Rubani wa ndege aina F-35 aelezea jinsi alivyonusurika kifo sekunde chache kabla ya ajali

Rubani wa ndege aina F-35 aelezea jinsi alivyonusurika kifo sekunde chache kabla ya ajali
Akizungumza muda mfupi baada ya tukio hilo mnamo Novemba 2021, rubani anayejulikana kama Hux alisema alikuwa na sekunde chache tu kujinusuru.
Uchunguzi rasmi ulihitimisha kupotea kwa nguvu kwa ghafla wakati wa kupaa kwa ndege hiyo pengine kulisababishwa na kifuniko kilichoachwa wazi kwenye moja ya sehemu za ndani za ndege.
Simulizi yake imejumuishwa katika mfululizo wa Makala ya BBC kwa jina The Warship: Tour of Duty.
Filamu hiyo pia inafichua jinsi meli ya Royal Navy ya HMS Queen Elizabeth ilivyonyanyaswa na ndege za Urusi na jinsi ilivyocheza mchezo hatari wa kujificha na Jeshi la Wanamaji la China.
Rubani wa Royal Navy alizungumza na watengenezaji wa filamu muda mfupi baada ya kuokolewa na alikuwa bado anaugua majeraha na michubuko iliyosababishwa na kutolewa katika ndege hiyo kasi kubwa.
Anaeleza jinsi ndege hiyo ilipopoteza nguvu ghafla: "Nilijaribu kutavuta nguvu za dharura - hiyo haikufanya kazi, kisha nikajaribu kupiga breki - hiyo pia haikufanya kazi ... kwa hivyo nilijua kuwa itatoka nje ya meli."
Maisha ya Hux yaliokolewa na kiti chake cha ejector - ambacho anakielezea kuwa cha teknolojia ya juu zaidi duniani. Hiyo na bahati aliokuwa nayo.
Parachuti yake ilipowashwa, anasema aliona bahari chini yake "na kisha sekunde moja baadaye niliona eneo la chini la meli likianza kuonekana chini yangu".
Alifanikiwa kufika kwenye meli - kwa futi chache - kabla ya kuvutwa hadi mahali salama. Ikiwa hangetua kwenye meli hiyo , alihatarisha kuburutwa chini ya meli hiyo ya kivita yenye tani 65,000.
Video iliyovuja kutoka kwa kamera ya ubaoni ya meli ilionyesha wakati F-35 ilipoanguka baharini.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Chanzo cha picha, Photoshot
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Uchunguzi rasmi ulihitimisha kuwa kupotea kwa ghafla kwa nguvu za umeme katika ndege hiyo labda kulisababishwa na kizuizi - kifuniko kilichoachwa wazi kimakosa ndani ya ndege.
Ndege hiyo – ambayo ndio ya kisasa Zaidi duniani inayoendeshwa kwa pamoja nchini Uingereza na Jeshi la Wanamaji la Kifalme na Jeshi la Wanahewa la Royal - baadaye ilipatikana chini ya bahari ili kuhakikisha haikuchukuliwa na mikono isiyofaa.
Chris Terrill, ambaye alirekodi filamu hiyo, alisema ajali hiyo ya F-35 "ilikuwa mshtuko kwa kila mtu", lakini akasema majibu ya kampuni ya meli yalikuwa"ya haraka kwani ilikuwa tukio la kushangaza".
"Ndege pengine ingepotea lakini kulikuwa na rubani, mwenza ambaye alipaswa kuokolewa," alisema.
"Mafunzo yalianza lakini kulikuwa na nguvu na uharaka wa ziada kwa mabaharia kutekeleza taratibu zao za dharura. Iilikuwa tukio la kutisha lakini la kutia moyo kutazama."
Msururu huu wenye sehemu sita unafuatia safari ya miezi minane ya HMS Queen Elizabeth, ya maili 49,000 ya baharini hadi Bahari ya Pasifiki na kurudi mwaka jana.

Inaonyesha jinsi meli hiyo ya kivita ya Uingereza ilivyoharakishwa na ndege ya Urusi yenye makombora mashariki mwa Mediterania. Jeti za F-35 zinaonekana zikizikatiza ili kuzizuia zisisogee karibu sana na meli hiyo ye kubeba ndege za kivita.
Hati hii inaieleza hatua iliokaribia mapigano ya kweli. Katika chumba cha oparesheni afisa wa vita alipendekeza kuweka ndege ya Urusi kwenye macho yao kwa "shambulio la kuiangamiza " ili kuwaonya.
F-35s pia huwekwa katika hali ya tahadhari wakati meli nyingine ya Uingereza, HMS Defender, inapokaribiana na ndege hizo za Urusi wakati ilipokuwa ikisafiri katika Bahari Nyeusi.
Katika Bahari ya China Kusini, meli ya kivita ya Malkia Elizabeth HMS inashiriki katika mchezo wa paka na panya na Jeshi la Wanamaji la China.












