Jinsi taka za miwa na nazi zilivyegeuka kuwa fursa

    • Author, Omary Mkambara
    • Nafasi, Mwandishi BBC Swahili

Uzalishaji wa takataka zinazotokana na shughuli za kila siku za binadamu zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika nyakati amabyo dunia inakabiliwa na mabadiliko tabia nchi.

Lakini kwa sasa takataka zinazotoka na maganda ya miwa na mabufuru ya Nazi zimegeuka kuwa fursa kwa vijana visiwani Zanzibar.

Uwepo wa Kiwanda kidogo kinachozalisha mkaa unatokanao na takataka za mabufuru ya madafu na Makumbi pamoja na Maganda ya Miwa umefanya takataka zote zinazozalishwa kuokotwa na kuuzwa.

Vijana katika maeneo ya majini kisiwani Unguja wamekuwa wakikusanya Mabufuru ya madafu kutoka sehemu ambazo vinauzwa madafu na kukusanya pamoja na maganda ya miwa ambayo kwa wingi yanapatikana katika sehemu ambazo wanafanya shughuli za kukamua sharubati ya miwa.

Ukusanyaji wa takataka hizo umekuwa ukifanya na aidha na vikundi vya vijana au kijana mmoja mmoja kwa kutembea katika maendo yanayotupwa taka na kukufanya na kisha kwenda kuziuza.

Kambi Othumani ni miongoni mwa vijana wanaokusanya takataka hizi na kuziuza kwa kiwanda kinachozalisha mkaa anasema takataka zinamsaidia kupata kipato.

'' Biashara ya takataka ya mabufuru ya madafu ni biashara nzuri inatusaida katika kujikwamua kiuchumi wanakuja hapa tunawauzia wao wanapata na sisi tunapata ''

Vijana wanaofanya shughuli ya kukusanya takataka na kuuza wanauza kila mfuko mmoja wa kilo ishirini wa takataka kwa kiasi cha shilingi elfu tano.

Miliki wa kiwanda cha mkaa mbadala Buheti Juma amelezea kuwa uzalisha wao wa mkaa umesaidia sana kuweza kusafisha mji wa Unguja kwa kukusanya takataka wao wenyewe lakini pia kutoa ajira kwa vijana ambao wanauza takataka katika kiwanda hicho.

'' Tunasafisha mji kwa kuokoata takataka zinazozalishwa kila siku lakini pia tunaongezea thamani hizo takataka ambazo miaka ya nyuma hazikuwa na kazi ziliachwa na kufanya maneno kuwa machafu lakini pia tumefungua fursa mpya ya watu kupata kipato kutokana na kutuuzia takataka''.