Kugandisha mafuta: 'Hiki ndicho kilichonitokea nilipogandisha mafuta ya mwili'

A photo of Ailsa Burn-Murdoch

Chanzo cha picha, AILSA BURN-MURDOCH

Maelezo ya picha, Ailsa amefanyiwa tiba ya kugandisha mafuta sawa na mwanamitindo Linda Evangelista

Kuondoa mafuta mwili kwa kugandisha 'Fat-freezing' kwa sasa ni maarufu, huku ikikadiriwa watu zaidi ya milioni nane wamefanyiwa huduma ama tiba hii kwenye kliniki au Spa duniani kote. Lakini kwa sasa taarifa zimetapakaa zaidi kwa sababu tofauti.

Mwanamitindo wa Canada Linda Evangelista, anayejulikana kama mmoja wa wanamitindo wakubwa wa asili kuanzia miaka ya 1990, kufungua kesi akitaka kulipwa dola $50 mil akidai tiba hiyo "imeharibu muonekano wake".

Anasema amepata madhara yanayoitwa kitaalamu paradoxical adipose hyperplasia (PAH) - ambayo ni adimu yanayosababisha "kuonekana tofauti kabisa na vile ilivyokusudiwa", inaongeza seli za mafuta, ambazo ni hatari, anadai kwamba hakuna madhara hayo kabla ya kufanyiwa tiba hiyo.

Kampuni ambayo Linda anadai imemuhudumia kumpa tiba hiyo haijajibu maombi ya BBC kuhusu madai hayo. Kwa sasa imeandika kwenye mtandao wake kwamba "matokeo kwa wagonjwa yanaweza kutofautiana na madhara adimu yanaweza kutokea", kitu ambacho mawakili wa Evangelista wanasema wamekiongeza hivi karibuni baada ya mteja wao kupatiwa tiba hiyo

Sasa nini madhara ya tiba hii na inahusisha nini hasa, huu ni uzoefu wa watu watatu.

'Nilijisikia kama nanyonywa na mashine ya usafi ya upepo'

Fat-freezing procedure in cosmetic salon, belly close-up

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tiba hii inalenga kuondoa mafuta ambayo kawaida hupatikana chini ya tumbo, mgongoni, mapajani, mikononi kwa juu na chini ya kidevu

Taratibu za urembo za ina hiyo sio mpya kwa Ailsa Burn-Murdoch, 39 wa Uingereza.

Amekuwa akihaha na muonekano wa mwili wake tangu akiwa binti mdogo na alipofikisha miaka 21 aliamua kufanyiwa upasuaji kurekebisha muokeno wake na kupandikiza matiti, lakini alifanya hivyo kwa siri bila familia na marafiki kujua.

"Sikupaswa kufanyiwa upasuaji,nilikuwa binti mdogo sana" aliambia BBC.

Safari yake ya kwenda Caribbean, ilichocheza hofu yake ya zamani kuhusu kuonyesha mwili wake, kwa hivyo akaamua kupata tiba ya kugandisha mafuta mwaka jana , akifanya hivyo mara tatu katika kipindi cha miezi mitatu, mgongoni, tumboni, mikononi na mapajani.

A photo of a woman's back with bruising

Chanzo cha picha, AILSA BURN-MURDOCH

Maelezo ya picha, Ailsa alipiga picha hii muda mfupi baada ya tiba yake ya kwanza ya kugandisha mafuta

Ailsa alitumia jumla ya dola $875 kwa ajili ya tiba hiyo.

Gharama ya tiba hiyo kwa Uingereza inaweza kuwa kati ya dola $545 mpaka $1090 kwa tiba ya mara moja, inategemea na mara ngapi na maeneo gani ya mwili yanatibiwa. Alisema yeye alifuata tiba ya bei rahisi kabisa.

Ailsa anasema kabla ya kufanya hivyo hakuwahi kushauriana na alikutana na mtu wa kumfanyia tiba hiyo siku hiyo hiyo aliyopaswa kufanyiwa.

Tiba hiyo inachukua dakika 45 kwa kila eneo, na kwenye eneo ambalo mafuta yanagandishwa ili yatoke, kunawekwa vitu vinavyovuta.

"Nilihisi kama nanyonywa na mashine ya usafi ya upepo. Nikapata kama na michirizi au michubuko myeusi. sehemu ambayo iliathirika zaidi ni mgongoni, ambapo paligeuka rangi ikawa kama ya zambarau kwa siku kadhaa", lakini michubuko hii haikuwa inauma."

Tiba ya kugandisha mafuta ikoje?

A photo of Linda Evangelista

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamitindo Linda Evangelista anasema amepata madhara kutokana na kufanyiwa tiba ya kugandisha mafuta, ili kuondoa mafuta kwenye sehemu zake za mwili

Ni tiba inayotumia mbinu inayoitwa cryolipolysis.

Inaelezwa kwamba inaondoa seli za mafuta kwa kuzipooza na kuwa kwenye joto la chini kabisa. Kliniki nyingi duniani zinatoa tiba hii inayodaiwa kuondoa ambayo hupatikana chini ya kidevu, karibu na mapaja, tumbo, mgongoni au mikononi

Sio nzuri kwa watu ambao wenye uzito mnene na wnaaotaka kupunguza uzito. Madhara ambayo ni ya kawaida kwa tiba hii pamoja na michubuko ama michirizi, kujisikia kuumwa, kupata ganzi kwenye eneo lililopatiwa tiba na kuwasha.

Madhara adimu ambayo mwanamitindo Linda Evangelista amesema ameyapata ikiwemo paradoxical adipose hyperplasia (PAH), ambapo seli za mafuta zinaongezeka, badala ya kupungua.

Hakuna chanzo kinachofahamika kinachosababisha PAH lakini inasemekana ni jambo la kawaida kwa wanaume.

'Tiba hizi zinafanya kazi'

A photo of Joanne Muhammad

Chanzo cha picha, JOANNE MUHAMMAD

Maelezo ya picha, 'Mimi ni mama, naweza kuona angalau tumbo langu limepungu'

Mpiga picha wa London Joanne Muhammad alifanyiwa tiba hii miaka minne iliyopita.

"Niigundua tumbo linaongezeka na halipungua hata nifanye mazoezi gani," aliiambia BBC.

"uamuzi wangu ilikuwa zaidi kuhusu muonekano wangu ilikuwa kuhusu namna ninavyojisikia," anaongeza.

Baada ya kufanya utafiti alifanyia tiba hiyo mara tatu, ikimgharibu dola $613 kwa ujumla kupitia ofa maalumu iliyotolewa na Kliniki ya London.

"kila hatua walichukua tahadhari na kuhakikisha nimehojiwa na daktari kabla ya kuendelea na mchakato.

"walinipa tahadhari", anasema, "kwa sababu ya mashine waliyokuwa wanatumia kama mambo yatakwenda mrama, na kupata PAH kwa mfano, wanalipia upasuaji mdogo wa kurekebisha madhara."

"Mimi ni mama naweza kuona kiasi tumbo limepungua. imeondoa seli za mafuta tumboni na mambo yalionekna kwenda vizuri, lakini sharti la corona la kusalia ndani likaja."

Joanne, ambaye ana umri wa miaka 50, amerejea kwenye Kliniki yake ya awalia kwa ajili ya kupata tiba tena kupunguza mafuta tumboni, lakini anasema tiba hiyo haiwezi kuwa na matokeo ya haraka".

"Tiba hizi zinafanya kazi", anasema "lakini unapaswa kufanya pia vitu sahihi kama mazoezi, kunywa maji mengi na kuishi maisha yanayojali afya"

''Kila mtu afanye anachotaka kuhusu mwili wake'

A photo of Rainer Juati

Chanzo cha picha, RAINER JUATI

Maelezo ya picha, Rainer alibadili uamuzi wa tiba ya kugandisha mafuta baada ya kufahamu madhara yake

Injinia wa madini Rainer Juati, kutoka Accra, Ghana alipata msukumu wa kubadili muonekano wake.

Alifikiria kufanya tiba, lakini sasa, anaona linaweza lisiwe jambo zuri baada ya kujua kuhusu PAH, baada ya kusoma nakufuatilia kuhusu kesi ya mwanamitindo Linda Evangelista.

Akiwa anakuwa Rainer aliona akiongezeka, alitoka kuzodolewa akiwa shuleni kwa kuwa mwembamba mpaka kuzodolewa kwa kuwa mnene.

Kwa Rainer, jambo la utamaduni na mitandao ya kijamii ni sababu kubwa zilizomfanya atake kubadili muonekano wa mwili wake.

Alitaka kupunguza uzito wake kwa muda mfupi bila kusubiri kwa muda mrefu kuona mabadiliko ya muonekano wake.

Upasuaji ni jambo ambalo sio la kawaida sana nchini Ghana, lakini Rainer anasema linapaswa kuchukuliwa kawaida.

"Kwa sasa ni zaidi ya mila, kwa sababu huko nyumba hakuna aliyekuwa anataka kujihusisha ama kuzungumzia kuhusu upasuaji lakini sasa mtu unayemjua anasafiri kwenda ng'ambo na akirudi anakuwa na muonekano tofauti

Rainer anafikiri kwamba licha ya uwelewa wa sasa wa watu kuhusu madhara ya tiba ya kuondoa mafuta mwilini , yanayomuweka mbali na tiba hiyo, anasema haitawazuia watu wengi kuikimbilia.

Watalaam wanasema nini hasa?

A black woman with fat folds

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalam wanasema tiba zisizohusisha upasuaji zinaweza kuwa na madhara

Marc Pacifico kutoka Uingereza anaonya kuhusu tiba hii inayoonekana nzuri na inayotolewa na watu ambao hawana mafunzo ya tiba

"Ni muhimu kuhakikisha kuwa mtu yeyote anayetoa matibabu haya afahamu wazi kwamba na mgonjwa wao sio mteja kwa sababu hayo ni matibabu, "anasema.

Bwana Pacifico anasema watu wanaotaka kupata tiba hii ya kuondoa mafuta mwilini wanapaswa kufahamu kwamba" haitabiriki".

Shirikisho la wataalam wa upasuaji Uingereza , ambalo Pasifico ni makamu wake wa rais, linasema wagonjwa 21 waliokutwa na maswahibu ya tiba ya kuondoa mafuta kwa wamefika na kushughulikiwa na wataalam wake, kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni.

Taasisi hiyo imetoa wito wa kuwepo kwa sheria nzutri za kusimamia uuzaji na utangazaji wa tiba hiyo.

"Tunavyozungumza tiba ambazo si za upasuaji haimaanishi kwamba hakuna madhara, nadhani hiyo ni dhana potofu."