Africa Eye: Uhamiaji 'Hakuna kurudi nyuma'

Maelezo ya video, Africa Eye: Uhamiaji 'Hakuna kurudi nyuma'

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji husafiri kutoka Nigeria, wakiwa na matumaini ya kufika Ulaya. Miaka 20 iliyopita, mkurugenzi wa Nollywood Ike Nnaebue alijaribu kufanya safari hiyo hiyo.

Akifuatilia hatua zake, Ike anakutana na wimbi jipya la wahamiaji. Anasikia kuhusu matumaini yanayowasukuma katika safari yao na kushuhudia hatari zinazowangoja.

Anakutana na wahamiaji ambao wanaishia kufilisika, kukwama au wahasiriwa wa mashambulio ya kibaguzi kwa misingi ya rangi.

Wengine wanajipata mikononi mwa walanguzi haramu wa binadamu.

Kwa wale wanaofika Morocco, Bara Ulaya inaweza kuonekana kuwa karibu sana, lakini mara nyingi inaweza kuwa ngumu kufika huko kama zamani.