Jinsi chuki dhidi ya Uislamu inavyodhuru sera ya kigeni ya India

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Aprili 2020 madai kuhusu mkutano wa Waislamu kuchangia kuongezeka visa vya Covid-19 nchini India kwa haraka ulichukua mkondo wa chuki dhidi ya waslamu.
Maelfu ya wahubiri kutoka ndani na nje ya nchi walikuwa wamehudhuria mkutano huko Delhi wa Tablighi Jamaat, vuguvugu la kimishonari la Kiislamu la karibu miaka 100. Serikali ya Narendra Modi ya chama tawala cha Hindu Bharatiya Janata Party (BJP) iliuita "mkutano ulioeneza zaidi".
Meme na alama za reli za kuchukia Uislamu zikililaumu kundi hilo kwa kueneza virusi zilivuma kwenye mitandao ya kijamii, na mitandao ya habari ilitangaza vichwa vya habari kama vile "Okoa nchi dhidi ya jihad ya Corona".
India ilihukumu karibu watu elfu moja waliohudhuria mkutano huo kwa kukiuka sharia za vizuizi miezi minane, lakini baadaye,mahakama zilimwachilia huru mhubiri wa mwisho kati ya waliozuiliwa, ikisema "wamefunguliwa kwa mashitaka yasiyo sahihi" chini ya maagizo kutoka kwa serikali.)
Wengi wa wahubiri walitoka Indonesia, mshirika wa kibiashara wa India. Indonesia ilionyesha wasiwasi wake juu ya suala hilo katika mikutano ya kilele ya kikanda. Wabunge wa nchi hiyo walidai kwamba mabishano hayo yalikuwa yakitumiwa kuwahangisha waislamu katika nchi yenye wahindu wengi. Mwanadiplomasia wa zamani wa India alisema huu ni mfano wa "kutoa nje" kwa masuala ya ndani.
Mizozo ya kidiplomasia inayoendelea kutokana na matamshi ya kuudhi yaliyotolewa na wanachama wawili wakuu wa BJP kuhusu Mtume Muhammad si ya kwanza kwa chama au serikali ya Modi kukabiliwa na shutuma za kimataifa kwa madai ya chuki dhidi ya Uislamu.
Miaka miwili iliyopita Mbunge wa BJP Tejasvi Surya alijikuta katikati ya dhoruba wakati tweet yake ya 2015 kuhusu wanawake wa Kiarabu iliposambaa. Wafanyabiashara mashuhuri, wanasheria na wachambuzi huko Dubai na Kuwait walilaani matamshi yake. (Bwana Surya alifuta tweet hiyo baadaye.)
Katika mkutano wa hadhara wa 2018, waziri wa mambo ya ndani wa India Amit Shah alisema kwamba raia wa Bangladeshi ambao waliingia India kinyume cha sheria walikuwa "wavamizi" ambao "wamekula nchi yetu kama mchwa".
Hili lilizusha dhoruba nchini Bangladesh yenye Waislamu wengi, ambapo waziri mkuu alielezea matamshi ya kiongozi wa pili mwenye nguvu wa India kama "yasiyotakikana na na yasiyo na maana". Mwandishi wa safu kutoka Bangladesh aliandika kwamba Bw Shah "alikuwa na historia ndefu ya kutoa matamshi ya chuki na matusi kuhusu Bangladesh".
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, India ilikumbwa na tsunami ya matamshi ya chuki ya viongozi wa Hindu wenye itikadi kali waliovalia mavazi ya zafarani dhidi ya jamii ya Waislamu milioni 200 nchini humo. Baadhi yao wamewahimiza waziwazi Wahindu kuchukua silaha na kutoa matamshi kuhusu mauaji ya kimbari ya Waislamu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Bw Modi aidha imedumisha ukimya, na kujikokota kujibu au kulaumu vitendo kama hivyo.
Haya yote yanaonekana kuwatia moyo Wahindu wa kawaida kuingia mtandaoni na kuwachafua Waislamu. Mnamo mwaka wa 2018, mpishi maarufu wa asili ya India aliyefanya kazi katika hoteli huko Dubai alifukuzwa kazi kwa kuchapisha tweet inayokosoa Uislamu. Wakati Wahindi wanaoishi Dubai walipoanza kutuma ujumbe wa Twitter dhidi ya Tablighi Jamaat mnamo 2020, mfanyabiashara wa ndani aliye na uhusiano na familia ya kifalme inayotawala alituma ujumbe kwamba "mtu yeyote ambaye ni mbaguzi wa rangi na ubaguzi katika UAE atatozwa faini na kulazimishwa kuondoka".
Wakati huu malalamiko yamekuwa ni makali - nchi 15, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Iran na Qatar, zimeilalamikia India.
Serikali ya Bw Modi imelazimika kumsimamisha kazi msemaji wake kwa matamshi yake. Ni ukumbusho kwamba "kuwalenga walio wachache bila kuadhibiwa, kutakuwa na madhara kwa sifa ya kimataifa ya India," asema Pratap Bhanu Mehta, msomi mkuu.
Hata hivyo viongozi wengi wa BJP wanaamini kuwa hasira hiyo itaisha hivi karibuni, na itakuwa biashara kama kawaida.

Chanzo cha picha, AFP
Licha ya hayo, India ina uhusiano jadi na wa kina na nchi za Ghuba. Baadhi ya Wahindi milioni 8.5 wanafanya kazi katika nchi sita za Ghuba zinazomilikiwa na Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC), zaidi ya mara mbili ya idadi ya Wapakistani, wafanyikazi wanaofuata kwa nafasi ya pili.
Wahindi pia huunda jumuiya kubwa zaidi ya wahamiaji katika kila moja ya nchi hizi. Wanatuma nyumbani takriban dola bilioni 35b kila mwaka pesa zinazosaidia wanafamilia milioni 40 nyumbani, wengi katika baadhi ya majimbo maskini zaidi ya India kama vile Uttar Pradesh inayotawaliwa na BJP. Biashara kati ya India na nchi za GCC ni takriban dola bilioni 87. Iraq ndio muuzaji mkubwa wa mafuta nchini India, ikifuatiwa na Saudi Arabia. Zaidi ya asilimia 4 ya gesi asilia ya India inatoka Qatar.
Waziri Mkuu Modi mwenyewe ameweka uhusiano na nchi za Ghuba kuwa kipaumbele. "India ina uhusiano mkubwa na nchi za Asia Magharibi katika suala la usalama wa nishati, ajira ya watu kama wahamiaji na pesa wanazotuma," anasema Srinath Raghavan, profesa wa historia na uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ashoka.
Wakati huu serikali ya Bw Modi, wataalam wanaamini, inaonekana kujibu kwa kuchelewa, lakini kwa uthabiti. "Inaonekana kuna kukiri kwamba mambo haya yakitokea kunaweza kuwa na madhara. Siasa za ndani na nje hazizuiliki. Serikali inapaswa kufanya uamuzi.













