Kwa nini watu wanaovaa nguo chafu wanaongezeka duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna vuguvugu linalokua la watu wanaoamini kufua nguo mara chache au kutokufua nguo kabisa. Matilda Welin alizungumza na kundi la watu wanaoamini katika 'kufua nguo mare chache na wale ambao hawafui nguo kabisa.
Brian Szabo na timu yake wametumia muda mwingi kuchunguza picha za nguo zilizotumika kama njia ya kushindanisha. Miongoni mwao kulikuwa na nguo ambazo zilikuwa zimepauka, zingine zimetoka nyuzi, uchafu kwenye magoti na mapajani. Kumekuwana kundi linalosifia nguzo chachu ama zilizofifia zaidi.
Szabo anakadiria kuwa zaidi ya washindani 9 kati ya 10 katika Indigo Invitational, ambayo imeadhimisha mwaka wake wa nne mwezi Januari, walifua suruali zao kwa mara ya kwanza baada ya kuvaa mara 150 au 200.
"Unakutana na harufu kidogo." Baadhi ya marafiki zake huvaa jeans zao kwa muda mrefu zaidi, na anaiita "falsafa ya kutokufua kamwe." Wananuka... Sio harufu mbaya, lakini unasikia harufu."
Szabo pia hutumia mashine ya kufulia. "Mke wangu anapoanza kunusa suruali yangu ya jeans, ananiambia moja kwa moja ziende kwenye chumba cha kufulia."
Kuongezeka kwa tabia ya kutopenda kufua
Kwa mujibu wa Szabo, tabia ya kufua mara chache nguo ilianza mnamo 2010, wakati aliponunua jozi yake ya kwanza ya jeans. Alichukua safari ya miezi sita kutoka nchi yake ya asili ya Canada hadi Ulaya. "Ilikuwa kama wazimu kuwa na jozi hiyo ya jeans yenye harufu nzuri," aliiambia BBC Culture. "Harufu ilikuwa isiyovumilika."
Alikutana na mke wake baadaye huko Budapest, na jeans ikawa sehemu ya uhusiano wao. "Suruali zangu zilikuwa zimerundikana mwisho wa kitanda," anakumbuka. "Yeyote aliyeingia chumbani kwangu aliweza kusikia harufu... Nilikuwa na bahati kwamba mke wangu alinipenda nilivyo."

Chanzo cha picha, Indigo Invitational
"Ikiwa hakuna uchafu kitu kikubwa sana cha kusafisha, usiisafishe."
Wavaaji wa nguo za kitambaa kigumu kama jinsi wamepunguza sana kufua.
Mnamo 2019, mbunifu wa mitindo Stella McCarthy aligonga vichwa vya habari kwa kufichua jinsi anavyofua nguo yake ya ndani safisha. Aliiambia The Guardian: "Kimsingi, sheria ya maisha ni, ikiwa sio chafu sana, usifue. Sibadilishi sidiria zangu kwa siku nzima. Siweki nguo kwenye mashine ya kufua kwa sababu tu nimeivaa. Mimi ni mtu wa usafi sana. Lakini mimi si shabiki wa kufua nguo mara kwa mara."

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Chelsea Harry kutoka Connecticut, Marekani, anasema anatoka kwenye kaya ambayo kila kitu kilioshwa ama kufuliwa hata baada ya kutumika au kuvaliwa mara moja," anaiambia BBC Culture.
"Taulo na pajama zilifuliwa hata baada ya kutumika mara moja." Kipindi fulani cha majira ya joto, Harry aliishi na bibi yake, na bibi yake alimfundisha kuweka pajama zake chini ya mto wake asubuhi na kuziweka tena usiku uliofuata.
Baadaye, alikutana na mumewe, na anasema, "hufua nguo mara chache chache sana."
Halafu, wakati wa janga la Covid, Harry alianza kutembea umbali mrefu. Mambo mengi yalibadilika baada ya janga hili.
"Ni vigumu sana kuoga baada ya kutembea siku nzima na kulala kwenye kitanda cha majani," anasema. Watu wengine katika jumuiya inayotembea wanapendekeza kuvaa chupi za Ex Officio, ambazo hukauka haraka na zinaweza kuvaliwa kwa siku. Harry aligundua kuwa kuzitumia kulifanya iwe rahisi kutembea kwa siku nyingi bila kufua. "Kisha, nikawaza, 'Kwa nini siwezi kufanya hivi katika maisha yangu ya kila siku?'" anasema.
Vipi kuhusu harufu na kunuka?
Harry hajali kuhusu harufu. "Ninaiamini pua yangu," anasema. Anaweza kujinusa anapovaa nguo. Kama Sabo, yeye hutumia mbinu mbalimbali ili kuepuka kufua nguo kabisa, kama vile kuziacha mahali wazi usiku kucha, au kuzinyunyiza kwa kinywaji kikali cha vodka. "Ninapenda kuning'iniza gauni langu, nguo zangu za ndani na soksi ninapozivua jioni," anasema. "Ninazitundika karibu na dirisha. Ninazikausha, nina nguo ya ndani ya Ex Officio. Ninaivaa tena asubuhi iliyofuata."
"Jambo baya zaidi unaweza kufanya ili kufupisha maisha ya nguo yako ni kuifua," alisema Mark Sumner, mhadhiri wa ubunifu wa mitindo endelevu katika Chuo Kikuu cha Leeds.
Anasema nguo zinaweza kuchanika, kusinyaa au kufifia zikifuliwa mara kwa mara. Mark Sumner anafanya kazi na mwenzake Mark Taylor kwenye utafiti kuhusu jinsi nguo za nyumbani zinavyoishia maharini na kuliwa na viumbe vya huko. Anasema kupunguza idadi ya kufua mara kwa mara nguo zako ni chaguo sahihi kwa mazingira, lakini haimaanishi usifue kabisa nguo zako.
"Hatuhitaji kuwashawishi watu kwamba wasifue. Lakini kufanya hivyo mara kwa mara 'aanaharibu sayari yetu," Sumner aliiambia BBC Culture.

Chanzo cha picha, Alamy
Unahitaji kufikiria tena ni mara ngapi unafua ama kwa mkono ama kwa kutumia mashine.
Ukishakuwa na mazoea ya kufua nguo mara kwa mara, ni vigumu kukadiria ni mara ngapi utazifua, Sumner na Taylor waanasema. Mbinu bora ni kuwa na utaratibu. "Ikiwa nguo zako hazina harufu mbaya, usijisumbue kuzifua," Sumner alishauri.
"Unapofua nguo zako, tumia njia nzuri zaidi ya kufua." Anashauri kufua nguo kwa kutumia joto la chini kama unatumia mashine. Au, anapendekeza kufua nguo bila kutumia sabuni.
Kwa kuongeza, kufua pia kunapoteza muda ambao ungeweza kufanya shughuli nyingine ya kukupatia kipato.
"Nani ana muda? Ninavutiwa sana na masuala ya mazingira na usimamizi wa maliasili," anasema Harry.
"Lakini, pia nina wasiwasi kuhusu muda wangu."
Szabo pia anajali kuhusu hilo, lakini ana sababu nyingine za kuondokana na tabia za kufua mara nyingi nguo zake.
"Nina kazi nyingi za kufanya," anasema. "Pia lazima nimtembeze mbwa wangu."













