeidah hakumaanishi mwisho wa vita vyao na migogoro ya kijeshi na kisiasa na Wahouthi.
Wakati huo huo, duru nyingine zinahoji ufanisi wa mashambulizi ya Wahouthi na majibu ya Israeli kwao. Kwa maoni yao, "mashambulizi ya Houthi hayawezi kuzuia uchokozi wa Israeli dhidi ya Gaza na Lebanon, wala majibu ya Israeli hayawezi kuwadhuru Wahouthi," kulingana na maoni ya duru hizo.
Ni vyema kutambua kwamba Bandari ya Ras Issa ni mojawapo ya bandari tatu katika Mkoa wa Al Hudaydah, ambayo ni pamoja na bandari ya kibiashara ya mji mkuu wa mkoa, pamoja na bandari ya kibiashara ya Al Salif, ambayo hapo awali ilikumbwa na mashambulizi makubwa ambayo yalisababisha vifo vya raia na majeraha miongoni mwa baadhi ya wanamgambo Waoputhi kutoka kwa walinzi wa bandari, pamoja na hasara ya nyenzo inayokadiriwa kuwa zaidi dola milioni tano.
.Ni vyema kutambua katika suala hili kwamba viongozi wa Magharibi na Israel wamechanganyikiwa sana kuhusu jinsi ya kukabiliana na mashambulizi ya Houthi, hasa kwa vile wanatoka katika nchi ambayo inakabiliwa na hali ya mgawanyiko mkubwa wa kisiasa na kijamii.
Hatua zozote za kijeshi zenye ufanisi zaidi dhidi ya kundi la Houthi zinaweza kuonekana kama adhabu ya pamoja kwa Wayemeni wote, wawe ni wakaazi au la katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hili lenye silaha, na itazuia nafasi ya kufikia suluhu la amani la kisiasa kwa mzozo wa kudumu nchini humo.
Asili ya Yemen inasimama pamoja na Houthis
Wamarekani na Waingereza wanathibitisha kwamba majibu yao kwa mashambulizi ya Houthi yalihusu tu kulipua majukwaa na maeneo ya kurushia makombora na ndege zisizo na rubani na kuzuia baadhi yao, wakilenga tu kudhoofisha uwezo wa Wahouthi wa kurusha makombora zaidi , lakini Wahouthi waliendelea na mashambulizi.
Hakuna njia ya kujua kwa usahihi uwezo halisi wa kijeshi ambao Wahouthi wanamiliki kwa sasa, kwasababu mapango ya milima kaskazini mwa nchi hiyo yanawakilisha ngome za asili za kujificha, na kuficha silaha nzito na risasi, ikiwa ni pamoja na maeneo ya utengenezaji wa makombora na droni.
Serikali ya sasa inayotambulika kimataifa imelaani mashambulizi ya hivi majuzi ya Israel dhidi ya Hodeidah, na katika taarifa yake ilisema Israel inawajibika kwa "athari zozote zinazotokana na mashambulizi yake mapya ya anga, ikiwa ni pamoja na kuzidisha mzozo wa kibinadamu unaozidishwa na mashambulizi ya kigaidi ya wanamgambo wa Houthi kwenye vituo vya mafuta na meli za kimataifa .
Hatahivyo, Iran daima imekuwa ikikanusha kwamba inaunga mkono vita vyote vya Houthi ndani na nje ya nchi.
Licha ya ushahidi wa kuhusika kwake, pamoja na Hezbollah ya Lebanon, katika kujenga silaha za makombora za Houthis, kuongeza idadi ya ndege zao zisizo na rubani, na kuendeleza viwanda vyao vya kijeshi, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alisema katika mahojiano na waandishi wa habari hivi karibuni huko New York, Marekani kwamba "hawatusikilizi."
Hatahivyo, ziara nyingi za safari za baadhi ya viongozi na wawakilishi wa vuguvugu la Houthi kwenda Tehran, Baghdad, Damascus na Beirut zinathibitisha, kama viongozi wa kundi hilo wanavyorudia, kwamba wao ni sehemu ya kile wanachoelezea kama "mhimili wa upinzani" na mshirika muhimu katika "chumba chake cha kufanya kazi".
Wayemeni wengi, hata walio ndani ya maeneo yanayodhibitiwa na Houthis, wanaamini kwamba mashambulizi yaliyoanzishwa na Wahouthi, iwe kwa Israeli, au katika Bahari ya Shamu au Ghuba ya Aden kwa kile wanachosema ni meli za mafuta zinazohusishwa na Israeli, " ziko ndani ya muktadha wa kutetea mshikamano na Wapalestina au Walebanon, na haziwezi kusimamisha vita vya Israel,” kama vile wanavyojumuisha “huduma kwa Iran na mkakati wake katika kukabiliana na Israel na Magharibi.”
Zaidi ya hayo, wachunguzi wa mambo wanasema kwamba mashambulizi hayo “mara nyingi huwa na athari mbaya kwa Yemen kwa ujumla na hata kwa nchi jirani kutokana na kupungua kwa usafiri wa meli za kimataifa na ongezeko la gharama za usafiri na bima kwa meli.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla na kuhaririwa na Yusuf Jumah












