Zifahamu familia 10 tajiri zaidi duniani, Je utajiri wao unatoka wapi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alice Walton ni binti wa muasisi wa Walmart Sam Walton.
Muda wa kusoma: Dakika 5

Katika orodha ya kila mwaka ya familia tajiri zaidi ulimwenguni ambayo huandaliwa na Bloomberg, familia ya Walton, mmiliki wa maduka makubwa nchini Marekani Walmart, ilishika nafasi ya kwanza mnamo 2024.

Zaidi ya miongo sita baada ya Sam Walton kufungua duka kuu la kwanza huko Arkansas, warithi wake ni matajiri zaidi kuliko hapo awali kutokana na utendaji uliovutia wawekezaji wa hisa za kimataifa, ambazo thamani yake imeongezeka kwa 80% mwaka huu.

Siri moja wapo ya kampuni zinazounda orodha hiyo, kwa mujibu wa Bloomberg, ni kwamba zimeendelea kuwa na umoja katika umiliki wa mali zao na, wakati fulani, zimeunda makubaliano ya kibiashara ambayo yanasimamia kuunganisha utajiri wao.

Familia nyingi katika orodha ya mwaka huu, kwa mujibu wa Bloomberg, zimekuwa tajiri zaidi kutokana na faida kubwa iliyorekodiwa kwenye soko la hisa.

Unaweza pia kusoma

Familia 10 tajiri zaidi ulimwenguni na chanzo cha utajiri wao.

1. Familia ya Walton

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Rob, Alice na Jim Walton walirithi na kuendeleza utajiri wa muasisi wa Walmart

Familia: Walton

Kampuni: Walmart

Utajiri: $432 bilioni (R$2.6 trilioni)

Nchi: Marekani

Vizazi: 3

Walton wanamiliki takriban 46% ya maduka makubwa, hisa ambayo ni msingi wa utajiri mkubwa wa familia hiyo.

Mwanzilishi wake, Sam Walton, aligawanya mali kati ya watoto wake kimkakati ili kuimarisha uchumi wa familia.

Unaweza pia kusoma:

2. Familia ya Al Nahyan

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamfalme wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed Al Nahyan ni sehemu ya familia ya mabilionea.

Familia: Al Nahyan

Sekta: viwanda

Utajiri: Dola za Marekani bilioni 323 (R$ 1.9 trilioni)

Nchi: Falme za Kiarabu

Vizazi: 3

Katika Umoja wa Falme za Kiarabu, familia tawala ya Al Nahyan ilizalisha utajiri wake kutokana na biashara ya mafuta.

Mtawala wa Abu Dhabi (mmoja kati ya wafalme saba), Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, pia ni rais wa nchi hiyo.

3. Familia ya Al Thani

.

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Tamim bin Hamad Al Thani, Amir wa Qatar, ni mwana familia yenye nguvu ya kifalme

Familia: Al Thani

Sekta: viwanda

Utajiri: US$ 172 bilioni (R$ 1 trilioni)

Nchi: Qatar

Vizazi: 8

Serikali ya familia ya Al Thani nchini Qatar ina maslahi ya kibiashara katika sekta ya mafuta na gesi.

Wanafamilia wanashikilia nyadhifa maarufu za kisiasa na wanamiliki kampuni kubwa katika tasnia mbalimbali.

Familia ni kubwa, ingawa nguvu yake kiuchumi imejilimbikizia katika maeneo machache muhimu.

4. Familia ya Hermès

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Axel Dumas, Mkurugenzi wa Hermès

Familia: Hermès

Kampuni: Hermès

Utajiri: US$ 170 bilioni (R$ 1 trilioni)

Nchi: Ufaransa

Vizazi: 6

Kizazi cha sita cha familia, kilichoundwa na wanachama zaidi ya 100, kinamiliki kampuni ya mitindo ya kifahari nchini Ufaransa.

Miongoni mwa wanafamilia wanaoshikilia nyadhifa za utendaji katika kampuni hiyo ni Axel Dumas, Mkurugenzi Mtendaji.

5. Familia ya Kochs

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Mfanyabiashara Charles Koch (pichani) na kaka yake Bill ni miongoni mwa wafadhili wakubwa wa wahafidhina wa Marekani

Familia: Koch

Kampuni: Koch Inc.

Utajiri: US$ 148 bilioni (R$ 900 bilioni)

Nchi: Marekani

Vizazi: 3

Ndugu Frederick, Charles, David na William Koch walirithi kampuni ya mafuta kutoka kwa baba yao, Fred. Lakini baada ya mzozo, ni Charles na David pekee waliobaki kwenye biashara hiyo.

Kampuni ya Koch ina biashara katika mafuta ya petroli, kemikali, nishati, madini, teknolojia ya komputa, fedha, biashara ya bidhaa, uwekezaji, miongoni mwa nyingine.

6. Familia ya Al Saud

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ni sehemu ya familia

Familia: Al Saud

Sekta: viwanda

Utajiri: US$ 140 bilioni (R$ 850 bilioni)

Nchi: Saudi Arabia

Vizazi: 3

Utajiri wa familia ya kifalme ya Saudia unatokana na biashara ya mafuta.

Makadirio ya Bloomberg yanatokana na malipo ya jumla ambayo wanafamilia ya kifalme wanakadiriwa kupokea kwa miaka 50 iliyopita kutoka kwa Royal Diwan, ofisi ya mtendaji mkuu wa mfalme.

Mwanamfalme Mohammed bin Salman anadhibiti binafsi mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja.

7. Familia ya Mars

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Jacqueline Mars (katikati) na wajukuu zake, Graysen Airth na Katherine Burgstahler

Familia: Mars

Kampuni: Mars Inc.

Utajiri: US$ 133 bilioni (R$ 810 bilioni)

Nchi: Marekani

Vizazi: 5

Kampuni ya Mars inajulikana kwa bidhaa zake kama vile M&M's, Milky Way na biskuti za chokoleti maarufu kama Snickers bar, ingawa bidhaa za utunzaji wa wanyama sasa zinachangia zaidi ya nusu ya mapato ya kampuni hiyo.

8. Familia ya Ambani

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Mukesh Ambani ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Reliance Industries

Familia: Ambani

Kampuni: Reliance Industries

Utajiri: US $ 99 bilioni (R $ 602 bilioni)

Nchi: India

Vizazi: 3

Mukesh Ambani ndiye anayesimamia eneo kubwa zaidi la kusafisha mafuta duniani.

Anaishi katika jumba la ghorofa 27 huko Mumbai, linalotajwa kuwa makazi binafsi ya gharama kubwa zaidi ulimwenguni. Yeye na kaka yake walirithi mali kutoka kwa baba yao.

Familia hiyo iliangaziwa hivi karibuni katika harusi ya Mukesh Ambani na Radhika Merchant. Ndoa hiyo ilitanguliwa na miezi minne ya matukio ya kifahari, ikiwa ni pamoja na matamasha ya nyota wa pop kama Rihanna.

9. Familia ya Wertheimer

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Alain Wertheimer na Gerard Wertheimer walirithi mali kutoka kwa babu yao

Familia: Wertheimer

Kampuni: Chanel

Utajiri: Dola za Marekani bilioni 88 (R$535 bilioni)

Nchi: Ufaransa

Vizazi: 3

Ndugu Alain na Gerard Wertheimer walirithi utajiri ambao babu yao aliyebuni ufadhili Coco Chanel huko Paris katika miaka ya 1920.

Familia yake inamiliki jumba la mitindo na pia farasi wa mashindano na mashamba ya mizabibu.

10. Familia ya Thomson

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, David Thomson, Rais wa Thomson Reuters

David Thomson, Rais wa Thomson Reuters

Familia: Thomson

Kampuni: Thomson Reuters

Utajiri: Dola za Marekani bilioni 87 ($529 bilioni)

Nchi: Canada

Vizazi: 3

Familia inamiliki takriban 70% ya hisa katika data na huduma za kifedha kutoka Thomson Reuters.

Utajiri wa familia tajiri zaidi ya Canada ulianza mapema miaka ya 1930 wakati Roy Thomson alifungua kituo cha redio huko Ontario.

Unaweza pia kusoma

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi