Siri ya hali ya kiafya ilivyomtesa mwanamichezo huyu wa Kitanzania

"Kwetu hapa Tanzania, ungekuwa mwisho wa dunia." Baba wa muogeleaji wa kwanza wa Tanzania wa Olimpiki akiongea na bintiye akikiri ukweli, huku akijaribu kueleza kwa nini alimficha hali iliyowaua jamaa zake watano hivi.

Hali ambayo - baada ya kuachwa bila kudhibitiwa - ilisababisha kukimbizwa hospitali mwishoni mwa mwaka jana, ambapo karibu kilo 4 za uvimbe zilitolewa kwenye mwili wa Magdalena Moshi kufuatia upasuaji wa dharura.

Wiki za maumivu zilifuata miaka na miongo kadhaa ya usumbufu aliokuwa nao tangu ujana wake, akipatwa na hali ambayo bila shaka ilizuia kazi yake ya kuogelea.

Kwa nini Alex, baba yake, hakuwahi kusema chochote kuhusu historia ya familia ya uvimbe? "Watu wanaweza kudhaniwa kuwa hawana uwezo wa kuzaa," alikiri waziwazi, kabla ya kuongeza.

"Ni mitazamo hiyo ya Kiafrika ambayo tunapaswa kujenga ufahamu kuhusu kuweza kuondoa."

Kwa kujibu, Magdalena anafanya dhamira yake kukomesha ukimya unaochochewa na utamaduni kuhusu masuala ya afya ya uzazi katika taifa lake la Afrika mashariki.

Kwani ni wakati tu anapata nafuu kutokana na upasuaji wake, huko Australia ambako ameenda kusoma, ndipo alipojifunza kwamba hali hiyo, ambayo inaweza kuwa ya urithi, imeendelea kwa muda mrefu katika familia yake.

Licha ya kupelekwa mara kwa mara katika hospitali katika mji mkuu wa Tanzania Dar-es-Salaam na masuala ya afya ya uzazi wakati wa ukuaji, unyanyapaa ulimaanisha uwezekano wa Magdalena kuwa nao haikumzuia.

"Sidhani kama kuna sehemu yangu ambayo itawahi kusamehe utamaduni kwa kufanya hivyo," mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 32 aliiambia BBC Sport Africa kutoka nyumbani kwake huko Adelaide, Australia.

Magdalena alikimbizwa hospitalini mnamo Septemba 2021 baada ya kupata maumivu katika sehemu yake ya chini ya tumbo la kushoto alipokuwa kwenye ukumbi wa mazoezi.

"Nakumbuka jambo la kwanza nililosikia nilipoamka ni daktari wa ganzi akisema 'uvimbe huo ulikuwa mkubwa - ulipanda kwenye mbavu zako!'" alikumbuka mwanamke aliyekuwa akisomea Shahada ya Uzamivu katika sayansi ya afya.

Alipokuwa akijifunza mwenyewe, uvimbe ni viota visivyokuwa na saratani ambavyo hukua ndani au karibu na uterasi na kwa kawaida hukua wakati wa miaka ya uzazi ya wanawake.

Hali hiyo inawaathiri sana wanawake wa Kiafrika, huku daktari wa Magdalena akisema asili yake ya Kiafrika inamaanisha kuwa uvimbe uligunduliwa akiwa amechelewa'.

"Wanawake wenye asili ya Kiafrika wana hatari ya kuongezeka kwa uvimbe mara mbili hadi tatu ikilinganishwa na wenzao wenye asili ya weupe," Dk Tran Nguyen aliiambia BBC Sport Africa.

Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, Moshi alipokea simu kutoka kwa baba yake Alex, nchini Tanzania, ikionesha kwamba ugonjwa wa fibroids ni ugonjwa unaoendelea katika familia.

"Kuelewa kwa nini familia ya baba yangu haikujadili mada hiyo ilikuwa ni kwa sababu fibroids inahusishwa na kusababisha utasa, kuharibika kwa mimba na kuzaliwa kwa watoto waliokufa - na kuamini kuwa mambo kama hayo kungezuia fursa za ndoa," aliongeza.

"Wazo ni kukaa kimya, kukuozesha na kisha unaweza kukabiliana nayo baadaye." Leo, Moshi anapitia awamu ya pili ya IVF huku akihangaika kupata ujauzito na mpenzi wake.

Moshi alikua mwana Olimpiki mwenye umri mdogo zaidi Tanzania alipofuzu Michezo ya Beijing 2008 akiwa na umri wa miaka 16.

Pia alishindana katika matoleo ya 2012 na 2016 lakini hakufanikiwa kupita kwani alikuwa akipambana mara kwa mara sio tu na wapinzani wake lakini pia maumivu sugu ya mgongo.

"Baada ya hali nzima nilijifunza kuwa dalili kubwa ya fibroids ni matatizo ya mgongo," alisema. Jinsi iliathiri kazi yangu ya kuogelea, siwezi kurudi nyuma kiakili kwa sababu itakuwa ya kufadhaisha sana."

Alipokuwa akipata nafuu kutokana na upasuaji, Magdalena - ambaye bado anaogelea kwa ushindani - alipanga simu ya video na baba yake ili kujadili suala hilo.

Akiwa amekatishwa tamaa na matukio, alitamani sana kugundua ni muda gani baba yake alikuwa amejua kwamba ugonjwa wa uvimbe ulienea katika familia, kwa nini aliendelea kuficha licha ya Magdalena kuonesha dalili wakati alipovunja ungo na ni funzo gani familia inajifunza kwa siku za usoni.

Huku BBC Sport Africa ikiruhusiwa kuketi kwenye mazungumzo, ilibainika kwamba Alex alikuwa amefahamu kwa muda mrefu watu kadhaa wa karibu wa familia ambao walikuwa wametibiwa uvimbe, wakiwemo wawili ambao walihitaji kufanyiwa upasuaji sawa na Magdalena. "Nilipokuwa mtoto, nilipoteza binamu yangu mmoja," Alex alisema.

"Kwa hiyo nimejua kuhusu suala hili, na kila mara nililiunganisha [hili] na uzazi. Kisha nikapoteza binamu zaidi kwa muda, na hatimaye nikagundua kuwa mama yangu alikuwa na matatizo kama hayo."

Alipoulizwa kwa nini masuala ya afya ya uzazi ya Magdalena wakati wa balehe na kutembelea hospitali mara kwa mara haikuwa sababu ya kutosha kufichua jambo hilo, Alex alijibu: "Mambo mengine hayajadiliwi tu kati ya baba na binti." "Katika tamaduni zetu, linapokuja suala la ndoa, watu huwa na tabia ya kujaribu kuficha udhaifu wao.

''Katika jamii yetu, zamani ilikuwa sheria ya kuishi - ambayo inamaanisha kila wakati unatafuta aina ya mwenzi mwenye afya zaidi. “Kwa hiyo kwa sababu hizo, mambo mengi haya yamefichwa kiutamaduni. "Kwa upande wangu, ilikuwa ugonjwa wa mbuni - wakati mbuni ana shida, huficha kichwa chake mahali penye giza, akitumaini sehemu nyingine za mwili ziko salama. Nilitarajia tutakuwa sawa."

Uzoefu huo umemfanya Alex kutafakari upya uhusiano wake na utamaduni wa muda mrefu wa kukataa na kunyamaza nchini Tanzania.

Anavunja mwiko na amezungumza na wanawake vijana wote katika familia yake ili waende kuchunguzwa ikiwa wako katika hatari ya kupata fibroids au hali zingine za afya ya uzazi.

Hata amepeleka kampeni yake katika kijiji cha familia hiyo, kilicho chini ya Mlima Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania. Wakati wa mazingumzo yao ya simu, Alex alimwambia Magdalena kwamba kifo chake kutokana na fibroids kingekuwa "matokeo mabaya zaidi" - lakini kutoweza kupata watoto kungekuwa "janga kubwa".

Magdalena hata hivyo anasema ataendelea kutetea mazungumzo ya wazi kuhusu afya ya uzazi kote Afrika. Baada ya shida zake mwenyewe, aliwasiliana haraka na jamaa ambao wanaweza kuteseka vivyo hivyo.

“Niliwapigia simu binamu zangu wa kike, nikawaambia nina hali hii na kwamba wote wanahitaji kuchunguzwa,” alieleza.

"Ujumbe wangu kwa wanawake vijana kote Afrika Mashariki na bara ni: kama una matatizo ya afya ya uzazi, haikuzuii wewe kuwa mwanamke - kwa hivyo zungumza na upate usaidizi." Baada ya kufanikiwa kuepuka hali iliyowapata wanafamilia wake wasiobahatika, Magdalena anapiga mbizi kwa kina huku akitumai kuwa kuhamasisha watu kuhusu ugonjwa wa fibroids nchini Tanzania na kwingineko kunaweza kuwasaidia wengine kwa kuvunja unyanyapaa.

Unyanyapaa ambao ulimaanisha kwamba mara nyingi alikuwa akiogelea na mkono mmoja nyuma ya mgongo wake, katika michezo na maishani. "Iliweka afya yangu ya muda mrefu, maisha yangu na uwezo wangu wa kupata watoto katika hatari kubwa."