Virusi vya corona: Saluni za kutengeneza kucha zaanza kufunguliwa Uingereza

Saluni za kutengeneza kucha zimeanza kufunguliwa nchini Uingereza baada ya marufuku dhidi ya maambukizi ya corona yakiwa yameanza kulegezwa.

'NUKA Nails' huko magharibi mwa mji wa London ni saluni maarufu ambayo imeanzisha namna ya kipekee ya utengenezaji wa kucha.

Wateja wanatoka hata upande wa mashariki ya London kwa ajili ya ubunifu wa kipekee wa utengenezaji wa kucha katika saluni hiyo.

Saluni hiyo ilipata umaarufu kupitia mtandao wa Instagram.

"Ukiwa unatengenezwa hapa kucha, ni sehemu inayovutia sana unakuwa kama umemtembelea rafiki yako wa karibu."

"Mteja anaweza kuja saluni na hasira lakini tunaweza kuondoa hasira hiyo - ninafurahia kazi yangu katika upande huo wa kumfanya mtu afurahi, hivyo wakati wa marufuku ya kutoka nje, nilikosa nafasi hiyo sana," alielezea Kadimah, mtengenezaji kucha.

Wateja wengi walikuwa wanahangaika kutengeneza kucha zao wakati wa marufuku ya kutoka nje.

Wateja wanasema fursa ya kutengeza kucha zao , inawafanya waone ,maisha yanarejea na kuwafanya kujihisi vizuri na kujiona kuwa ni wao.

All photos subject to copyright.