WARIDI WA BBC: Kutana na Getrude Mungai kungwi kutoka Kenya

Getrude Mungai

Chanzo cha picha, Getrude Mungai

    • Author, Anne Ngugi
    • Nafasi, BBC Swahili

Getrude Mungai ni kungwi kutoka nchini Kenya, kazi yake kuu ni kuelimisha watu walioko kwenye ndoa au wanaopania kuingia kwenye ndoa kuhusiana na masuala ya unyumba miongoni mwa mambo mengine.

Mwanamke huyu anasema kuwa maisha yake akiwa binti ni kana kwamba yalimtayarisha kuwa kuwa kungwi, kwani alizaliwa na wazazi waliokuwa bado na umri mdogo, na kisha kujipata akilelewa na bibi huko Mombasa pwani ya Kenya.

Mwanzo wa maisha ya ndoa yalikumbwa na misukosuko ambayo ilitokana sana na malezi yake.

Je alianza aje kuwa mtoa mawaidha ya chumbani

Katika pilka pilka za kutafuta biashara za kufanya alianza kuandaa kitchen party au mapishi wakati wa sherehe za shughuli ya kumpa bibi harusi mawaidha.

Getrude aliona mwanya wa kutotayarishwa kwa wanawake katika ndoa, hasa kwa kuwa alihisi mwanamwali alikuwa anapewa mawaidha ya kuvumilia ndoa na wala sikuifurahia.

miaka 17 iliyopita alipoanza kazi hii kama biashara ilizua mjadala mkali na nchini Kenya.

Wakati Getrude alikuwa anaanza kazi hii ilikuwa nadra sana na huenda hakuna mwanamke mwengine aliyejitokeza kimasomaso kufundisha masuala ya chumbani hadharani hata ndani ya vyombo vya habari.

Getrude ni miongoni mwa wanawake wa kizazi cha sasa waliokuwa na ukakamavu wa kufundisha hayo.

Wakati Getrude Mungai alikuwa anajitambulisha kwa watu alikuwa anatumia neno la kiingereza Sexologist kujitaambulisha na baadhi ya watu walirudi kwenye vitabu kusoma maana yake sahihi.

Wakati huo Getrude alikumbana na maswali kama ni kwa nini mwanamke afanye iwe taaluma na pia kulikuwa na maswali mengi ya ni kwa nini mtu aifanye taaluma ya kufundisha watu maswala ya ngono iwe biashara ?

”Wakati nilianza kazi hizi kulikuwa na shauku na vile vile mashaka , lakini hata sasa bado hukose wakosoaji wa kazi ninayoifanya ila tunapambana kila siku ”anasema Getrude.

G

Chanzo cha picha, Getrude Mungai

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa mfano anasema kuwa kunao wanawake ambao hawakukaribisha hatua ya Getrude kuwafundisha mabinti wao, hali kadhalika taasisi za elimu baadhi zilikuwa na wasiwasi kuhusiana na mada hiyo, ilikuwa ni lazima kwanza apitie idara ya elimu mafundisho yake yapitishwe.

Getrude anasisitiza kuwa yeye ana utaalamu kando na hayo akiwa mama ya wavulana wakubwa anaimani kuwa maswala ya kufundisha watu kuhusu ngono inakujia kwa mazingira ya wanandoa au ambao wako katika mchakato wa kufunga ndoa.

Lakini pia inasisitiza kuwa kuna baadhi ya vijana ambao tayari wamejiingiza kwa ndoa za mapema na kwa hiyo anawajibika kuzungumzia atahari ya tabia kama hizo kwa vijana.

Miaka kadhaa iliyopita jina lake Getrude lilikuwa ndio Gumzo mitandaoni wakati alipozindua makala maalum katika mfumo wa CD au kanda spesheli ambayo ilikuwa na mafundisho yaliojumuisha mitindo na namna ya wanandoa wanavyoweza kufurahia tunda la ndoa, kadhalika umuhimu wa usafi kwa mwanamke ili kujiandaa kufurahia mapenzi na mwenzi wake.

PIa aliangazia mambo mengine yanayohusu ndoa hususan chumbani, pamoja na jinsi ya mwanamke kuendelea kupendeza machoni mwa mume wake licha ya kukaa kwa ndoa miaka mingi.

Getrude Mungai ni nani ?

Yeye ni mke na ni mama pamoja na kuwa ni mjasiriamali, Getrude amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 23 na yeye na mume wake Peter Mungai wamejaaliwa wana wa kiume wawili.

Kando na kuwa alisomea taaluma ya mapishi aliona pengo katika mahusiano hasa kwenye ndoa.

Tulipomuuliza mbona anafunza wanawake pekee masuala ya unyumba anajibu kwamba ni rahisi kwa wanawake kutulia na kusikiliza mafundisho hasa inayohusu jamii, wanawake ni wepesi wa kulipia mafundisho ya kunufaisha jamiii.

Getrude pia anasema wanaume wengi hawawezi kuchukua muda kufundishwa maswala kadha wa kadha hasa kama haina faida ya kifedha.

”Ila nadhani kwa sababu ninawafunza wanawake, wanaume wao wanajifaidi kwani wale wake hurudi nyumbani kutekeleza mambo ambayo nimewafundisha, ni vizuri pia nisisitize kuwa wanaume huwa wananipigia simu na wengine kuingia kwenye mitandao yangu kupata maelezo zaidi. ”Getrude anasema

Getrude anasema kuwa wengi wa wanawake walioko kwenye ndoa hutafuta mafundisho yake hasa inapotokea kuwa mwenza ametoka nje ya ndoa, aidha anasisitiza kuwa baadhi ya wanawake hujilaumu hali kama hiyo inapojitokeza na hutafuta mawaidha ya kuimarisha mapenzi.

Licha ya hayo mwanamke huyu anasema kuwa kwa mwanandoa kuchipuka huwa hakuna sababu za kimsingi kulaumu mwenzake, na analaumu wale wanaowalekezea kidole cha lawama mume anapotoka nje ya ndoa.

Gertrude Mungai ni mjasiriamali ambaye ametumia ukakamavu wake kuzungumzia swala nyeti katika ndoa kwa uweledi na mtindo unaoeleweka kwa mfano ametumia manenoz kama ‘mombasa raha’ anapozungumza na watu wazima juu ya maswala e ya chumbani.

Ametumia mitandao ya Kimani ie, vipi ndio ya televisheni na radio kunadi kazi zake .

Anamatumaini kuwa juhudi zake kuvunja kinywa kuhusu changamoto enda jinsi ya kudumisha ndoa hasa tendo la ndoa litasaidia jamii kujadili maswala Haya bila hofu.