Sheikh Mansour bin Zayed: Fahamu jinsi mmiliki wa Machester City anavyodaiwa kuwasaidia mabilionea wa Urusi kuhamisha utajiri wao kuelekea UAE

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Nje ya Falme za Kiarabu, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan anafahamika zaidi kuwa mmiliki wa klabu ya soka ya Uingereza ya Manchester City huku nyumbani, yeye ni naibu waziri mkuu na mwanachama maarufu wa familia inayotawala.

Lakini vyanzo kadhaa vinavyofahamu ushirikiano wa Abu Dhabi na Warusi, ambao waliomba kutotajwa majina, walisema katika ushahidi wao kwa Shirika la Bloomberg kwamba Sheikh Mansour pia ana jukumu nyuma ya pazia, jukumu ambalo limeongezeka umuhimu katika miezi ya hivi karibuni na anawakilishwa katika kusaidia kusimamia mahusiano na matajiri.

Warusi ambao wanafikiria kuhamisha fedha zao katika nchi za Falme za Kiarabu.

Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa, wakati Sheikh Mansour amekuwa akihusika kwa muda mrefu katika maendeleo ya uhusiano wa Emirate na Urusi, umuhimu na utata wa jukumu hilo umejitokeza tangu uvamizi wa Urusi huko Ukraine.

Kabla ya uvamizi wa Ukraine, Sheikh Mansour bin Zayed aliandamana na kaka yake, Mohammed, Mrithi wa Kifalme na mtawala mkuu wa Emirates katika mikutano mbalimbali na makampuni ya Urusi. Na mnamo 2019, alikuwepo wakati Mohammed bin Zayed alipokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Abu Dhabi.

m

Kabla ya uvamizi huo, Warusi pia walishika nafasi ya nne kati ya watalii walioongoza kwenda Dubai katika miezi miwili ya kwanza ya 2022, na watalii wapatao 137,000, zaidi ya mara mbili ya mwaka uliopita, ingawa ni chini ya viwango vya kabla ya janga, kulingana na serikali ya Dubai.

Baada ya uvamizi huo, Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine ziliifunga Urusi kwa maelfu ya vikwazo vipya vya kifedha, na kuifanya kuwa nchi iliyowekewa vikwazo zaidi duniani, lakini Umoja wa Falme za Kiarabu haukuweka vikwazo vyovyote.

Viongozi wa hapo walichukua msimamo kuwa Abu Dhabi inaheshimu sheria za kimataifa, lakini haitakiwi kufuata taratibu zinazotekelezwa na baadhi ya nchi.

Washirika wengine wa Marekani, pamoja na Israeli na India, wamechukua msimamo sawa na UAE kwa kusita kuweka vikwazo.

Lakini mbinu hii imewatia wasiwasi baadhi ya maafisa wa nchi za Magharibi ambao wana wasiwasi kuhusu mianya katika mipango yao ya vikwazo

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alikutana na mwenzake wa Emirate Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan huko Moscow mwishoni mwa Februari iliyopita.

Mapema mwezi huu, Naibu Waziri wa fedha wa Marekani, Wally Adeemo, aliibua wasiwasi wa Marekani kuhusu wafanyabiashara wakubwa wa Urusi wanaowatumia fedhai katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa njia ya simu na maafisa wa Emirate, watu wawili wanaofahamu majadiliano hayo waliiambia Bloomberg.

Wadadisi kadhaa wa habari waliiambia Bloomberg kwamba maafisa wakuu wa serikali, wafanyabiashara matajiri na wasimamizi wa fedha kutoka Urusi wanazidi kuwasiliana na Sheikh Mansour na ofisi yake ili kusaidia kuendesha shughuli za serikali katika UAE, na kuongeza kuwa Warusi wamevutiwa zaidi kuwekeza nchini humo tangu Urusi ilipovamia. Ukraine.

Vyanzo hivyo viliongeza kuwa baadhi wanatafuta kununua nyumba huko Dubai, huku wengine wanataka kununua magari ya kifahari au wanahitaji usaidizi wa kufungua akaunti za benki na makampuni ya kifedha.

Vyanzo hivyo viliendelea kuiambia Bloomberg kuwa Wizara ya Masuala ya Rais, inayoongozwa na Sheikh Mansour, imetoa msaada mkubwa zaidi tangu uvamizi huo.

Maafisa wa Emarati wanaona juhudi za Sheikh Mansour kama sehemu ya mkakati mkubwa wa serikali kuvutia biashara ya kimataifa na kudumisha uhusiano wa kimkakati na Mashariki na Magharibi.

Vyanzo hivyo vilisema kuwa uhusiano kati ya Urusi na UAE ni muhimu hasa kutokana na ushirikiano wao ndani ya muungano wa OPEC Plus wa nchi zinazouza mafuta.

Na Shirika la Bloomberg lilisema kuwa Wizara ya Masuala ya Rais wa Falme za Kiarabu haikujibu simu za kutaka maoni juu ya habari hii, na Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE ilikataa kutoa maoni.

Juhudi za kumpata Sheikh Mansour kupitia Manchester City na ofisi zake pia hazikufua dafu. Msemaji wa waziri wa fedha wa Marekani alikataa kutoa maoni yake.

Mapema mwaka huu, msemaji wa Ofisi ya Mtendaji wa UAE ya Kupambana na Utakatishaji wa fedha na Ufadhili wa Ugaidi aliiambia Bloomberg kwamba nchi itaendelea kutafuta ushirikiano wa kina na washirika wa kigeni katika kufuatilia mtiririko wa fedha wa kimataifa.

Je Sheikh Mansour bin Zayed ni nani?

Encyclopedia Britannica inasema kwamba Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan alizaliwa Novemba 20, 1970 huko Abu Dhabi, na ni mwanachama mashuhuri wa familia inayotawala katika Emirate ya Abu Dhabi, na mmoja wa wafanyabiashara mashuhuri nchini humo.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Aliwahi kuwa Mkuu wa Ofisi ya Rais wa UAE kati ya mwaka 1997 na 2004, na alikuwa Waziri wa Masuala ya Rais mnamo 2004. Anajulikana kimataifa kwa uwekezaji wake katika kandanda ya kulipwa, haswa ununuzi wake wa Manchester City FC.

Mansour bin Zayed ni mtoto wa Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan, ambaye aliwahi kuwa mtawala wa Emirate ya Abu Dhabi kati ya mwaka 1966 na 2004 na rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu kati ya 1971 na 2004.

Kaka yake Khalifa alikua mtawala wa Abu Dhabi na rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu mnamo 2004, na kaka yake Muhammad akawa mwanamfalme wa Abu Dhabi mnamo 2004 na mtawala mkuu wa Falme za Kiarabu mnamo 2014.

Mansour alijulikana sana kwa shughuli zake za kifedha kwani aliongoza mashirika kadhaa ya kifedha huko Abu Dhabi ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Benki ya Kwanza ya Ghuba (sasa ni sehemu ya Benki ya Kwanza ya Abu Dhabi), na Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji wa Petroli.

Aidha, alihudumu katika bodi za wakurugenzi wa mashirika mengine kadhaa likiwemo Baraza Kuu la Masuala ya Fedha na Uchumi.

Ana vitega uchumi vingi nje ya UAE, na Mansour pengine anajulikana zaidi kwa ubia wake wa soka nje ya nchi kupitia kampuni yake ya kibinafsi ya uwekezaji, Abu Dhabi United Group for Development and Investment, ambayo ilinunua hisa katika Klabu ya Soka ya Manchester City mnamo 2008 na klabu ikawa moja na kuwa miongoni mwa timu nyingi zilizo na mafanikio kwenye Ligi Kuu ya England.

Manchester City "iliyo na nguvu zaidi kifedha duniani"

Ingawa safari Manchester City bado ni ndefu, licha ya rekodi ya faida

Mnamo 2013, Mansour alikua mwekezaji mkuu katika New York City FC, na baadaye akanunua hisa katika vilabu vingine kadhaa ulimwenguni ikijumuisha hisa nyingi katika Jiji la Melbourne mnamo 2014 na Mumbai City mnamo 2019.

Encyclopedia Britannica inasema kwamba Mansour ana jukumu tulivu lakini muhimu katika sera ya umma ya Emirate pia. Kando na kazi yake kama waziri wa masuala ya rais, aliongoza Idara ya Mahakama ya Abu Dhabi, ambayo ilianza kusimamia mfumo wa kisheria wa emirate mnamo 2006.

Sheikh Mansour luxury yacht off the Turkish coast

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Boti ya kifahari ya Sheikh Mansour ikiwa katika ufukwe wa Uturuki

Pia, kama mkwe wa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai na waziri mkuu wa Falme za Kiarabu, Mansour pia anaweza kuongeza ushawishi wake kwa emirate ya pili kwa nguvu zaidi nchini. Mnamo 2009, aliteuliwa kuwa naibu wa Mohammed bin Rashid katika nafasi yake kama waziri mkuu.

Hata hivyo, mbali na mikutano ya hadhara ya hapa na pale na viongozi wengine na viongozi wa kigeni, uharakati wa Mansour katika masuala ya kisiasa nchini kwa kiasi kikubwa umebaki kutoonekana.

Mvutano na Marekani

Ijapokuwa UAE haijaweka vikwazo vyovyote kwa Urusi, baadhi ya Emirate, ikiwa ni pamoja na Khaldoon Al Mubarak, mtendaji mkuu wa mfuko wa utajiri wa uhuru Mubadala Investment Company, na Yousef Al Otaiba, balozi wa UAE mjini Washington, wamejaribu kuwatuliza Marekani, Uingereza. na maafisa wa Ulaya.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika mkutano wa kifedha huko Dubai mwezi uliopita, Mubarak alisema Mubadala ataepuka kuwekeza nchini Urusi kwa wakati huu, na kuwa mkuu wa kwanza wa hazina ya utajiri katika Mashariki ya Kati kutoa maoni kwa umma juu ya vita.

Mubadala, ambaye Sheikh Mansour ni makamu mwenyekiti, alisema katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwamba imesitisha kwa muda uwekezaji wowote wa ziada nchini Urusi "kutokana na hali hiyo", lakini hakutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo, maafisa wa Magharibi walikaribisha maoni kutoka kwa Mubadala, wakiyaona kama ushahidi wa wasiwasi wa UAE kuhusu adhabu ya pili kwa mtu yeyote anayeshughulika na vyombo vya Urusi vilivyoidhinishwa.

Kwa hakika, uhusiano kati ya UAE na Marekani umedorora hivi karibuni huku UAE na Saudi Arabia zikiitaka Marekani kufanya jitihada zaidi kukabiliana na mashambulizi ya makombora ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen.

Wakati huo huo, nchi hizo mbili za Ghuba hadi sasa zimekataa ombi la Washington la kuongeza uzalishaji wa mafuta ili kupunguza bei.

Saudi Arabia na UAE bado zimejitolea kutochukua upande wowote katika operesheni ya kijeshi ya Urusi iliyoanza nchini Ukraine mnamo Februari 24.

Wengi wa washirika wa Washington katika Mashariki ya Kati huepuka kuchukua misimamo ambayo inaweza kuathiri vibaya uchumi wao, na nchi za eneo hilo pia zimekuwa na uhusiano wa kimkakati na China na Urusi.

Tangu kuzuka kwa vita vya Ukraine, Saudi Arabia na UAE zimekabiliwa na shinikizo la Marekani la kuongeza uzalishaji wa mafuta na mauzo ya nje ili kuzuia ongezeko jipya la bei ya mafuta, ambapo imefikia chini ya dola 140 kwa pipa.

Sera ya mashinikizo kati ya Marekani na kila taifa la Falme ya Kiarabu na Saudi Arabia inadhihirika kwa kutofuata vikwazo vilivyowekwa na utawala wa Marekani dhidi ya Urusi na kuendeleza miamala ya kifedha na benki za Urusi.

Wachambuzi wa masuala ya nishati wanaamini kuwa Saudi Arabia na Emirate hazitajibu matakwa ya Marekani ya kuuza nje viwango vya ziada vya mafuta kwenye soko la kimataifa.

UAE, ambayo ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa mafuta katika OPEC baada ya Saudi Arabia na Iraq, imejitolea kwa sera za mafuta za Saudi, ndani ya shirika na katika muungano wa "OPEC Plus".

Suhail bin Muhammad Faraj Al Mazrouei, Waziri wa Nishati na Miundombinu wa UAE, alithibitisha katika taarifa yake kwa wakala wa WAM wa UAE kwamba nchi yake imejitolea kwa makubaliano ya "OPEC Plus" na utaratibu wake wa sasa wa kurekebisha uzalishaji wa kila mwezi.

m

Chanzo cha picha, EPA

Waangalizi wa mambo wanaamini kwamba msimamo huu wa Emirate lazima uwe umechukuliwa kwa uratibu na Saudi Arabia, na kwamba nchi hizo mbili zinakataa kuchukua maamuzi ambayo yangemdhuru mshirika wao, Urusi, ndani ya muungano wa "OPEC Plus".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alikutana na mwenzake wa Emirate Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, huko Moscow mwishoni mwa Februari iliyopita.

Mnamo Machi 18, Rais wa Syria Bashar al-Assad, mshirika wa Moscow, alitembelea UAE, ambapo alikutana na Mrithi wa Kifalme wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed bin Zayed, ambaye alisisitiza kwamba Syria ni nguzo muhimu ya usalama wa Waarabu, na kwamba UAE inapenda kuimarisha ushirikiano nayo katika suala la kutoa msaada wa Kisiasa na kibinadamu, pamoja na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Sheikh Mansour bin Zayed alihudhuria mkutano huo, ambao ulidhihirisha ukosoaji nchini Uingereza.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa ziara hiyo imekuja wakati ambapo Mashariki ya Kati inashuhudia mabadiliko ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na baadhi ya nchi za Kiarabu zikitaka kufufua uhusiano wao na Assad, na wanaona kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya faili la Syria na Uvamizi wa Urusi kwa Ukraine.

Washington ilitangaza Machi 19 kwamba "imesikitishwa na kusikitishwa sana" na ziara ya Rais Bashar al-Assad wa Syria katika UAE, wakati ambapo Urusi, mshirika wa Syria na nchi ambayo inadumisha uhusiano mkubwa na UAE, inaendelea na mashambulizi yake. juu ya Ukraine tangu Februari 24.

Kwa hivyo, inaonekana kwamba Saudi Arabia na UAE zinataka kuondoka kutoka kwa upande wa vita vya Ukraine.