Ukraine yakosoa sera ya nishati ya Merkel
Ukraine imemkosoa kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel baada ya kusema ‘’hakuwa na la kuomba msamaha’’ kuhusu jibu lake kwa hatua ya Urusi kunyakua Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.
Merkel, ambaye aliondoka madarakani miezi sita iliyopita, alisema Jumanne kwamba Ulaya na Urusi ni majirani ambao hawakuweza kupuuza kila mmoja.
‘’Lazima tutafute njia ya kuishi pamoja licha ya tofauti zetu zote,’’ alisema.
Lakini mshauri wa rais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak alisema Merkel ‘’ameisukuma’’ Ulaya kuelekea utegemezi zaidi wa usambazaji wa nishati wa Urusi.
‘’Ikiwa Kansela Merkel siku zote alijua kwamba Urusi ilikuwa inapanga vita na lengo la Putin ni kuharibu EU, basi kwa nini [Ujerumani] ingejenga Nord Stream 2,’’ aliandika kwenye Twitter.
Mrithi wa Merkel Olaf Scholz alisimamisha mradi wa bomba la gesi mwezi Februari baada ya uvamizi huo.