Fahamu kwanini kimo cha watu warefu zaidi duniani nchini Uholanzi kimeanza kupungua?

Kwa miongo mingi, Uholanzi imekuwa na watu warefu zaidi duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa miongo mingi, Uholanzi imekuwa na watu warefu zaidi duniani.

Kwa miongo mingi, Uholanzi imekuwa na watu warefu zaidi duniani.

Tangu mwaka 1958, Uholanzi imekua ikiongoza , kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi kuu ya takwimu (CBS).

Hata hivyo utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba urefu wa kizazi chake cha mwisho umepungua kwa wastani wa sentimita 1 kwa wanaume na 1.4 kwa wanawake ukilinganisha na kizazi kilichopita.

Licha ya sababu kadhaa zilizosababisha urefu wa waholanzi kupungua kutajwa, hakuna hata moja inayowaridhisha wataalam.

.Karne ya utata wa ukuaji wa vimo kwa uholanzi

CBS hufanya tafiti za afya kila baada ya miaka minne ambayo ni pamoja na kipimo cha urefu.

Mwaka 2020, Wanaume wa kiholanzi wenye umri wa miaka 19 walifikia urefu wa sentimita hadi 182.9 cm, wakati wanawake wa umri huo huo walifikia urefu wa sentimita 169.3.

Hili limeendelea na kuwa endelevu tena kwa haraka, wanaume waliozaliwa mwaka 1980 urefu wao uliongezeka kwa wastani wa sentimita 8.3 ukilinganisha na wale waliozaliwa mwaka 1930. Vivyo hivyo, kwa upande wa wanawake urefu wao uliongezeka kwa Sentimita 5.3 zaidi katika kipindi hicho hicho.

"Tunakunywa maziwa kwa wingi katika nchi hii," Ruben van Gaalen, mtafiti wa takwimu kutoka CBS na Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam, aliiambia BBC kama moja ya sababu zinazoelezwa za urefu wa watu wa Uholanzi.

Hata hivyo alisema kuwa zipo nadharia zingine kadhaa. "Inaweza kuwa kiwango (bora) cha maisha. Tukiangalia orodha ya maendeleo ya binadamu ya nchi zote, Uholanzi ni miongoni mwa nchi za kwanza kwanza. Denmark, pia wako juu. "

Lakini pia iligusia kuhusu jambo la asili. Kwa upande mmoja, kuwa na kimo kikubwa kunamsaidia mtu kuona mbali zaidi.

Pia kumekuwa na tafiti kuhusu uhusiano kati ya urefu na kipato. "Unavyozidi kuwa mrefu, ndivyo unavyozidi kutengeneza pesa."

'Kama ni mtu mrefu inakupa mamlaka makubwa na pengine utasikilizwa zaidi na watu, unapata upendeleo zaidi kwenye jamii," alifafanua na kuongeza kwamba, kwa ujumla wanawake wanavutiwa na wanaume warefu kuliko wao, kwa hiyo wanakuwa na uwanda mpana wanapochagua wapenzi'.

Nchini Uholanzi ni kawaida kuona wanawake wakiwa na kimo cha urefu wa sentimita 1.80 au zaidi ya wanaume wao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Nchini Uholanzi ni kawaida kuona wanawake wakiwa na kimo cha urefu wa sentimita 1.80 au zaidi ya wanaume wao.

Sababu za kupungua kwa urefu wa waholanzi

Kwa sasa, hata hivyo, ukuaji wa watu wa Uholanzi ama kuongezeka kwa urefu wao kumepungua, kwa mujibu wa utafiti mpya wa CBS kupitia vipimo vilivyotolewa na watu binafsi wapatao 719,000 wenye umri wa kati ya miaka 19 na 60.

Matokeo ya utafiti huo unaonyesha kwamba wanaume waliozawa mwanzoni mwa milenia ambao sasa wana miaka 19 urefu wao umepungua kwa wastani wa sentimita 1 ukilinganisha na wenzao wa umri huo waliozaliwa kwenye miaka ya 1980s. Wakati wanawake wenyewe urefu umepungua kwa sentimita 1.4.

Watalaam wametoa maelezo kadhaa kama sababu za kupungua huko kuanzia suala la kuongezeka kwa wahamiaji, mabadiliko ya ulaji na athari za majanga ya kiuchumi.

"Uhamiaji ni moja ya sababu. Kama sisi ni watu warefu duniani, maana yake, wahamiaji wanaoingia ni wafupi, hivyo maumbile yao ni ya watu wafupi," ilisema taarifa ya CBS.

"Lakini kusuasua kwa urefu wa waholanzi kulirekodiwa katika vizazi ambavyo wazazi wawli waliozaliwa Uholanzi, na pia vizazi ambayo mababu na mabibi zao wamezaliwa nchini humo,".

Uhamiaji ni moja ya sababu zilizosababisha urefu wa vimo vya wholanzi kupungua.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uhamiaji ni moja ya sababu zilizosababisha urefu wa vimo vya wholanzi kupungua.

Uhamiaji ni moja ya sababu zilizosababisha urefu wa vimo vya wholanzi kupungua.

Aidha, CBS alibainisha kwenye tovuti yake kwamba wanaume wasio na historia ya uhamiaji hawakuongezeka urefu sana na wanawake wasio na historia ya uhamiaji walionyesha mwenendo wa chini ama urefu kupungua kiasi.

Nadharia nyingine inayowezekana ambayo mtaalam Ruben van Gaalen anaisema ni kwamba kupungua kwa wastani wa urefu kunaweza kuwa kutokana na kikomo cha kibiolojia: kwamba mtu hawezi kukua tena.

Lakini kinachowatia wasiwasi wataalam zaidi ni kwamba inawezekana ikawa ni kutokana na mabadiliko ya maisha na ongezeko la matumizi ya 'wanga' wakati wa ukuaji wa vijana," Van Gaalen alisema na kuonya kwamba ka aukuaji unaathiriwa na maisha duni ya kiafya, inapaswa kuchunguzwa kwa sababu inahusiana na maisha ama umri wa mtu kwenye maisha.

"Hatuvuti sigara lakini tuna maisha ya kubweteka na kutumia zaidi wanga unaotupa uzito. Kwa hivyo athari isiyo ya moja kwa moja ya kutokuwa na warefu zaidi kama huko nyuma inaleta wasiwasi zaidi kuliko hali ya kutokuwa warefu. "

Vipimo vya kimo cha watu

Chanzo cha picha, BBC REEL