Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi mchoraji huyu alivyopambana na wakosoaji wa kidini Somalia
Na Mary Harper
Mhariri wa Afrika, BBC World Service News
Hashi hakuwahi kwenda shule ya sanaa.
‘’Baba yangu alikuwa mwalimu wangu. Hakuwa msanii lakini alikuwa akiigiza katika muda wake wa ziada. Nilimwomba anionyeshe jinsi ya kuchora. Lakini alifariki nikiwa mdogo.’’
Mama yake hakuunga mkono ndoto zake za kuwa msanii.
Wala majirani zake, ambao walimshtumu kuwa si Mwislamu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba sanaa inayoonyesha wanadamu na wanyama ni haramu.
"Walinilazimisha kuacha uchoraji. Niliachana kabisa na sanaa na kusomea uuguzi. Lakini niliona inachosha. Siku moja niliamua sanaa isiniache na kamwe sitaiacha sanaa yangu, haijalishi watu wananifikiriaje.’’
Sasa Hashi anaishi maisha mazuri kutokana na sanaa yake na anaweza kusaidia familia yake kubwa.
Mzee wa miaka 26 anaishi Hargeisa, mji mkuu wa jamhuri ya Somaliland, na anapokea mgao wake wa pesa kutoka kwa idara za serikali, mashirika ya kimataifa na watu binafsi.
Wizara ya elimu ya Somaliland ilimwomba kutoa picha kwa ajili ya kampeni yake ya kuwaingiza wasichana wengi shuleni.
‘’Msichana huyu anafanya kazi zake za nyumbani wakati anachunga mbuzi wa familia baada ya kutembea kwa muda mrefu nyumbani kutoka shuleni. Nilitaka kuonyesha kwamba wasichana wanaweza kusoma pamoja na kazi zao za nyumbani.’’
Tume ya hivi majuzi ilikuwa picha ya jumba la wanahabari la wanawake pekee, Bilan, lililoanzishwa hivi karibuni mjini Mogadishu.
Inaonyesha mwandishi wa habari akiwarekodi wanawake wanapoendelea na maisha yao ya kila siku.
Ukitazama kwa makini chini ya mti, unaweza kuona Hashi akichora picha.
Si rahisi kupata nyenzo za wasanii nchini Somalia na Somaliland kwa hivyo inabidi awaombe marafiki wamtumie rangi, brashi na turubai kutoka Kenya, Djibouti na kwingineko.
Sanaa ya Hashi inazidi kuwa ya kisiasa - na baadhi ya mashirika ya habari na waandishi wa habari hutumia kazi yake.
Wakati wa maandamano ya upinzani ya Agosti huko Somaliland, takriban watu watano walipigwa risasi na kufa wakati wa mapigano na vikosi vya usalama.
‘’Niliona picha ya wanawake wakiwa wamejificha nyuma ya viti huku polisi akifyatua risasi. Sikuweza kuiondoa akilini.’’
‘’Waziri mmoja alijitokeza bila kualikwa kwenye mazishi ya mmoja wa waandamanaji. Watu walikasirika na mwanamke mmoja akampiga teke la mgongoni.
‘’Sasa anaonekana kama shujaa wa upinzani!’’
Huku eneo hilo likistahimili ukame wake mbaya zaidi katika miongo minne, Wasomali wanakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu.
‘’Wanasiasa wanaomba ulimwengu wa nje kutuma pesa kwa watu wenye njaa,’’ anasema Hashi.
‘’Kisha wanaiingiza kwenye mifuko yao wenyewe.’’
Ukame na uharibifu wa mazingira huhamasisha baadhi ya picha zake za kuchora.
Mchoro huu katika studio yake ya Hargeisa unaashiria ardhi iliyopasuka, kavu na kuchomwa kwa miti ya thamani kutengeneza mkaa.
Picha nyingi za Hashi zinaonyesha watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
Hii ni familia ya kuhamahama inayomsikiliza mwanahabari maarufu Ahmed Hassan Awke kwenye Idhaa ya Kisomali ya BBC.
‘’Cha kusikitisha amefariki sasa.’’
Watu walimpenda sana, haswa sauti yake ya ajabu.’’
Baadhi ya michoro ni ya kibinafsi sana.
‘’Hii inanionyesha nikipambana na virusi vya Covid. Nilikuwa mgonjwa sana na niliogopa kufa kama watu wengine wengi karibu nami.
‘’Baada ya kuchora picha hii, watu walianza kunipigia simu kuniuliza jinsi nilivyoweza kupona.’’