Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Je Urusi inaishiwa hifadhi yake ya silaha?
Urusi imeanzisha mashambulizi ya mfululizo karibu katika maeneo yote ya Ukraine wiki hii - lakini baadhi ya wataalam wa usalama wanasema hifadhi zao nyingi zinaishia, hasa za makombora ya kisasa.
Ni makombora gani ambayo Urusi imekuwa ikirusha?
Huku Urusi ikizidisha mashambulizi yake ya makombora katika siku za hivi karibuni, maswali yameibuka kuhusu aina ya silaha zinazotumiwa.
Wataalamu wa masuala ya ulinzi wanasema matumizi ya Urusi ya makombora ya ardhini kwenda angani kuyatumia kulenga shabaha za nchi kavu ni dalili ya uhaba wa zana zinazofaa zaidi.
"Jambo muhimu zaidi katika [mashambulizi ya hivi karibuni] ni kuongezeka kwa matumizi ya aina mbalimbali za makombora kwenye mapambano ya nchi kavu," anasema Douglas Barrie, Mshiriki Mwandamizi wa Anga ya Kijeshi katika Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati.
"Makombora ya ardhini, hapo ndipo tunapofikiri kunaweza kuwa kuna kitu. Angalau katika baadhi ya maeneo, si kwamba yameisha kuisha, lakini inawezekana yamepungua."
Urusi ilitumia makombora mengi kulenga shabaha za ardhini kote Ukraine mwanzoni mwa vita, lakini mashambulio hayo yalisuasua wakati wa kiangazi, huku baadhi ya maafisa wa ulinzi wa nchi za Magharibi wakisema hifadhi zao za silaha zilikuwa zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Wiki hii, Sir Jeremy Fleming, mkuu wa shirika la ujasusi la Uingereza GCHQ, amesema: "Tunajua - na makamanda wa Urusi walioko chini wanajua - kwamba vifaa na silaha zao zinaisha."
Kuna ushahidi gani unaoonekana kuhusu hilo?
Hifadhi ya makombora ya Urusi ni siri inayolindwa kwa ukaribu, na hatujui wanatumia vitu gani mashirika ya kijasusi ya magharibi kufanya tathmini zao, lakini kuna vidokezo katika picha zinazotokana na mashambulio ya hivi karibuni.
Baadhi ya picha za mabaki zilizowekwa mtandaoni zikionyesha uchafu wa makombora ya S-300 ardhini nchini Ukraine.
Hizi ni silaha zimetengezwa kwa ajili ya kushambulia angani (ndege), sio ardhini.
Machapisho kama haya kwenye mitandao ya kijamii yamedai kuwa makombora haya ya S-300 yametumika tena na Urusi kushambulia nchi kavu:
Tumeangalia kwa karibu msururu wa picha zinazosambaa mtandaoni, na tumethibitisha picha tatu za mabaki ya silaha hizi nchini Ukraine ambazo zinalingana na makombora ya S-300 - ingawa Urusi na Ukraine zote zinamiliki silaha hizi, zimekuwa zikilaumiana zenyewe kwa zenyewe kuhusu kuzitungua.
Tumeyatizama maandishi ambayo yanaonekana kando ya mabaki ya picha za S-300, na uwekaji lebo unafafana.
Vipimo pia vinalinganishwa.
Baadhi ya wataalam wanasema Urusi imeamua kutumia silaha hizi kwa sababu ya kupungua kwa makombora mengine ya ardhi.
"Wamekuwa wakitumia makombora machache ya masafa marefu kushambulia huko Kyiv, Lviv na kadhalika. Nina hakika waliangalia hifadhi zao, waliangalia uwezo wao wa kutengeneza... na wakagundua bora zaidi ni kutumia makombora ya S-300," anasema Louise Jones, mkuu wa ujasusi katika Huduma za Ujasusi za McKenzie.
Je inawezekana haya yakawa makombora ya Ukraine?The Ukrainians also use S-300 in a defensive role to shoot down Russian missiles, and the Russians say these are falling to the ground causing collateral damage and civilian casualties.
Waukraine pia wanatumia S-300 katika kujihami kusambaratisha makombora ya Urusi, na Warusi wanasema kuwa makombora hayo yanaanguka chini na kusababisha uharibifu mkubwa na kujeruhi raia.
Evgeny Popov, afisa katika bunge la Urusi, aliiambia BBC kwamba uharibifu katika maeneo ya kiraia kama vile uwanja wa michezo wa watoto ni "kazi ya mifumo ya [Kiukreni] ya kuzuia makombora".
Ni vigumu sana kujua asili ya kombora kutoka kwa mabaki yake, wanasema wataalam wa silaha.
"Mlipuko wa vichwa vya vita vya kugawanyika kama vile vilivyo kwenye aina nyingi za kombora zinazoendana na S-300 vinaweza kuunda uchafu sawa kwa njia yoyote ... kwa hivyo nadhani jibu ni lisiloweza kutabirika huko," anasema Sidharth Kaushal, mtafiti mwenza katika Taasisi ya Royal United Services.
Ian Williams, mwenzake katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, anasema hajaona ushahidi wowote wa mifumo ya Kiukreni kurusha risasi wakati wa mashambulizi ya hivi majuzi.
Silaha gani nyingine Urusi inazitumia?
Urusi ilianza vita kwa mfululizo wa mashambulizi ya makombora. Kufikia Machi 7, Pentagon ilikadiria kuwa Warusi walikuwa wamerusha karibu makombora 600 katika siku 11 za kwanza za mzozo.
Mashambulizi yaliendelea kutoka ardhini, baharini na angani - kwa kiasi kikubwa yalitokea ndani ya mipaka salama ya Urusi.
Aina ya silaha za Kirusi zilizorushwa ni pamoja na makombora ya balestiki na yale yanayorushwa na Iskander, na makombora ya kusafiri ya Kalibr kutoka meliniu na manowari zilizowekwa kwenye Bahari Nyeusi.
Kh-101 and KH-555 air-launched cruise missiles have been deployed, as well as Tochka-U missiles, responsible for the deaths of more than 50 people at the Kramatorsk railway station in April.
Makombora ya ndege ya Kh-101 na KH-555 yanatumiwa na warusi, pamoja na makombora ya Tochka-U, yaliyohusika na vifo vya zaidi ya watu 50 katika kituo cha reli cha Kramatorsk mwezi wa Aprili.
BBC analysis of an attack on the Kremenchuk shopping centre in late June, which killed at least 20 people, determined that the missiles used were either Kh-22s or a more modern variant, the Kh-32.
These are older missiles originally designed to attack ships, rather than land targets, which has further fuelled the view that Russian stocks of some modern weapons may be running low.
Uchambuzi wa BBC wa shambulio kwenye maduka ya Kremenchuk mwishoni mwa mwezi Juni, ambalo liliua takriban watu 20, unaonyesha makombora yaliyotumiwa yalikuwa ya Kh-22s au lile la kisasa zaidi, Kh-32.
Haya ni makombora ya zamani ambayo yaliundwa awali kushambulia meli, badala ya mashambulizi ya nchi kavu, ambayo imechochea zaidi maoni kwamba hifadhi ya Urusi ya baadhi ya silaha za kisasa inaweza kuwa imepungua.