Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 12.08.2021: Lukaku, Ramsdale, Varane, Abraham, Kounde, Vestergaard, Messi

Barcelona bado wanadaiwa na mshambuliaji wao wa zamani wa Argentina Lionel Messi € 39m (£ 33m) kama sehemu ya bonasi ya uaminifu iliyojumuishwa katika mkataba wa mwisho wa mchezaji huyo wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 34. (El Espanol, via 90min)
Arsenal iko kwenye mazungumzo ya hali ya juu na Sheffield United kumsajili kipa wa England mwenye umri wa miaka 23 Aaron Ramsdale, na The Gunners wakilazimika kulipa ada ya mwanzo ya £ 24m ambayo inaweza kuongezeka hadi £ 30m na nyongeza. (Football. London)

Chanzo cha picha, Reuters
Romelu Lukaku yuko anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 97.5 kutoka Inter Milan kwenda Chelsea baada ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 kusafiri kwenda London Jumatano jioni. (Sky Sports)
Manchester United itatangaza kutia kumsaini beki wa kati wa Ufaransa Raphael Varane kutoka Real Madrid siku ya Alhamisi baada ya mchezaji huyo wa miaka 28 kumaliza vipimo vya matibabu Jumatano (Sun)
Chelsea wamekubali dau la pauni milioni 34 kutoka Roma kwa mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 23, ambayo ni pamoja na kifungu cha kumnunua tena (Goal)
Meneja wa Roma Jose Mourinho atazungumza na Abraham siku ya Alhamisi kujaribu kumshawishi ajiunge na klabu hiyo ya Serie A. (Mirror)
Walakini, Arsenal itatoa mshambuliaji wao wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, kwa Roma ili kumrahisishia njia Abraham kuhamia kwa Gunners. (Calciomercato - in Italian)
Sevilla wako tayari kumuuuza mchezaji anayelengwa na Chelsea Jules Kounde, hata hivyo Blues hawataki kuafikia kifungu kumuachilia mlinzi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 na inaweza badala yake kumjumuisha mchezaji katika ofa yao. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sevilla ingetaka nyongeza ya pauni milioni 20 kwa kuruhusu Chelsea ilipe ada ya Kounde kwa awamu, na Blues wana wasiwasi juu ya sheria za uumiaji wa Fedha. (90min)
Southampton wamekubali dau la pauni milioni 15 kutoka kwa Leicester City kwa mlinzi wa Denmark Jannik Vestergaard, 29. (Daily Echo)
Tottenham Hotspur na Aston Villa wote wanaandaa ofa kwa kiungo wa Southampton mwenye umri wa miaka 26 wa England James Ward-Prowse (Telegraph - subscription required)
Lyon wanafanya mazungumzo na Liverpool juu ya makubaliano ya kumsajili kiungo wa Reds mwenye umri wa miaka 29 Xherdan Shaqiri. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 21 wa Italia, Moise Kean, ambaye alicheza msimu uliopita kwa mkopo huko PSG (Sky Sports)
Inter walikuwa wamepanga kutoa ofa ya pauni milioni 50 kwa mshambuliaji wa Ufaransa wa Manchester United Anthony Martial - lakini timu hiyo ya Ligi Kuu haina nia ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 25(Mail)
Lazio wanakaribia kuafikia mkataba wa mkopo kwa kiungo wa Arsenal Uruguay, Lucas Torreira, 25, na chaguo la kufanya uhamisho huo kuwa kudumu mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Newcastle United na Joe Willock bado wako mbali kukubaliana masharti ya kibinafsi, baada ya Magpies kukubali ada ya pauni milioni 25 na Arsenal kwa kiungo huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21(Sky Sports)
Tottenham wamepania kuongeza jaribio lao la kumsajili Joao Palhinha wa Sporting Lisbon, na meneja Nuno Espirito Santo amekuwa akimtamani mchezaji huyo kwa muda mrefu (A Bola - in Portuguese)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wamefungua mazungumzo na Roma juu ya makubaliano ya kumsajili winga wa Uhispania Carles Perez mwenye umri wa miaka 23 na chaguo la kumnunua (Calciomercato - in Italian)
Waamuzi wataanza kutoa ufafanuzi wa ndani ya mchezo wa maamuzi muhimu kuanzia mapema msimu ujao chini ya mipango inayopendekezwa na Ligi ya premia (Telegraph - subscription required)














