Je vita 'dhidi ya ugaidi' vitawahi kuisha?

Chanzo cha picha, Reuters
Shambulio baya la kisu lilitokea wiki iliyopita magharibi mwa mjini London, limekumbusha watu kuwa tishio la ugaidi halijaisha. Lakini je vita dhidi ya ugaidi iliyotangazwa na aliyekuwa rais wa Marekani George W Bush mwaka 2001 vimefikia wapi? Je bado mapambano hayo yanaendelea? Na kama jitihada hizo zinaendelea zimefua dafu ama ni hasara tu ya kupoteza fedha?
Ni takribani miaka 19 tangu Marekani iliposhambuliwa na tukio la kigaidi, Septemba 11, 2001 na kuacha maelfu ya Wamarekani na wafanyakazi wa taifa hilo kupata janga.Na wanawake wengine walisalia Afghanistan, Iraq, na maeneo ya Afrika.
Mashambulizi ya anga katika maeneo ya pembezoni za dunia dunia yamekuwa yakiendelea kuwalenga washukiwa wa ugaidi duniani kote.
Jitihada kubwa ambazo zimewekwa bado hazijaweza kufanikiwa kukabiliana na vitisho vya ugaidi vinavyoendelea duniani kote.
Sasha Havliclek, tmkurugenzi wa taasisi ya mdahalo wa mkakati huo wa kupambana na ugaidi amekuwa akifuatilia vita hivyo tangu vilivyoanza.Na anaeleza kuwa kuna utofauti kati ya uhalisia na matamko ya jukwaani."Hotuba ilipuuziwa mara tu rais [Barack] Obama alivyoingia madarakani mwaka 2009 lakini uhalisia ni kuwa kulikuwa na mengi zaidi ambayo yalikuwa yanaendelea na kinyuma na makubaliano ya mbinu za kupambana katika vita hiyo ya ugaidi.
Chini ya utawala wa Obama inafahamika wazi kuwa mashambulizi mengi ya anga yalifanyika katika maeneo kama ya Afghanistan na Pakistan. Na mazungumzo yote yalikuwa Marekani kwanza na kulikuwa na mtazamo mkubwa ambao haujakaa sawa... Ni kama vile tunaona kuwa operesheni za kigaidi zinakuwa zaidi.
'Kuibuka kwa makundi ya makubwa zaidi ya kigaidi'
Mtazamo mkubwa kuhusu mpango ulioanzishwa na rais Donald Trump wa kupambana na ugaidi uko tofauti,balozi Nathan Sales.
Alisema alimuuliza kama vita hii ni ileile ambayo ilianzishwa na utawala wa Bush - au vita ile iliisha?"Hapana, mapambano bado yapo yanaendelea , tunashinda mapambano haya dhidi ya maadui wetu au makundi yaliyojidhatiti kuwa maadui."

Chanzo cha picha, Reuters
Alianisha kuwa mfano kundi la kiislamu la Islamic State (IS) ambalo limeenea katika katika mataifa mbalimbali walifanikiwa kumuangamiza kiongozi wa kijihadi huko Baghuz nchini Syria mwaka jana pamoja na kiongozi wa kigaidi Abu Bakr Al-Baghdadi.
Wakati kundi hilo la kigaidi la IS bado lina nguvu duniani kote.
Siku ya Jumatano,Marekani ilitoa ripoti ya ugaidi nchini humo.
Kwa baadhi ya Wamarekani , inaonekana wazi kuwa ilisitishwa baada ya kumbukumbu za shambulio la Marekani 9/11.
Kutangazwa kuanza kwa vita dhidi ya ugaidi wakati ule wa utawala wa rais Bush alisema kuwa "uwe pamoja nasi au usiwe pamoja nasi". Hakukuwa na aliyekuwa upande wa wa kati, hakuna fedha zilizotolewa, ili mataifa ya Mashariki ya kati kuachana na mpango huo.
Nchini Iraq, ambako Marekani na Uingereza iliivamia mwaka 2003, nah ii ilisababisha kutengeneza maadui wakubwa ambao wapo mpaka sasa kutokana na msingi ambao ulikuwepo na hivyo kusababisha ongezeko la harakati za makundi ya kijihadi.
Mina Al-Orabi ni mhariri katika gazeti la nchi za falme za Kiarabu UAE 'The National'. Asili yake ni kutoka Mosul, mji wa pili wa Iraq , ambao unachukizwa na kuharibika kwa mitaa yake kutokana na mapambano ya IS.
"'Nchini Iraq," alisema, "kulikuwa na matukio ya wazi ambayo yanaonyesha kuwa Marekani inalionea taifa la Iraqi. Mwaka 2003 maamuzi ya kuondoa majeshi na polisi, maamuzi hayo yalisababisha maelfu ya kama sio mamia ya wafanyakazi vijana bila ajira.… kwa wazo la kuwaondoa wote katika taifa hilo, nao wakaamua kuwa washirika wa kundi la kigaidi la al-Qaeda nchini Iraq na baadae washirika wa IS."
'Tuko mbali kumaliza'Sera nyingine ambazo zilikuwa zina makosa zimetengenezwa kuwa sehemu ya vita hivi licha ya kwamba baadae rais Obama alizifanyia mabadiliko lakini matokeo ya maamuzi mabaya yapo mpaka leo.
Kushikiliwa kwa mamia ya washukiwa katika gereza la Guantanamo Bay,uhalisia wake ni kwamba vitendo vya kikatili ambavyo vilifanyika kwa mateka huku dunia ikiwa imefumbia macho duniani kote ndio matokeo yake yanaendelea mpaka sasa.
Haya yote yamekuwa yakifanyika wakati mataifa ya magharibi yakikosoa mamlaka.Balozi Sales kutoka Marekani anasema "dunia imejifunza mengi kwa kile kinachofanya kazi na kile ambacho hakiwezi kufanyika… hivyo kujumuisha kile tulichojifunza katika namna mpya ya kukabiliana na tatizo hili la ugaidi
Anakosoa zaidi kile ambacho kilikuwa kikifanyika katika gereza la Guantanamo Bay, pamoja na Marekani na washirika wake wa mataifa ya Magharibi , ambao sasa sasa wamewatelekeza raia wao katika kambi za kuteswa huko Syria na Iraq.Anasema mataifa haya yanapaswa kujirejea.
Haiwezekani kuanisha matokeo ambayo yamesababishwa na vita hivi vikubwa vya ugaidi. Lakini labda unaweza kukadiria kwa kusema dola za Kimarekani trilioni moja.
Gharama kubwa ambayo imetumika kwa ajili ya jeshi, wataalamu wa kiintelijensia pamoja na mashambulizi ya kianga.Na matokeo ni kidogo sana yameweza kuonekana kuzuia majanga haya ya ugaidi na kuwaweka watu katika mtazamo wa kigaidi.Shiraz Maher kutoka taasisi ya Kings iliyopo mjini London, utafiti walioufanya unaamini kuwa vita hiyo imesababisha matatizo mengi ya sasa katika jamii.
Shiraz Maher kutoka taasisi ya Kings iliyopo mjini London, utafiti walioufanya unaamini kuwa vita hiyo imesababisha matatizo mengi ya sasa katika jamii.
"Kama ukiangalia haya mambo kwa mtazamo mkubwa wa kiislamu, wanajeshi wa Islamic State na Syria na Iraq au wote ambao wana mlengo moja," alisema, "utaona wote wana vita ya kibaguzi dhidi ya bara la ulaya , kuchochea chuki kwa waislamu kutokana na kile kilichotokea dhidi ya waislamu,matokeo ya janga la wakimbizi wa Syria na hayo yote na mengine mengi yamepelekea kutengenezwa kwa maadui . Si sawa kufikiri kuwa vita imekwisha kwa mtazamo wowote ule.
Je kuna namna yeyote kampeni hizo za ugaidi kuisha?
Mpango huu utaisha na kusababisha vita ya ugaidi kuisha?, Ni kama haiwezekani tena.
Kwa sababu ni kama uhalifu, ugaidi unaweza kupungua endapo maafisa watataka jambo hilo. Na leo tayari kuna vitisho vipya vya ugaidi na hata inaonekana kuhoji kama inaweza kutokea kuwa vita hii inawea kukoma siku.












