MC3R: ‘Kihisio’ kwenye ubongo kinachosababisha urefu wa binadamu, kwa mujibu wa utafiti

aa

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasayansi wanasema kwamba fumbo la wanadamu kuwa warefu na kufikia balehe mapema kuliko zamani sasa linaweza kubainishwa kwa kihisio 'sensor' iliyopo kwenye ubongo wa mwanadamu.

Pamoja na lishe kuwa bora katika karne ya 20, wastani wa urefu wa watu nchini Uingereza kwa mfano umeongezeka kwa sentimita kumi wakati katika nchi nyingine urefu wa watu umeongezeka kwa sentimita ishirini.

Kwa nini utofauti huo unatokea, bado haijaeleweka. Wataalamu nchini Uingereza wanasema utafiti huu wa sasa unaweza kufungua njia ya dawa za kuimarisha misuli na kuzuia kuzeeka.

Wanasayansi wanajua kwamba chakula kizuri ama lishe bora kinamchango kwenye urefu wa mtu. Kwa mfano, Korea Kusini, nchi maskini zaidi iliyoendelea sasa, watu wake halisi wa huko wamekua warefu kuliko hapo awali.

Katika sehemu nyingi za Kusini mwa Asia na Afrika urefu wao unaongezeka angalau kidogo kuliko hapo awali.

Wanasayansi tayari wamebaini kwamba ishara hufikia sehemu ya ubongo inayoitwa 'hypothalamus' kupitia chakula. Ishara hii inaujulisha ubongo kuhusu lishe ya mwili na kuharakisha ukuaji wa mwili.

ss

Chanzo cha picha, Thinkstock

Utafiti huu mpya umechapishwa katika jarida la sayansi na utafiti 'Nature'. Utafiti huo ulifanywa na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Cambridge kwa kusaidiana na wataalamu kutoka vyuo vikuu vya Queen Mary, Bristol, Michigan na Chuo Kikuu cha Vanderbilt.

Utafiti huu umegundua uwezo wa kipokezi kinachoitwa MC3R. Pamoja na chakula, kipokezi hiki kina jukumu muhimu katika uongezekaji wa urefu wa mwili hasa wakati wa ujana.

Stephen O'Reilly, mwandishi wa utafiti huo na profesa katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alisema kuhusu kifaa 'hiki' kisichoshikika: "Huuambia mwili kuwa mwili uko katika hali ya ukuaji. Kuna chakula kingi mwilini. Kinauambia ni wakati wa kuwa na watoto."

"Sio uchawi huu, ni kweli hutokea na tunao mpango mzima," anasema O'Hareley.

Je, hii hutokeaje?

Kwa mujibu wa utafiti huo, wakati vipokezi vya ubongo havifanyi kazi ipasavyo, watu huwa wafupi.

Utafiti huo pia uligundua mabadiliko ya maumbile kwa watoto wengi. Vipokezi vilizuiwa kwa watoto hawa, hivyo watoto hawa walikuwa wafupi kwa umbo na wakawa na uzito mdogo.

Mabadiliko haya sio tu kwa wanadamu. Kulingana na watafiti, utafiti huo ulifanywa kwa panya na wanyama wengine.

bb

Chanzo cha picha, Getty Images

Watafiti hawa wanasema walichobaini katika utafiti huu ni kwamba unaweza kutatua matatizo mengine kama vile ukosefu wa ukuaji wa watoto na kuchelewa kubalehe.

"Utafiti wa siku zijazo unapaswa kuangalia ikiwa kalori za mwili zinaweza kutumika kujenga misuli bora kwa kutumia MC3R ili kuboresha utimamu wa mwili wa wagonjwa," alisema Profesa O'Hareley.

Wanasayansi tayari wamegundua kipokezi kinachodhibiti hamu ya kula. Hikii kinaitwa MC4R. Watu ambao wana upungufu ndani yake mara nyingi huwa ni wanene wa kupindukia.

Je, watu wanaweza kukua bila kikomo?

Kuna kikomo cha urefu wa mwanadamu. Ukomo hu unahusiana na lishe na afya zao.

Ikiwa watoto wa familia maskini wanapata chakula na kalori za kutosha, na wao pia wanaweza kukua kufikia urefu waliorithi kutoka kwa wazazi, babu na nyanya zao.

Pia watu warefu wana uwezekano mdogo wa kuteseka na ugonjwa wa moyo.

hh

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata hivyo, binadamu hawawezi kuishi muda mrefu. Katika karne iliyopita, kama ilivyokuwa kwa nchi zingine za Ulaya, urefu wa watu wa Uingereza pia umeongezeka. Lakini takwimu za miaka kumi iliyopita zinaonyesha kuwa urefu wa wastani hauongezeki.

Katika karne iliyopita, wanawake wa Korea Kusini na wanaume wa Irani wamekua warefu ulimwenguni, lakini watu warefu zaidi duniani ni wanaume waliozaliwa Uholanzi na watu wafupi zaidi duniani ni wanawake waliozaliwa Guatemala.