Wafahamu wanandondi 3 kutoka Afrika wanaovuma Ulaya licha ya kupitia changamoto

Maelezo ya video, Wafahamu wanandondi 3 kutoka Afrika wanaovuma Ulaya licha ya kupitia changamoto

Mcameroon Francis Ngannou ambaye alinusurika kama mhamiaji, alipovuka bahari ya Mediterranian kwa mtumbwi na kuishi katika mitaa ya jiji la Paris hadi kuwa namba mbili katika mapambano ya UFC ya uzani wa juu duniani, Kamaru Unman alipambana na tatizo la kufugwa kwa baba yake na kumpoteza mtu wa familia hadi kuwa bingwa wa uzani wa welter, huku Israel Adesanya akipanda hadi kuwa bingwa wa uzani wa kati baada ya kukumbwa na ubaguzi wa rangi na kuzomewa wakati alipokuwa katika miaka ya sekondari.