COP28 Dubai ni nini na ni kwa nini ni muhimu?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Na Mark Poynting

Mtafiti wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, BBC News

Viongozi wa dunia wanakutana kujadili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa mjini Dubai.

Mkutano huu unafanyika baada ya mwaka wa matukio mabaya ya hali ya hewa ambayo yamemevunja rekodi nyingi za hali ya hewa.

COP28 ni nini na iko wapi?

COP28 ni mkutano wa 28 wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa (UN) wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo serikali zitajadili jinsi ya kupunguza na kujiandaa kwa mabadiliko ya tabia nchi siku zijazo.

Mkutano huo unafanyika Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023.

COP inamaanisha "Mkutano wa Vyama", ambapo "vyama" ni nchi ambazo zilitia saini makubaliano ya asili ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1992.

Kwa nini kufanyika kwa COP28 Dubai kunazua utata?

UAE ni mojawapo ya mataifa 10 yanayoongoza duniani kwa uzalishaji wa mafuta.

Imemteua mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali, Sultan al-Jaber, kuwa rais wa mazungumzo ya COP28 .

Mafuta - kama gesi na makaa ya mawe - ni mafuta ya kutumia visukuku. Hizi ndizo sababu kuu za mabadiliko yatabia nchi kwa sababu hutoa gesi chafu zinazoongeza joto katika sayari yetu kama vile kaboni dioksidi zinapochomwa kwa ajili ya nishati.

Kampuni ya mafuta ya Bw Jaber inapanga kupanua uwezo wake wa uzalishaji .

Nyaraka zilizofichuliwa kwa BBC zinaonyesha kuwa UAE ilipanga kutumia nafasi yake kama mwenyeji kusaini mikataba ya mafuta na gesi .

Bwana Jaber hapo awali alitoa hoja kwamba yuko katika nafasi nzuri ya kipekee kusukuma hatua kutoka kwa sekta ya mafuta na gesi, na kwamba kama mwenyekiti wa kampuni ya nishati mbadala ya Masdar, pia amesimamia upanuzi wa teknolojia safi kama vile nishati ya upepo na jua.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sultan al-Jaber amekuwa chaguo lenye utata kuongoza mazungumzo ya mabadiliko ya tabia nchi ya COP28

Kwa nini COP28 ni muhimu?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Inatarajiwakuwa COP28 itasaidia kutekeleza lengo la kupunguza ongezeko la joto la muda mrefu duniani hadi kufikia kiwango cha 1.5C. Hii ilikuafikiwa na karibu nchi 200 katika makubaliano ya mjini Paris ya mwaka 2015 .

Lengo la 1.5C ni muhimu ili kuepuka athari mbaya zaidi za mabadiliko ya htabia nchi , kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la ambadiliko ya tabia nchi na Jopo la Serikali za nchi kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC).

Ongezeko la joto la muda mrefu duniani kwa sasa limekaribia kipimo cha 1.1C au 1.2C ikilinganishwa na nyakati za kabla ya viwanda - kipindi kabla ya wanadamu kuanza kutumia nishati ya mafuta kwa kiwango kikubwa.

Lakini makadirio ya hivi majuzi yanaonyesha kuwa ulimwengu kwa sasa uko kwenye mstari wa karibu 2.4C hadi 2.7C za ongezeko la joto kufikia mwaka 2100 , ingawa idadi kamili haijulikani.

Kama matokeo, dirisha la kuweka kikomo cha 1.5C kufikia "linapungua kwa kasi", Unasema Umoja wa Mataifa.

Nini kitajadiliwa katika COP28?

Pamoja na maendeleo kuelekea malengo yaliyopo ya Paris, COP28 itazingatia :

  • kufuatilia kwa haraka hatua ya kusafisha vyanzo vya nishati, "kupunguza" uzalishaji wa gesi chafu kabla ya 2030
  • kutoa fedha kwa ajili ya hatua za hali ya hewa kutoka nchi tajiri hadi maskini zaidi, na kufanyia kazi mpango mpya kwa mataifa yanayoendelea
  • kuzingatia asili na watu
  • kufanya COP28 kuwa "jumuishi zaidi" daima

Nani atakuwa kwenye COP28?

Zaidi ya serikali 200 zimealikwa.

Rais wa Marekani Joe Biden na Xi Jinping wa China hawatarajiwi kuhudhuria, lakini nchi zote mbili zitawakilishwa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak atashiriki, na Kasri la Buckingham limethibitisha kuwa Mfalme Charles pia atahudhuria. Atatoa hotuba ya ufunguzi kwa wajumbe tarehe 1 Desemba.

Misaada ya mazingira, vikundi vya jamii, biashara na vikundi vya kidini pia vitashiriki.

Mamia ya wajumbe walio na nishati ya visukuku walihudhuria COP27 mwaka wa 2022 .

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rishi Sunak alitangaza kurudi nyuma kwa baadhi ya sera za kijani mwezi Septemba, jambo ambalo liliibua ukosoaji wa kimataifa

Ni mada zipi zitajadiliwa katika COP28?

Kuna uwezekano wa kuwa na kutokubaliana kuhusu mustakabali wa makaa ya mawe, mafuta na gesi ambayo hutengenezwa bila teknolojia yinayofaa ya uzalishaji wake.

Bw Jaber ametoa wito ''kiwango cha chini " cha matumizi yake. Hata hivyo, Umoja wa Ulaya unatarajiwa kushinikiza matumizi yake "kuondolewa " kabisa

Wanaharakati wa mabadiliko ya tabia nchi wanaeleza kuwa kuzuia mikataba ya nishati ya mafuta ya "visukuku" kungeruhusu baadhi ya uzalishaji kuendelea. Wanasema hakuna dhamana ya kuzuia uzalishaji wa hewa chafu. Wanashauri ufanyike kwa kiwango.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Umoja wa Mataifa umetoa wito wa " kumalizwa " kabisa kwa nishati ya mafuta ya "visukuku" kama makaa ya mawe

Pesa pia litakuwa ni suala muhimu

Katika COP27, mfuko wa "hasara na uharibifu" uliafikiwa ambapo nchi tajiri ziliahidi kulipa nchi maskini zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Lakini kwa jinsi gani makubaliano haya yatatekelezwa bado haijulikani wazi. Marekani, kwa mfano, imekataa kulipa fidia ya athari za mabadiliko ya tabia nchi yaliyotokana na uzalishaji wake wa kihistoria wa hewa chafu.

Mnamo mwaka wa 2009, nchi zilizoendelea zilijitolea kutoa $100bn (£82bn) kwa mwaka, ifikapo 2020, kwa nchi zinazoendelea ili kuzisaidia kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kujiandaa kwa mabadiliko yatabia nchi.

Lengo halikufikiwa lakini linatarajiwa kufikiwa mnamo 2023.

Je, COP28 italeta tofauti yoyote?

Wakosoaji wa COPs za awali, ikiwa ni pamoja na mwanaharakati Greta Thunberg , wanashutumu mikutano ya kilele ya "greenwashing": yaani, nchi na biashara hunadi s juhudi zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi bila kufanya mabadiliko yanayohitajika.

Lakini viongozi wa dunia wanapokusanyika, mikutano hiyo inatoa uwezekano wa makubaliano ya kimataifa ambayo huenda ukasaidia kuchukuliwa kwa hatua za kitaifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mfano, kikomo cha ongezeko la joto cha 1.5C, kilichokubaliwa dkatika kikao cha Paris katika COP21, kimewezesha kuchukuliwa kwa "hatua ya hza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi karibu ulimwengu kote", kulingana na Umoja wa Mataifa.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwana Yusuf Jumah