Wanazuoni Nigeria wanasema nini juu ya ubakaji uliokithiri nchini humo?

Tatizo la ubakaji limekuwa likiisumbua jamii, hususan nchini Nigeria. Katika miaka ya hivi karibuni kumekua na ongezeko la vitendo vya unyanyasaji wa aina hii katika jamii nyingi nchini humo.

Ubakaji wa watu wazima dhidi ya wasichana limekua si jambo la ajabu, hususani ni kwa wasichana wadogo nchini Nigeria.

Kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la Noipolls nchini humo mwezi Julai 2019, ilionyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu alibakwa walau kabla ya kutimiza umri wa miaka 25.

Matukio ya ubakaji ni nadra sana kuripotiwa na waaathiriwa wa ubakaji huhofia kuongea wazi kuhusu waliyotendewa kwa hofu ya kunyanyapaliwa.

Adhabu ya ubakaji

Kumekua na mjadala mkubwa nchini Nigeria juu ya hukumu inayopaswa kutolewa kwa mtu anayepatikana na hatia ya kubaka.

Hakuna hukumu inayotambuliwa rasmi ya kosa la ubakaji nchini Nigeria, kwani kila jimbo lina adhabu yake kwa wale wanaopatikana na kosa la ubakaji.

Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na kosa la ubakaji ni hadi kifungo cha miaka 14 jela katika baadhi ya majimbo, na kifungo cha maisha jela katika mengi ya majimbo.

Je Uislamu unasemaje?

Mwanazuoni maarufu wa Kiisalamu nchini Nigeria , Dkt. Isa Ali Pantami anasema kuna haja ya kujumuisha sheria za kidini katika sheria ya ubakaji, kwani anasema dini inakinzana na sheria hizo.

''Kama ubakaji haukufanyika kwa nguvu, haukutishia maisha ya mwanamke au kumshushia hadhi yake kama inavyoelezwa katika Suratul Anur," Pantami alisema.

Hata hivyo, anasema kwamba matumizi ya nguvu kama silaha, hukumu yake inaelezwa katika Surah Maidah.

Dkt. Pantami pia anasema kwamba sheria hizi ni sheria nzuri za Mungu na akaongeza kuwa nchi zinazozifuata sheria hizi huishi kwa amani.

Sheikh Ibrahim Daurawa pia ni mwanazuoni maarufu nchini Nigeria anayesema kuwa ubakaji ni uhalifu mkubwa katika Uislamu iwe kwa wanaume au wanawake.

"Pia inategemea ni wapi mwanaume alipombaka mwanaume, suala la ni wapi alikombaka pia litaangaliwa, mfano kama ni nyumbani kwa mwanaume, basi nyumbani inageuka kuwa yao wawili. Halafu kama ubakaji umefanyika kazini, barabarani, suala la mahali ulikofanyiwa linaangaliwa ". alisema.

Jinsi hukumu inavyotolewa

Inaangaliwa kama mbakaji alitumia nguvu, kwahiyo mtu anayembaka mwanamke , adhabu inayotolewa kwake ni sawa nay a mtu aliyeiba silaha, inamaanisha atauawa mara moja.

  • Iwapo mwanamke mwanamke mzee adhabu itatolewa kwa kuzini na adhabu ya uzinzi kama hajaoa ni hukumu ya kifo na pia kama hajaoa ataadhibiwa . Viboko 100 na kifungo cha mwaka mmoja gerezani na atatozwa faini ya $ 80,000 .
  • Kama mwanaume atabakwa, mbakaji atahukumiwa kifo kwasababu atakua ameshiriki mapenzi ya jinsia moja na muathirika atatakiwa kulindwa kulipia gharama za matibabu .
  • Kama ni mtoto, hata kama silaha haikutumiwa, hukumu itakayotolewa kwa mbakaji ni kifo.
  • Kama mwanamke ataenda mahali ambapo anafahamu atabakwa, pia atahukumiwa
  • Mwili wa mwanafunzi wa chuo kikuu, Uwavera Omozuwa, ulipatikana akiwa amebakwa na kudungwa visu ndani ya kanisa, na mshukiwa kwa sasa anashikiliwa.
  • Wanaume kadhaa walibainika kuwa walikua wanambaka msichana mwenye umri wa miaka 12 kwa muda wa miezi 12 katika jimbo la Jigawa kaskazini magharibi ; Washukiwa 11 wanashikiliwa na vyombo vya usalama
  • Kikundi cha wanaume kinadaiwa kumbaka Barakat Bello katika jimbo la Oyo ; hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyakamatwa kuhusiana na kisa hicho.
  • Msichana mwenye umri wa miaka 17- pia alibakwa na kikundi cha wanaume katika eneo la Ekiti; wanaume wawili walikamatwa kuhusiana na tukio hilo.
  • Mwili wa msichana ulipatikana katika msikiti katika eneo la Kurmi Mashi katika jimbo la Kaduna.
  • Mtoto wa miezi mitatu alibakwa katika jimbo la Nasarawa ; Mtu mzima alifikishwa mahakamani kwa mashraka ya ubakaji kuhusiana na tukio hilo.

Kwanini visa vya ubakaji vimekithiri Nigeria?

Inadaiwa kuwa nchini Nigeria kwamba waathiriwa wa ubakaji wanahisi kwamba vikosi vya usalama havitafuatilia wahalifu na badala yake watalazimika kuwalipa maafisa wa usalama.

Tatizo la ubakaji na unyanyasaji wa kingono limeongezeka hivi karibuni, na mkuu wa polisi anasema kuwa kuanzia mwezi Januari nadi Mei mwaka huu, kulikua na visa vya ubakaji 717 vilivyoripotiwa kote nchini Nigeria.

Wataalamu wa sheria kama vile Barrister Bulama Bukarti wanasema tatizo hilo limetokana na mchakato mrefu wa uchunguzi wa polisi wa makaso ya ubakaji pamoja na mfumo wa mahakama unaozorota nchini humo.

Bulama amesema kwamba utekelezwaji wa sheria ya kiislamu utasaidia kutatua kesi zilizopo mahakama ambazo zingeweza kuwa rahisi kupata ushahidi wa uhalifu au kuwaachilia huru wasio na hatia kwa muda mfupi.

"Katika mahakama zinazofuata sheria ya kawaida, washukiwa lazima wafahamishwe kuhusu kosa lao, lakini katika Mahakama za Kiislamu mshitakiwa ataambiwa kuapa katika Quran kwamba hakutenda kosa hilo," Audu alisema Bulama.