Muda mwafaka,bahati au talanta-kipi humfanya mtu kuwa bilionea?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Simon Jack
- Nafasi, Mhariri wa Biashara, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Je,Mwanafunzi wa kikomunisti wa Kiitaliano na mwigizaji, mtoto mchanga anayependa mpira na mcheshi anayefanya mzaha kuhusu chochote wana uhusiano gani?
Wote walipiga hatua na kuwa wanachama wa klabu ya kipekee sana ya kimataifa.
Miuccia Prada, Tiger Woods na Jerry Seinfeld ni miongoni mwa watu wapatao 2,800 kwenye sayari ambao ni mabilionea wa dola za Marekani.
Lakini orodha ya matajiri wakubwa ni ya kimataifa sana.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani la Forbes, linalofuatilia utajiri wa matajiri duniani, Marekani ina mabilionea 813, China (pamoja na Hong Kong) ni ya pili kwa 473, na India ni ya tatu kwa 200.
Ukubwa wamali hizi unaweza kuwamgumu kuelewa. Bilioni ni kiasi kikubwa - kutoa taswira ya kukuelewesha kuhusu hilo , sekunde milioni moja ni siku 11, lakini bilioni ni miaka 32.
Na kwa wengine, uwepo wa mabilionea ni kama 'uchafu'
Themanini na moja ya watu tajiri zaidi duniani - wanaoweza kujaa katika basi moja - wana utajiri zaidi ya watu maskini zaidi bilioni nne duniani kwa pamoja.
Katika ripoti ya 2023 kuhusu ukosefu wa usawa, Oxfam ilihitimisha: "Kila bilionea ni kosa la kisera. Uwepo wa mabilionea wanaoongezeka na kurekodi faida, wakati watu wengi wanakabiliwa na umaskini unaoongezeka, na mgogoro wa gharama ya maisha, ni ushahidi wa kuwepo kwa mabilionea na mfumo wa kiuchumi ambao unashindwa kuleta manufaa kwa binadamu.”
Kukosekana kwa usawa huko kumesababisha wito katika nchi nyingi za kodi kwa utajiri kamili badala ya mapato. Nchini Marekani, Seneta wa Chama cha Kidemokrasia Elizabeth Warren alipendekeza ushuru wa 2% kwa mali ya zaidi ya $50m (£39m) na 3% kwa mali zaidi ya $1bn (£778m).

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini wengine wanasema utajiri mkubwa huchochea na kuhimiza uvumbuzi unaoboresha maisha ya mamilioni ya watu.
Mwanauchumi wa Marekani Michael Strain anahoji kuwa tunahitaji mabilionea zaidi, sio wachache, na anataja mshindi wa tuzo ya Nobel William Nordhaus ambaye aligundua kuwa karibu 2% ya mapato kutoka kwa uvumbuzi wa teknolojia huenda kwa waanzilishi na wavumbuzi - mengine huenda kwa jamii.
Strainanawaita mabilionea "kwa kiasi kikubwa wabunifu waliojitengenezea ambao wamebadilisha jinsi tunavyoishi". Anataja mifano kama vile Bill Gates na Steve Ballmer ambao walibadilisha kompyuta , mwekezaji maarufu Warren Buffett, Jeff Bezos ambaye aliboresha uuzaji wa rejareja, na Elon Musk ambaye alitatiza tasnia ya magari na biashara ya anga.
"Hakuna hata mmoja wao ambaye ni ishara ya 'kufeli kwa sera'," anahitimisha. "Badala ya kutamani kwamba wasingekuwepo, tunapaswa kufurahishwakwamba wapo"

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mabilionea wengi pia hutoa pesa nyingi kwa uhisani. Gates na Buffett walitengeneza “The Giving Pledge” - ahadi ya kutoa zaidi ya nusu ya utajiri wa mtu katika maisha yao yote.
Rapa, gwiji wa biashara na bilionea Jay-Z, ingawa hajasaini ahadi hiyo, alitoa utetezi huu wa kina wa utajiri wake: "Siwezi kuwasaidia maskini kama mimi ni mmoja wao. Kwa hivyo nilitajirika na kuwasaidia. Kwangu mimi huo ndio ushindi kwa wote."
Mabilionea hawapati utajiri katika ombwe. Mafanikio yao pia yanatuambia kitu kutuhusu.
Ni vigumu kuwa tajiri sana isipokuwa unapotoa kitu ambacho watu wanahitaji, wanataka au wanafurahia.
Iwe ni mitindo ya kisasa zaidi ya Prada, filamu za Star Wars au TikTok, mabilionea tunaowajadili kwenye podikasti wamebadilisha ulimwengu kwa kiwango kikubwa au kidogo - na hadithi za jinsi walivyofanikiwa zinavutia.
Kwa mfano, waanzilishi wa Google walijaribu kuuza toleo la awali la injini yao ya utafutaji kwa $1m lakini hapakuwa na wanunuzi. Leo Google ina thamani ya $2.3tn na mwanzilishi mwenza Sergey Brin ana thamani ya $135bn binafsi - takriban Pato la Taifa la Morocco.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maria Bianchi alikuwa mkomunisti katika miaka ya 1960 Italia akisomea maigizo katika shule ya uigizaji kabla ya kubadili jina lake hadi Miuccia Prada.
Bilionea wa kwanza wa kike wa aliyejifikisha katika hadhi hiyo kwa bidii yake nchini India, Kiran Mazumdar-Shaw, alianza kutengeneza bia kabla ya kukumbana na ubaguzi wa kijinsia na badala yake akajaribu kuunda dawa, na kuwa mzalishaji mkuu wa insulini barani Asia.
Wazazi wa Jerry Seinfeld wote walikuwa yatima na baba yake hakuwahi kumkumbatia. Labda moja ya sababu ambazo yeye na Larry David walikuwa na sheria kwa wahusika katika pindi cha chao cha vichekesho ,Seinfeld: "Iwapo humkumbatii mwenzio hufunzwi."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mafanikio ya kibinafsi ya mabilionea hawa pia mara nyingi husimulia hadithi ya mielekeo pana ya kihistoria, kisiasa au kiteknolojia.
Mjasiriamali wa teknolojia Jack Ma, ambaye alianzisha kikundi cha Alibaba, alikuwa mnufaika wa nguvu mbili zenye nguvu na za wakati mmoja - kuzaliwa kwa uuzaji wa rejareja mtandaoni na kuongezeka kwa nguvu za kiuchumi za Uchina na ukwasi mkubwa.
Chuck Feeney, mwanamume aliyevumbua ununuzi bila kutozwa ushuru (na akatoa mali yake yote ) alisimamia wimbi kubwa la utalii wa Kijapani baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna hadithi ambazo bahati ilihusika .
Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates alienda katika mojawapo ya shule chache sana nchini Marekani mwishoni mwa miaka ya 1960 ambazo zilikuwa na kompyuta. Wakati mwimbaji na mwanamke mfanyabiashara Rihanna alipata mafanikko yake kutokana na majaribio ya bahati na mtayarishaji wa rekodi ambaye alikuwa likizo huko Barbados.
Na tusikie kwa wazazi.
Familia nzima ya Taylor Swift ilihama kutoka Pennsylvania hadi Nashville ili kuendeleza taaluma ya binti yao kijana huku mama yake Michael Jordan akipendekeza "asikie kile Nike inachosema" kabla ya kusaini mkataba na Adidas au Converse -na kumweka katika njia ya kupata dili la faida kubwa zaidi la kuidhinisha katika historia ya michezo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna baadhi ya matukio ya "milango kujifungua" katika hadithi hizi - matukio madogo ambayo kwa kuangalia nyuma yalibadilisha maisha ya mabilionea hawa.
Lakini milango inapofunguliwa, lazima uipite, na ikiwa kuna sifa moja ya kawaida ni msukumo, bidii na kujitolea ambako watu hawa wameleta kwa taaluma zao. Pamoja na hamu yao ya kuendelea, wakati wengi wangekuwa wamesalimu amri zamani.
Mtangazaji mwenza wa My Good Bad Billionaire Zing Tsjeng na mimi huwa tunatania kwamba tukifika, sema, $10m,utaona vumbi - tungekuwa na viti viwili tu vinavyozunguka kama ushahidi kwamba nilikuwa nimeenda kuvua samaki na yeye amekwenda kwenye tamasha jingine la muziki.
Nadhani watu kama sisi hatutawahi kufaulu kupata utajiri mkubwa kama huo lakini tumekuwa tukivutiwa , kusukumwa, kushangazwa na kutishwa na wale ambao wamefaulu kupata kiasi hicho cha utajiri mkubwa .
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah












