Uvunaji wa viungo: Alisafirishwa kutolewaa figo na sasa analazimika kujificha

DFGHJ

Chanzo cha picha, Getty Images

BBC imepata fursa ya kuzungumza na timu ya Polisi iliyochunguza kesi ya kwanza ya kihistoria ya usafirishaji wa binaadamu kwa ajili ya kuvuna viungo.

Akiwa amekaa katika chumba cha ushauri cha hospitali ya Royal Free, jijini London akizungumza na madaktari kwa kiengereza chake kidogo, Daniel alikuwa na hofu kubwa. Na mtafsiri aliyelipwa alikuwa akisema kila ambacho madokta walitaka kusikia.

Mwanaume wa miaka 21 mchuuzi wa biashara ndogo ndogo katika jiji la Lagos, Nigeri alipelekwa Uingereza kwa kile alichoambiwa ni fursa ya kubadilisha maisha yake. Akidhani anakwenda kupata kazi ya ndoto ya maisha yake.

Madaktari walikuwa wakizungumza naye kuhusu athari za operesheni na uhitaji wa kupatiwa matibabu ya kiafya katika maisha yake yote. Wakati huo ndipo Daniel aliwaambia wapelelezi, kwamba alitambua hakuna kazi na aliletwa Uingereza kutoa figo lake kwa mtu asiyemjua.

Bahati kwa Daniel madokta walishuku kwamba hakujua kinachoendelea, na kulikuwa na hofu ya kushawishiwa. Ndipo madokta walisitisha mpango huo. Lakini Daniel hakuwa huru kuto kwa wasafirishaji wa viungo. Katika nyumba aliyokuwa anakaa wanaume wawili walikuja kumchunguza na alisikia kwa bahati mbaya mazungumzo yao wakijadili kumrudisha Nigeria ili figo lake likatolewe huko.

Alikimbia na baada ya siku mbili ya kulała nje, alikwenda kituo cha polisi karibu na Heathrow, na kupelekea uchunguzi wa mashitaka ya kwanza ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya kuvuna viungo.

Hiyo ilikuwa Mei 2022, Daniel sio jina lake halisi, kwa sasa anaishi chini ya ulinzi mkali wa Polisi. BBC imeelewa kwamba kesi yake ya kihistoria imetoa mwamko kwa mamlaka ya Uingereza kuhusu kesi nyigine za usafirishaji wa viungo.

JJDJD

Chanzo cha picha, METROPOLITAN POLICE

Maelezo ya picha, Sonia Ekweremadu akiwa na Daniel, ambaye si jina lake halisi

Uvunaji viungo ni nini?

Uvunaji wa viungo unahusisha uondoaji wa sehemu ya mwili kinyuma na sheria, na mara nyingi hufanywa kwa sababu za kibiashara kwa kujua au bila kujua kwa mwathirika.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Daniel alipopewa nafasi ya kwenda Uingereza wakati akiwa bado Nigeria, aliambiwa aende kuchunguza damu. Alidhani ilikuwa ni kwa ajili ya viza ya kweda Uingereza, lakini ilikuwa ni kuangalia damu yake ikiwa inafaa kwa ajili ya kutolewa figo.

Aliingizwa katika ndege kwenda London akiwa hana pesa na hakuruhusiwa kugusa paspoti. Kila hatua yake ilikuwa inadhibitiwa. Wasafirishaji wake kisha walimtambulisha kwa mwanaume wa Kinaigeria.

Picha yake na mwanamke huyo ilipigwa kama ushahidi wa uhusiano wao wa kifamilia. Akielezwa ni mpwa wake na yuko tayari kuchangia figo.

Sonia, aliyekuwa na umri wa miaka 25 wakati huo, ana tatizo sugu la figo. Anahitaji kubadilishiwa figo na hutolewa maji kwa masaa matano - mara tatu au nne kwa wiki.

Ushuhuda wake ulipelekea baba wa Sonia, moja kati ya mwanasiasa mwenye nguvu nchini Nigeria. Ni seneta wa zamani na bilionea Ike Ekweremadu, ambaye alikuwa analipia watoto wake wasome UK.

Katika kesi yake mwanzoni mwa mwaka huu, Ekweremadu anasema alipotoshwa na hakuwa na dhamira ya kumtumia Daniel. Jaji alisikia kuwa mtuhumiwa alisaidia kutunga sheria ambayo kuchangia kiungo ni kosa la jinai nchini Nigeria.

EEEE

Chanzo cha picha, MET POLICE

Maelezo ya picha, Mwanasiasa maarufu na seneta wa zamani wa Nigeria, Ike Ekweremadu

Mtu wa kati

Mahakamani ilibainika kuwa Daniel hakuwa mtu pekee kuletwa UK kwa ajili ya uvunaji wa figo. Uvunaji mwingine haramu ulifanyika 2021. Mwanaume ambaye alipokea figo hilo ana ukaribu na Ekweremadus, jina lake ni Dtk. Obinna Obeta, aliyeratibu kumtumia Daniel.

Dkt. Obeta alitambua mchakato mzima, upandikizaji wake ulifanyika katika hospitali ya Royal Free Hospital.

Akitoa hukumu, Jaji Johnson, akirejelea operesheni hiyo ya kwanza, aliiweka wazi: "Madaktari katika hospitali ya Royal Free, na wakaguzi wa kujitegemea katika taasisi ya Human Tissue Authority, walidanganywa."

Uwongo ulikuwa kwamba upandikizaji huo mnamo 2021 ulifanywa kwa maelewano na wafadhili na mpokeaji walikuwa binamu. Kwa kweli, iliibuka kuwa hawakuhusiana.

Ingawa upandikizaji wa Daniel ulisimamishwa, hakuna mtu kutoka Royal Free alikuwa amewaarifu polisi juu ya wasiwasi wao - ambapo ilimaanisha kuwa Daniel alikuwa hatarini.

Hospitali ya Royal Free ilituambia ilifuata mwongozo rasmi katika kesi ya Daniel na uamuzi wa kutoendelea ulichukuliwa.

Hospitali pia ilisema inaendelea "kufanya kazi kwa karibu na Polisi wa Metropolitan ili kuhakikisha wale wote wanaofanya kazi katika huduma zetu za upandikizaji wanafahamu sheria kuhusu usafirishaji wa viungo na wanajua nini cha kufanya ikiwa wanashuku kuwa uhalifu umetendwa".

JAJJAJ

Chanzo cha picha, MET POLICE

Maelezo ya picha, Dkt. Obinna Obeta, mtu wa kati na mke wa Seneta, Beatrice wote walipatikana na hatia

Utalii wa upandikizaji

Mtaalamu wa figo anayeishi Birmingham Dkt. Adnan Sharif anasema ni uhalifu mgumu kuthibitisha lakini tunajua kwamba hutokea. Akitoa mfano wa utafiti wa hivi karibuni wa NHS unaonyesha kumekuwa na kesi 150 zilizorekodiwa za watu waliorejea Uingereza katika kipindi cha miaka 10. Matukio mengi yalikuwa upandikizaji wa figo.

Kesi za utumwa wa kisasa mara nyingi ni ngumu sana kudhibitisha. Katika kesi ya Daniel, maafisa wa Polisi walitarajia uchunguzi ungedumu kwa miaka, kwa sababu wahalifu waliondoka nchini.

Lakini, tarehe 21 Juni 2022, mpelelezi sajenti Andy Owen alipokea simu ikimwambiwa Ike Ekweremadu na mkewe Beatrice walikuwa wakisafiri kwa ndege kwenda London.

Haraka alipeleka timu yake katika uwanja wa ndege wa Heathrow, na maafisa wenye silaha wakawasindikiza wenzi hao kutoka katika ndege.

Walipokamata simu za mshukiwa, polisi waliweza kubaini njama hiyo. Ushahidi muhimu ulijumuisha jumbe kuhusu ada ya wafadhili ya naira milioni 4.5 (pauni 4,317 au dola za kimarekani 5,487)

"Ilikuwa kama sanduku la hazina,"Owen alituambia. "Nilikuwa nikipata ushahidi zaidi na zaidi wa kuwatia hatiani. Lakini kushughulika na mshukiwa mwenye nguvu kama huyo haikuwa kazi rahisi.

HJKK
Maelezo ya picha, Kaka wa Danie, Baba yake na ndugu wamekuwa wakilia kutoweka kwake

Haikuwa kesi rahisi

Wakati wa uchunguzi, maseneta wa Nigeria walijaribu kushawishi kesi hiyo ipelekwe Nigeria.

Pia walitaka kuzungumza na mwathiriwa, alisema mpelelezi Andy Furphy, "ombi hilo lilitutia wasiwasi. Mara moja tulihisi mwathirika hakuwa salama."

Baada ya kutafuta ushauri wa kisheria, polisi waliweza kuhakikisha hawawezi kuzungumza na mwathirika.

Seneta Adamu Balkachuwa aliyeongoza ujumbe wa kumtembelea Ike Ekweremadu gerezani. Alituambia alitaka kuweka shinikizo la kidiplomasia na shinikizo kwa serikali ya Uingereza kuona ikiwa wataweza kuokoa hali hiyo.

Lakini Bw Bulkachuwa alisisitiza kuwa haikuwa kumpa mwenzake njia rahisi ya kurudi nyumbani, akieleza kuwa "sisi pia ni watia saini wa sheria za ulanguzi wa binadamu kimataifa".

Mnamo tarehe 23 Machi watu watatu waliohusika na sakata la Daniel walipatikana na hatia. Ike Ekweremadu alihukumiwa kifungo cha miaka tisa na miezi minane jela. Mkewe Beatrice alipata miaka minne na nusu. Mhusika mkuu, Dk Obeta, alihukumiwa miaka 10. Sonia hakupatikana na hatia.

Det Sgt Owen alikuwa mahakamani na Daniel. "Kwa kweli alisema, 'Nini maana ya hatia?' Hicho ndicho kiwango cha uelewa wa mfumo wa haki ya jinai aliokuwa nao." Aliiambia BBC Daniel alikuwa na furaha kwa kuaminiwa, na alitaka tu kuendelea na maisha yake.

Familia masikini

Huko Nigeria, makala haya yamehuzunisha mioyo ya wapendwa wa Daniel. Sasa wanahofia mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa washirika wa mwanasiasa mwenye nguvu wa Nigeria ambaye amemfungwa jela.

Tulikutana na kaka yake Daniel katika soko la Lagos lenye shughuli nyingi ambapo Daniel alikuwa akiuza vifaa vya simu za mkononi.

Alituambia hajazungumza na ndugu yake tangu alipotoweka ghafla Februari 2022 na alijua tu mahali alipo wakati habari za kesi hiyo ziliporipotiwa miezi kadhaa baadaye.

“Tumekuwa tukilia kila siku na baba yangu amehuzunika sana amekuwa mgonjwa sana,” anasema.

"Danieli alidanganywa na kuchukuliwa mbali."

Mwenye nyumba na mshauri wa Daniel, ambaye alizungumza naye kila siku kabla ya kutoweka, anashikilia kuwa asingekubali kuuza figo yake.

"Kwa sababu anajua kuna njia zingine za kupata pesa. Hata kwa pauni milioni moja asingefanya hivyo," alisema.

Danieli sasa anaogopa usalama wake. Yuko chini ya ulinzi wa polisi nchini Uingereza na anahisi hawezi kurejea Nigeria. Huenda hataiona familia yake tena.

Aliokoa figo yake na kutengeneza historia ya kisheria, lakini maisha yake yamesambaratika.