Dubai: Visiwa 300 vilivyogharimu dola bilioni 12 na kutelekezwa

jj

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Visiwa vya "dunia" ni mojawapo ya miradi ambayo Falme za Kiarabu ilianzisha.

Kuelekea mwisho wa karne iliyopita, Umoja wa Falme za Kiarabu ulianza miradi ya kujenga visiwa vya kifahari.

Mojawapo ya miradi hiyo, uilikuwa ni "dunia,” mkusanyiko wa visiwa karibu 300 ambavyo vilitengeneza sura ya mabara saba ya dunia kama yanavyoonekana kwenye ramani.

Mradi huu ulizinduliwa na Sheikh mwenyewe wa UAE, Mohamed bin Rashid Al Maktoum, mwaka 2003.

Kwa uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 12 na matumizi ya karibu mita za ujazo milioni 321 za mchanga na tani milioni 386 za mawe, lengo lilikuwa kuunda visiwa vya kifahari kwa ajili ya matajiri.

"Maono ya Umoja wa Falme za Kiarabu ilikuwa kutafuta njia mbadala ili kuchukua nafasi ya utegemezi wa mafuta kama chanzo kikuu cha mapato. Na chaguo lilikuwa biashara ya mali isiyohamishika," anasema Profesa Alastair Bonnett, mwanajiografia katika Chuo Kikuu cha Newcastle na mwandishi wa kitabu "A journey into the era of artificial islands.”

Pia unaweza kusoma
FGV

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Kuna visiwa vichache tu vilivyo na majengo.

Lakini biashara hiyo inaonekana kuwa mojawapo ya zile ambazo hazikufanikiwa. Tovuti ya Top Luxury imetangaza hivi karibuni, “mradi wa dunia ni mradi mkubwa usio na mafanikio duniani."

Sababu ni rahisi; miaka 21 ya mradi huo, ni visiwa vichache tu vimejengwa majengo na kukamilika na kutoka angani vinaonekana kama vilivyotelekezwa.

Pamoja na kuwa 60% ya mradi huo tayari umeuzwa, na wajenzi wanaonyesha kuwa mipango yao inaendelea, lakini uchunguzi unaonyesha visiwa vina dalili za kumomonyoko.

Kwanini mradi ulikwama?

KJHG

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Hivi ndivyo mradi ulivyowasilishwa mwaka 2003 na Mtawala wa Falme za Kiarabu.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwaka 1999, Umoja wa Falme za Kiarabu ulijitambulisha duniani kama nchi ya kisasa na ya kimataifa.

Mwaka huo, hoteli ya Burj al Arab ilifunguliwa. Mwaka huo huo, Sheikh wa UAE pia alitangaza ujenzi wa mradi wa "Palm Jumeirah," nyumba za makazi na hoteli ambazo zitakuwa kwenye kisiwa ambacho kitakuwa na mwonekano wa mtende.

Mradi huo ulifanya vizuri katika mauzo na kusababisha mipango mingine ya kujenga visiwa kama hivyo kuanza.

Kwa hivyo, 2003, Al Maktoum mwenyewe alitoa ruhusa kwa ujenzi wa visiwa 300 karibu na fukwe za Dubai, maradi huo ulijaribu kuiga mafanikio ya "Palm Jumeirah.”

Lengo ni watu matajiri ambao wanaweza kununua moja ya visiwa na wajenga chochote wanachotaka.

Kama mwandishi wa gazeti la The Guardian, Oliver Wainwright anavyosema, "miradi katika kila kisiwa pia ilikuwa ya kuvutia sana. Bilionea wa China alikuwa amepanga kutengeneza mji wa Shanghai kwenye kisiwa chake, kwa kujenga Mnara wa Shanghai.”

Na kampuni inayoitwa Opulence Holdings ilikuwa imenunua Somalia, "kwa nia ya kuichonga katika umbo la samaki wa baharini, ambapo wakazi wangeweza kupiga mipira ya gofu kutoka kwenye roshani zao," anasema Wainwright.

Majengo machache yamejengwa. Mgogoro wa kifedha wa 2008 ulifanya mradi kuyumba. Wengi wa wale ambao walijitolea kununua nyumba hizo waliachwa bila rasilimali za kutosha

Kwa hivyo, mradi unaendelea, ingawa bila maendeleo makubwa.

“Moja ya matatizo makubwa ya mradi huu, inaelezwa kuwa ni tofauti na Palm Jumeirah, visiwa hivyo havina muingiliano, hakuna daraja ambalo mtu anaweza kuvifikia kwa gari wala hakuna daraja kati ya visiwa,” anasema Bonnett.

Lakini kampuni ya Nakheel Properties, inayojenga mradi huo imesema mara kadhaa mradi wa dunia unaendelea na wanatafuta rasilimali ili kuuendeleza.

Miradi mingine

fg

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Palm Jumeirah, moja ya miradi inayovutia zaidi huko Dubai.

Licha ya mradi wa dunia, kutoendelea kama inavyotarajiwa - haimaanishi wazo la kugeuza Dubai kuwa kitovu cha biashara ya mali isiyohamishika halijafanya kazi.

Hivi sasa, Palm Jumeirah, ina karibu nyumba 4,000 na takribani watu 25,000 wanaishi. Kuna hoteli nyingi na vivutio vingi vya kitalii vinavyofanya kazi huko.

Ingawa kuna mafanikio mzuri, biashara ya visiwa vya namna hiyo ili kuunda nafasi ya maendeleo ya miji ya kibiashara ni hatari.

"Kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari hufanya uwekezaji katika kisiwa kuwa hatari. Na jambo moja ambalo linaitambulisha Dubai, ni utayari wake wa kufanya miradi ya hatari, hata kama ni kwa gharama kubwa,” anasema Profesa Alastair Bonnett.

KJH

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Hii ndio hali ya sasa ya visiwa vya dunia

Zaidi ya hayo, ujenzi wa Jumeirah na miradi mengine kama vile "dunia" au "Kisiwa cha Deira" - ambacho ujenzi wake ulisimamishwa pia kutokana na ukosefu wa rasilimali - imekuwa na athari za kimazingira na kukosolewa vikali.

Shirika la Greenpeace limedokeza, miradi hiyo sio rafiki kwa mazingira na ujenzi wa visiwa hivyo umeathiri pakubwa miamba ya matumbawe karibu na pwani ya emirate.

Ingawa Nakheel Properties, ilikubali kuwa baadhi ya mifumo ya ikolojia ya baharini iliathiriwa na ujenzi ya miradi huo, imesisitiza kuwa timu ya wanabiolojia wa baharini iliajiriwa ili kujenga upya na kukarabati miamba iliyoathiriwa.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah