Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 11.08.2021:Messi, Martial, Martinez, Zakaria, Shaqiri, Buta, Zouma

Zakaria

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal, Tottenham na Everton wana nia ya kumsajili kiungo wa Uswisi Denis Zakaria, 24, kutoka Borussia Monchengladbach. (Bild - in German)

Manchester City wanapanga kufungua mazungumzo mapya na kipa wa Brazil Ederson, 27, na kiungo wa England Phil Foden, 21, juu ya kandarasi mpya huko Etihad. (Mail)

LM

Paris St-Germain italzimika kuuza hadi wachezaji 10 wa kikosi cha kwanza ili kusawazisha mahesabu yao baada ya kumsajili a Lionel Messi, 34. Kiungo wa Senegal Idrissa Gueye, 31, kiungo wa Uhispania Ander Herrera, 31, na 28- mshambuliaji wa zamani wa Argentina Mauro Icardi ni miongoni mwa wale ambao wanaweza kuuzwa. (Sport - in Spanish)

Manchester United hawana nia ya kumuuza Anthony Martial msimu huu wa joto baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 kuhusishwa na uwezekano wa kuhamia Inter Milan. .(Telegraph - subscription required)

BM

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham bado wanaendelea na mazungumzo ya kumsaini Lautaro Martinez, 23, licha ya ripoti zinazoonyesha kuwa Inter Milan hawataki kumuuza mshambuliaji huyo wa Argentina na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, anayekamilisha uhamisho wa kujiunga na Chelsea. (Football Insider)

Liverpool na Lyon wametofautiana sana katika uthamini wa Xherdan Shaqiri, na Reds wanataka angalau pauni milioni 12 kwa fowadi huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 29. (Liverpool Echo)

Everton wamepanga kutoa ofa ya pauni milioni 3 kwa beki wa kulia wa Antwerp na Ureno Aurelio Buta, 24, ambaye pia ameivutia Celtic. (Sun)

Arsenal wanataka kusalia na mlinzi wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 Rob Holding klabuni hapo licha kuvivutia vilabu vya Newcastle na Leicester.(Football.London)

R

Chanzo cha picha, Getty Images

Fowadi wa Everton Richarlison, 24, anaweza kucheza kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu , Jumamosi dhidi ya Southampton licha ya kutokuwa na mapumziko ya kiangazi baada ya kuiwakilisha Brazil kwenye Copa America na Olimpiki huko Tokyo. (Liverpool Echo)

Chelsea wamesimama kidete juu ya uthamini wao wa pauni milioni 25 kwa mlinzi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 Kurt Zouma, ambaye amekuwa akiivutia West Ham(90 Min)

Mkurugenzi wa soka wa Sevilla Monchi anasubiri Chelsea wampigie simu ili aweze kushinikiza uhamisho wa mlinzi wa Ufaransa 22 Jules Kounde kwenda Stamford Bridge(Express)

O

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wanasubiri Martin Odegaard aamue juu ya mustakabali wake huko Real Madrid kabla ya kutafuta mkataba wa kudumu wa kiungo huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 22. (DefensaCentral, via Express)