Saul 'Canelo' Alvarez amchapa Plant na kuwa bingwa asiyepingika

Chanzo cha picha, Getty Images
Bingwa wa dunia wa ndondi wa uzani wa super-middle Saul 'Canelo' Alvarez ameweka historia mjini Las Vegas baada ya kumchapa Caleb Plant na kuwa bingwa wa dunia wa uzani huo bila kupingwa.
Bondia huyo alimchapa kwa 'knocked out' bond Plant katika raundi ya 11 na kuzoa mikanda mikubwa minne katika kipindi kifupi cha miezi 12.
Alvarez anayetokea Mexico kabla ya pambano hilo alikuwa na mikanda mitatu ya WBA Super, WBC na WBO, sasa baada ya kumchapa Plant ameongeza mkanda mwingine wa nne wa IBF.
Alvarez alimwangusha Mmarekani huyo mara mbili katika raundi ya 11 - kwanza kwa konde la kushoto kabla ya kumtandika 'uppercut', liliohitimisha ubabe wa Plant.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Alitaka kuendelea. Nikamwambia hakuna aibu. Bila shaka niliibuka kidedea," alisema Alvarez, ambaye aliungwa mkono na umati wa mashabiki kwenye ukumbi wa ndondi wa Las Vegas alipokuwa akishinda. Kutokana na ushindi huo sasa Alvaarez atakuwa ameshinda mapambano 57, akipoteza moja na kutoka sare mawilii, kati ya hayo aliyoshinda ameshindwa kwa 'knockouts mapambano 39. Kwa upande wake Plant ameshindwa kwa mara ya kwanza.
"Caleb ni mpiganaji mzuri. Alikuwa mpinzani mgumu na mwenye uwezo mkubwa na ninamheshimu.
"Alikuwa akifanya pambano kuwa gumu sana, lakini Eddy [Reynoso, mkufunzi] aliniambia nishikilie tu kwenye mpango wa mchezo katika raundi mbili zilizotangulia. Mwishowe, nilimpata. Hiyo ndiyo njia ambayo ilibidi kumaliza. Tayari alikuwa ameumia na nikamaliza mchezo."











