Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Je shule kufungwa ni suluhu kwa watoto kuepuka maambukizi?
Wakati shule nyingi duniani zikiwa zimefungwa, wazazi sasa wanahangaika kujua nini wanapaswa kukifanya kwa ajili ya kuwalinda watoto wao na nini wasikifanye kwa watoto wao.
Iwapo shule zimefungwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona, je hata nyumbani watoto hawapaswi kucheza na watoto wengine?
Je hii inamaanisha kuwa watoto hawatatakiwa kucheza kabisa?
Kwa upande wao watoto wanaweza kudhani kuwa hii ni likizo kama ilivyo likizo nyingine, ambazo watataka kwenda kutembea na kufurahi na watoto wenzao.
Ingawa mpaka sasa idadi ya watoto waliothibitishwa kuambukizwa ni ndogo lakini wataalamu wa tiba hawajahitimisha kwamba hii ni kwasababu wao hawawezi kuambukizwi.
Maelezo ambayo yanaonekana kujitokeza kwa sasa ni kwamba mlipuko wa virusi vya corona unahusishwa na kuambukiza zaidi watu wazima ikilinganishwa na watoto.
"Hili huenda lina ukweli zaidi kuliko ile dhana ya kwamba watoto wana mfumo wa kinga imara zaidi kukabiliana na virusi vya corona," Andrew Freeman, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukizwa katika chuo kikuu cha Cardiff, ameiambia BBC.
Kwa kawaida watoto wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi na mara nyingi huchukuliwa kama wasambazaji wakubwa', kulingana na Ian Jones.
Kwa hiyo tunaweza kutarajia idadi kubwa ya watoto kuambukizwa lakini hali ni tofauti kwa sasa.
Huenda ikawa watoto wana mfumo imara wa kinga kukabiliana na virusi, au makali ya virusi vyenyewe inakuwa kidogo kwa watoto ikilinganishwa na watu wakubwa, na hivyo basi watoto hawapelekwi kupata matibabu, hawafanyiwi vipimo wala kusajiliwa.
Utafiti zaidi unastahili kufanywa ili kupata uelewa wa mlipuko huu dhidi ya watoto.
Lakini pia huenda ikawa watoto wametegwa kabisa na kuwa katika uwezekano mdogo wa kupata maambukizi kwa kufunga shule, na kuwekwa katika mazingira mazuri.
Unawezaje kuwazuia watoto kuwa kuacha kucheza katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa corona
- Ni muhimu kufuata maelekezo ya wizara ya afya ya namna ya kujikinga na virusi vya corona
- Kuepuka kwenda kwenye maeneo ya michezo kwa watoto
- Mzazi anapaswa kumletea michezo mtoto wake katika maeneo ya karibu
- Wasiliana na marafiki na familia kupitia mtandao
- Wazazi wanapaswa kuwahamasisha watoto wajisomee nyumbani na kufanya kazi za sanaa
- Ni vyema kucheza michezo ya kwenye video
Kufungwa shule kuna mtazamo gani?
Baadhi ya wazazi na haswa walimu, ambao wao wako nyumbani na watoto kuna ambao haungi mkono kukataza watoto kucheza.
Lakini wengine wamekiri kuwa kuwachunga watoto ni kazi ngumu.
Kikubwa sasa kwa watoto ambao wanafahamiana na wazazi au ni vyema watoto wa jamii moja wawe na mzunguko mmoja wa kucheza.
Familia majirani wachukue hatua ambazo zinafanana katika tahadhari dhidi ya corona.
Wazazi wanapaswa kupanga muda kwa ajili ya watoto wao kusimamia watoto wakati wa kusoma na kupumzika.
"Hii sio likizo, ni dharula, wanapaswa kuzingatia kuwafundisha watoto, haijalishi taaluma yao ni ipi?" mzazi ambaye ni mwalimu pia amesisitiza.
Hofu kwa wazazi na wanafunzi kuhusu likizo ya waliyopewa
Hajajulikana ni lini ugonjwa wa corona utaisha au utapata tiba au chanjo yake, jambo ambalo linawapa hofu kwa wazazi kuhusu athari ambazo wanafunzi watakabiliana nazo
Athari kwenye upande wamasomo, mitihani na hata mtiririko wa elimu ulivyo.
Mfano kwa Tanzania, taifa limetangaza siku 30 za mapumziko , huku wengine walikuwa wanatarajia kuanza mitihani yao au kuhitimu.
Ni namna gani watoto wanaweza kupimwa uwezo wao wa ueleo wakati walikuwa nyumbani kipindi kirefu.