Waarabu wa Israel wakamatwa kuhusiana na habari za mitandaoni Gaza

Chanzo cha picha, Supplied
Maafisa wa usalama nchini Israel wamewakamata makumi ya Waisraeli wenye asili ya Kiarabu kwa kuhusika katika kuchapisha na kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vita vya Israel na Hamas na hali ilivyo kwenye ukanda wa Gaza.
Miongoni mwao ni muimbaji mashuhuri na mwanamitindo mwenye ushawishi mkubwa kutoka Nazareth Dalal Abu Amna, ambaye alizuiliwa na polisi kwa siku mbili na kuachiliwa huru jumatano wiki jana.
Mwanamitindo huyo wa kike, anaendelea kuzuiliwa nyumbani kwake hadi jumatatu wiki hii.
Kulingana na wakili wake Abir Baker , msanii huyo ameshutumiwa kwa kushiriki katika ‘tabia ya kuleta madhara’. Mamlaka nchini humo zimesema zinaamini taarifa alizochapisha kwenye anwani zake za mitandao ya kijamii zinachochea wafuasia wake kujihusisha na ghasia.
Baker amesisitiza Kamba muimbaji huyo anaumaarufu mkubwa katika eneo la mataifa ya kiarabu kwa miziki yake kuhusu Paletsina , na utamaduni wake na kwamba taarifa zake zilikuwa zinashiria hisia zake za kidini.
Lakini Israel imesemataarifa hizo kama hatua ya kuwataka wapelastina kujihami na kuingia vitani.
Tangua kuzuka kwa makabiliano ya kivita kati ya Israel na Hamas, polisi kutoka Israel wamekuwa wakiangazia sera ya kutokubali chochote kinachodunisha taifa hilo hasa katika mitandano ya kijamii ambayo inaonyesha uungwaji mkono wa kundi la Hamas.
Kundi hilo linalenga kumaliza taifa la Israel na limetajwa kama kundi la kigaidi na Israel kwa Pamoja na Marekani, Uingereza, na mengine mengi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu Zaidi ya 100 wanazuiliwa
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ni nini kinachoendelea?
Ni nini kilichoenedelea?
Tunaangazia kwa haraka na kwa ukamilifu kilichojiri n ani kwa nini ni muhimu n ani kitu gani itakachofanyika kuanzia sasa.
Abu Amma ni mmoja kati ya makumi ya watu wenye uraia wa Israel ambao wana asili ya kiarabu ambao wamekamatwa kwa kushukiwa kuhusika kwenye uchapishaji na usambazaji wa taarifa tete kuhusu vita vya sasa mitandaoni.
Wengi wamesimamishwa kazi kwa muda au kufutwa kazini , nao wengine wakiadhibiwa na wakuu wa vyuo vikuu.
Waisraeli wenye asili ya kiarabu , baadhi ambao wanapendelea kutambuliwa kama raia wa Palestina, ni asilimia 20 ya idadi ya jumla ya taifa la Israel.
Polisi wamesema kwamba watu zaidi ya 100 wamezuiliwa kwa wanachokiendeleza kupitia mitandao ya kijamii tangu shambulizi la Hamas la wiki mbili zilizopita.
Mjini Jerusalem pekee, watu 63 walikamatwa na kuhojiwa. Wengi wao wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi wa chuki na kuunga mkono ugaidi.
‘yeyote anayechochea ghasia dhidi ya taifa la Israel, alama/mifumo yake , viongozi waliochaguliwa kisiasa, wanajeshi na polisi ni sharti wafahamu kuwa polisi wa Israel watajibu kwa makali na bila ya huruma,’ amesema kamishena wa polisi Yaakov Shabtai, mapema wiki hii.
Waarabu wengi ni wakazi wa Nazareti – mji uliopo kaskazini mwa Israel.
Wawakilishi wa kituo cha sheria cha Adal, ambacho kinatetea haki za jamii ndogo ya warabu wenye uraia wa Isarel kimesema kuwa kinaamnini kwamba waliokamatwa na kuziliwa ni wengi zaidi, kutokana nah atua za kukamatwa kwa watu zaidi katika siku chache zilizopita.
Kuzuiliwa kwa waarabu waisreali kutokana na kuchapisha taarifa zinazoonekana tete kwenye mitandao sio jambo geni. Ni hali iliyowahi kutokea hapo awali. Hata hivyo, kituo cha kisheria cha Adal kinasema kwamba katika muda ambapo makabiliano yamezidi kuchacha katika ukanda wa Gaza mnamo Mei 2021 , ni watu 16 pekee ambao walikamatwa na kushtakiwa na tuhuma za kuchochea ghasia, 15 miongoni mwao wakiwa ni waarabu.
Watetezi wa haki za kibinadamu wanahofia kwamba polisi wameanza hatua ya kuwakatama na kuwauzia watu wengi zaidi kwa misingi ya kuangazia kwa upana suala la ‘uchochezi wa ghasia’
Kwa mfano, katika mji wa wa kibedouin wa Rahat, uliopo kusini mwa Israel , polisi wanamzuilia aliyewahi kuwania kiti cha Umeya mjini humo Amer al Huzail ambaye alichapisha kwenye mitandao ya kijamii ramani ya ukanda wa Gaza kwa Pamoja na tathmini ya mbinu mbali mbali zinazoweza kutumika na jeshi la Israel kutekeleza shambulizi la ardhini . Alishtumiwa kwa kosa la kuwafaa maadui wakati wa vita.
Hata hivyo, wale ambao hawajakabiliwa na mashtaka makuu kisheria, wanakumbwa na adhabu nyingine kuu kwa shughuli zao mitandaoni.
Mawakili wa Adalah wanasema kwamba wamepokea data[taaarifa] muhimu ya kesi zaidi ya 40 ambapo waisraeli wenye asili ya kiarabu wamesimamishwa kazi au kufutwa kabisa katika muda wa siku moja.
‘Wakati mwingine watu hupoteza kitega uchumi chao kwa sababu tu ya kukubaliana na taarifa lililochapishwa mitandaoni kwa kubonyeza alama la ‘like’, ‘ anasema Salaam Irshade, msemaji wa shirika la kutetea haki za kibinadamu. ‘Tumekuwa na kesi ambapo mtu ametishwa kufutwa kazi kwa ku’like’ ripoti ya hali ilivyo katika ukanda wa Gaza kwenye mitandao ya kijamii.’
Wanafunzi wa vyuo vikuu wenye asili ya kiarabu, pia wanakabiliwa na tishio la kupokea adhabu kutoka kwa vyuo hivyo vikuu.
Wiki jana, Ariel Porat- rais/kiongozi wa chama cha wanafunzi katika chou kikuu cha Tel Aviv alisema kwamba wanafunzi kadhaa wameeleza kuunga mkono ‘madhila ya kundi la Hamas’
‘Tutakuwa wakali kwa wanafunzi hao,’ aliandika kwenye tovuti ya chou hicho. ‘Na tukiamua kufanya uamuzi kwamba makosa husika ni ya jinai, basi tutairipoti kwa polisi.’ ‘ Tutachukuwa hatua ya haraka, kwani hali katika muda huu mgumu inatulazimu kufanya hivyo, ila hatutamzuia mwanafunzi yeyote haki ya kufanyiwa uchunguzi uliokamilifu.’
Mawakili wa Adala aidha wamesema kwamba wamepokea malalamishi kutoka kwa wanafunzi 83 wa shula ambao wamesimamishwa kuhudhuria shule kwa muda katika maeneo mbalimbali nchini humo , na katika baadhi ya kesi, wameamrishwa kuondoka kwenye mabweni ya shule bila ya kupawa muda wa kutosha kujiandaa.
‘ Hamna hata kesi moja miongoni mwa yaliyotajwa ambayo yanahusisha hatua, ishara, au watu kuhusika katika hatua zilizokinyume na sheria. Tunazungumiza tu kuhusu taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii,’ amesema Dkt. Hasan Jabarin, afisa mkuu mtendaji wa Adaah.
‘ Zaidi ya asilimia 90 ya taarifa zilizochapishwa zinapinga vita hivyo kwa uwazi, na vile vile kupinga hatia za Israel ndani ya Gaza, huku zikiunga mkono maobi ya kuwaangazia waathiriwa wa vita hivi Gaza,’ ameongezea.
‘Asilimia 10 ya taarifa zilizochapishwa ziko katika hali ambayo sio Dhahiri na inaweza kutafsiriwa kama uungaji mknono wa Hamas japo sio wa moja kwa moja. Katiak hali ya kawaida hayawezi kutasfiriwa hivi, lakini sasa Israel inaangazia utafsiri huu wa jumbe hizi katika njia kali.’
Sio Waarabu pekee
Katika hatua ya kulaani shambulizi lililotekelezwa na kundi la Hamas ambalo liliwauwa watu 1400(wengi wakiwa raia), ghadhabu/hasira ya raia nchini Israel kwa wakati mmoja imewalenga waIsraeli ambao ni wayahudi ambao wanatoa ombi la kusitishwa kwa mapigano na kunedelezwa kwa uhasama.
Jumamosi iliyopita, polisi walilazimika kumuondoa mwanahabari Israel Fey ambaye ni myahudi wa kiothodoksi mwenye kuunga mkono upande wa kushoto kutoka nyumbani mwake mjini Tel aviv kwa sababu za kiusalama.
Fey alichapisha video kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliwaombea raia wali ondani ya Gaza , hatua iliyozua ghadhabu iliyochochea maandamano karibu na nyumbani kwake ambako shambulizi la fataki lilitekelezwa.
Na hapo jumatano, Osef kassif, mbunge wa kiyahudi kutoka kwenye kundi linaloongozwa na Waarabu la Hadash-Ta’al alisimishwa kwa muda wa siku 45 vkutohudhuria vikao katika bunge la Israel baada yah atua yake kushutumu vikali mashambulizi ya angani yanayoelekezwa kwenye ukanda wa Gaza.
Katika moja ya taarifa alizochapishwa katika mtandao wa X uliofahamika kama Twitter, alikashifu vikali polisi ,ambao kulingana naye hawakuchukuwa hatua za dharura kumlinda Frei.
‘Polisi wenye kujihami kwa silaha wanatumwa kumkamata yeyeote ambaye anaonyesha huruma kwa mauaji ya halaiki yanaoendelezwa katika ukanda wa Gaza,’ aliandika Kassif. ‘Lakini polisi hawana haja ya kumlinda mwanahabari mwenye kuunga mkono mrengo wa kushoto ambaye Maisha yake yammo hatarini,’














