Je wanawake ni bora kuliko wanaume katika kusimamia jamii na nchi?

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Unajisikiaje unapokuwa kiongozi katika ulimwengu wa wanaume?

Je, wanawake wanakabiliwa na changamoto gani wanaposhika nyadhifa za uongozi?

Na wanafanya nini tofauti kama viongozi?

BBC ilihoji muungano wa viongozi wanawake nchini Finland kuhusu uongozi, ili kujua jinsi wanavyoweka uangalifu wanapofanya maamuzi na kuweka malengo ya siku zijazo.

Dk. Nela Smolovic-Jones anasema akijibu swali: Je, ungependa kuongozwa na timu ya wanawake wote? Je, unajisikiaje kuwa kiongozi katika dunia inayoongozwa na wanaume?

"Kuna hatari kubwa inayohusishwa na kuchukua nafasi za uongozi wakati wewe ni mwanamke, kwa sababu hukumu hutolewa dhidi yako mapema kwa sababu ya jinsia yako."

Hapa, tutaangalia kile kinachohitajika ili kuwa kiongozi. Inaweza pia kuwa na mengi

Picha ambayo iligonga vichwa vya habari duniani kote ya viongozi wa serikali mpya ya mseto ya Finland, ilikuwa ya kipekee katika masuala ya jinsia na ilionyesha misimamo yao ya kisiasa na mtindo wa uongozi.

Viongozi hao watano ni wanawake, wote chini ya miaka 35 walipochukua madaraka, isipokuwa mmoja, Sanna Marin, ambaye alikuwa na umri wa miaka 34 alipokuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini Finland.

Finland ina rekodi inayoongoza katika masuala ya haki za wanawake.

Ilikuwa ni nchi ya kwanza duniani kutoa haki kamili kwa wanawake, na wanawake kushika nyadhifa za uongozi.

Wanawake wanasema kuna mapungufu wakati timu inayoongoza ni ya wanawake wote.

Ahadi za kutekelezeka

"Kiukweli, hatutaki kutumia mifumo ile ile ambayo wanaume walitumia, lakini badala yake kubadilisha miundo hiyo kwa kiasi fulani," anasema Sanna Marin, Waziri Mkuu wa Finland.

Kulikuwa na kutoelewana kati ya viongozi, lakini Finland, kama nchi zingine zinazoongozwa na wanawake, ilipata sifa kwa kukabiliana vyema na janga la coronavirus.

Serikali inazindua mpango unaoahidi wa usawa ambao unajumuisha haki zaidi kwa watu waliobadili jinsia, kuwahimiza akina baba kushiriki majukumu ya malezi na kuziba pengo la utofauti wa mishahara kutokana na kijinsia.

Je, tumejifunza nini kutokana na uzoefu wa Finland kuhusu uongozi wa wanawake katika ulimwengu wa wanaume ?

Ellen Johnson Sirleaf

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ellen Johnson Sirleaf

"Viongozi wa muungano wana aina ya uelewa wa kutohusishwa, kutengwa na kuishi katika matatizo," anasema Nela Smolovic-Jones. "Na nadhani hiyo pia inawafanya kuelewa na kuthamini utunzaji zaidi, pamoja na ujumuishaji na mshikamano

Kwa hivyo, je, viongozi wanawake uzingatia maamuzi wanayofanya na malengo wanayoweka?

"Ndiyo, lakini kwa kweli kufanya kazi kwa lengo hilo kunahitaji uvumilivu, kwenda zaidi ya tofauti na migogoro na kujaribu kutafuta njia ya kuzunguka tofauti, kama vile misimamo ya kisiasa, imani, mitazamo, nk," anasema Smolovic-Jones.

"Kwa hiyo, nadhani wanawake wamewekwa kufanya kazi kwa njia hii tangu umri mdogo, na hawakati tamaa katika kikwazo cha kwanza wanachokutana nacho, wanavumilia."

Mama Merkel, wakimbizi, mwanamke wa chuma ambaye kwa hiari yake aliacha uongozi wa chama chake.

Viongozi wanawake wa Finland wana misimamo na imani tofauti za kisiasa, kwa hivyo wanasuluhisha vipi tofauti zao pamoja?

"Kuna hatari kubwa inayohusishwa na kuwa katika nafasi za uongozi wakati wewe ni mwanamke, kwa sababu unahukumiwa kwa upendeleo wa kijinsia," Smolovic-Jones anasema.

Kwa hivyo, ikiwa kwa sababu fulani, kwa mfano, muungano wa Wafini watano utashindwa, au umeshindwa kutekeleza ahadi ulizojitolea, wanaweza kuhukumiwa kwa ukali zaidi kuliko wenzao wa kiume, na wanasiasa, vyombo vya habari au wapiga kura wao.

Maelezo ya video, Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

Kwa hiyo, viongozi wa kike wanahukumiwa kwa ukali zaidi kuliko viongozi wa kiume na kukabili upendeleo huu wa kijinsia, si ni haki?

"Janga hilo, au mzozo wa kifedha, au mzozo wa hali ya hewa, uliweka wazi kuwa nchi inahitaji aina hii ya uongozi na matunzo ili kuweza kuimaliza," anasema Smolovic-Jones, na kuongeza, "Nadhani ndio sababu hii. Uongozi wa wanawake unasukumwa mbele.Unaweza kukua zaidi katika siku zijazo.

Kwa hivyo, sifa za uongozi zinazohusishwa kijadi na wanawake, kama vile kuwajali wengine na kufanya kazi pamoja, zimethibitishwa kuwa na mafanikio katika kushughulikia migogoro ya kimataifa pia.

BBC pia alimhoji Meggie Palmer, ambaye alianza maisha yake kama mwandishi wa habari lakini hivi karibuni aligundua kuwa alikuwa na hadithi tofauti ya kusimulia.

Wanawake kote ulimwenguni kwa ujumla hulipwa fedha kidogo chini ya wanaume na hawashikilii nyadhifa nyingi za juu katika makampuni.

m

Meggie aliamua kufanya jambo kuhusu hilo, kwa kuunda programu inayoitwa PepTalkHer ambayo inafunza wanawake jinsi ya kupata malipo ya haki na kutetea usawa wa kijinsia na usawa katika nyadhifa kuu.

Lengo lake ni kumaliza pengo la mishahara na kuwasaidia wanawake kuwa viongozi wa ndoto zao.

"Kwa kweli nimepata uzoefu mzuri kama mwanamke katika nafasi ya uongozi," Palmer anasema. "Wanaume na wanawake wengi wamenisaidia kufikia vyeo vya juu katika biashara niliyofanya. Lakini kwa upande mwingine, nimekuwa na uzoefu mbaya katika sehemu ya kazi, kama vile mtazamo na tabia zisizofaa na mimi. Kuzungumza nami tofauti na kunitendea tofauti, kwa sababu mimi ni mwanamke."

Palmer anasema amepata uzoefu wa usawa wa mshahara katika kazi yake.

"Niligundua kuwa nalipwa mishahara kidogo kuliko wenzangu wa wanaume, na vigezo na masharti ya kazi yangu yalikuwa tofauti ukilinganisha na wao, haukupenda, unaweza kujiuzulu au kutushtaki."

"Hiyo ilikuwa miaka michache iliyopita, natumani mambo yamebadilika kwa kiasi fulani sasa, kutokana na kwamba pengo hili la malipo ya kijinsia bado lipo duniani kote hadi leo," anasema.

Meggie alikuwa na uzoefu wake wa kulipwa kidogo kuliko wenzake wa kiume, kwa hivyo alitaka kufanya jambo kuhusu hilo.

Palmer anasimulia uzoefu wake: "Kuwa mtu wa pekee popote kunakufanya ujisikie mpweke, sivyo? Ikiwa wewe ndiye mtu pekee wa rangi au mwanamke pekee mahali pa kazi, hiyo inakufanya ujisikie mpweke, na ndivyo viongozi wanawake wanavyosema. mimi - kuwa mpweke kama mimi." .

Sasa nahudumu kwenye bodi za mashirika yasiyo na faida ya wanaume na wanawake, na nimepata uzoefu na kuibua masuala hapa pia, haswa yale yanayohusiana na wanawake, lakini bado nasikia juu ya tetesi na kero zote za wanaume mimi, na ninapata usaidizi mdogo sana kutoka kwa mjumbe wa bodi wa kike.

Idadi yetu ni ndogo. Wakati idadi yako sio kubwa, ni ngumu sana kufanya mabadiliko yoyote, kwa hivyo inakuwa ya kukatisha tamaa, lakini ni jambo lisiloepukika na tunahitaji kuendelea kulizungumza na kulikuza suala hilo hadi lengo tunalotaka litimie."

Maelezo ya video, Finland inaongozwa na muungano wa vyama vitano

Baada ya yote, Meggie anajua maana ya kuwa na mwanamke mmoja tu katika chumba cha mikutano, na viongozi mara nyingi wanaweza kuhisi upweke na kutengwa.

"Kwa hiyo, tunapofikiria ni nani anayehusika na kuboresha hali hizi? Jibu ni sisi sote."

Hili si tatizo ambalo wanawake pekee wanapaswa kulitatua, na si uongozi pekee unaoweza kutatuliwa, ni tatizo ambalo sote tuna wajibu wa kulitatua.

Unapokuwa katika usimamizi wa kati na unaajiri, unaweza kusema, "Nataka kuhakikisha kuwa ninawahoji wagombea wa kiume na wa kike," na unapohoji, unaweza kuuliza shughuli, "Je! sera za mahali hapa ili kuhimiza utofauti kwenye timu.

Meggie anasema , mabadiliko ni jukumu la kila mtu, na kila mtu katika kila ngazi anapaswa kuuliza maswali ambayo yatasababisha usawa zaidi mahali pa kazi.

Meggie anafafanua hoja yake: "Tunafahamu kwamba kunapokuwa na wanawake katika uongozi, makampuni hufanya vizuri zaidi.

Tunajua kwamba makampuni yanayoanza yanayoongozwa na wanawake yanaleta faida kubwa kwa wawekezaji, ikilinganishwa na makampuni yanayoongozwa na wanaume pekee.

Tunajua pia kwamba tunapoangalia makampuni makubwa yanayoendeshwa na wanawake, msingi wao unapanda, na tunagundua kuwa kwa wanawake katika uongozi, maamuzi wanayofanya yana nguvu na ufanisi zaidi."

Utafiti unaonesha kwamba makampuni yenye wanawake katika nafasi za uongozi hufanya vizuri zaidi.

Kwa hivyo, tumejifunza nini kuhusu wanawake katika uongozi?

Wanakabiliwa na chuki zaidi na hatari kwa sifa zao, lakini wana uwezekano wa kutanguliza utunzaji na huruma katika kufanya maamuzi na wanaweza kufanya kampuni na serikali kuwa na ufanisi zaidi.