Coronavirus: Wafahamu watu mashuhuri duniani waliopata maambukizi ya virusi vya corona

Tom Hanks na mkewe Rita Wilson

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Muigizaji wa filamu wa Marekani Tom Hanks na mkewe Rita Wilson

Wananasiasa, wanamichezo na waigizaji maarufu duniani ni miongoni mwa watu walioambukizwa na virusi vya corona.

Muigizaji nyota wa tuzo za Oscar Tom Hanks amebainika kuwa yeye na mke wake Rita Wilson wamekutwa na maambukizi ya virusi vipya vya ugonjwa wa corona nchini Australia.

Bwana Hanks na mkewe Wilson, ambao wote wana miaka 63, walienda kupata ushauri wa daktari baada ya kuona kuwa wana dalili za mafua huko Queensland,na baadae muigizaji huyo kuandika katika kurasa yake ya Instagram kuwa na virusi vya corona.

Muigizaji huyo na mkewe walitengwa wakiwa katika hali nzuri katika hospitali ya nchini humo, taarifa zilisema.

Hanks aliigiza filamu kuhusu Elvis Presley.

Maambukizi ya wapenzi hao yamebainika mara baada ya shirika la afya duniani kutangaza rasmi kuwa mlipuko wa virusi vya corona ni janga la dunia.

Hanks aliandika kwenye kurasa yake ya Instagram: "Tulikuwa tunajihisi uchovu, tulikuwa na mafua na mwili ulikuwa hauna nguvu. Tulikuwa tunahisi homa pia.

"Kama jambo sahihi dunia inapaswa kufanya inapaswa kufanya sasa, tulipimwa na kukutwa na virusi vya corona".

Eshaq Jahangiri, Makamu wa rais wakwanza wa Iran

Iran

Chanzo cha picha, Getty Images

Huko Iran, makamu wa kwanza wa rais bwana Eshaq Jahangiri, amekutwa ameathirika na virusi vya corona pia.

Bwana Jahangiri ni kiongozi wa juu wa kisiasa ambaye amepata virusi hivyo ambavyo vimeuwa watu zaidi ya 354 na watu 9,000 kupata maambukizi tangu maambukizi yaingie nchini Iran mnamo Februari.

Mkamu wa rais huyo mwenye umri wa miaka 63 ni miongoni mwa maafisa 24 ambao na watunga sheria humo kuambukizwa na corona.

Mbunge wa zamani, Jahangiri ni kiongozi wa ngazi ya juu katika jumla ya makamu wa rais 12 wa serikali ya rais Hassan Rouhani.

Haijajulikana ni kwa kiasi gani kiongozi wa nchi hiyo kama hajakutana na watu wenye maambukizi kama Jahangiri.

Nadine Dorries Waziri wa Afya wa Uingereza

Waziri wa Afya wa Uingereza
Maelezo ya picha, Waziri wa Afya wa Uingereza

Katika hali ya kustaajabu pia, Waziri wa afya na mbunge wa chama cha Conservative nchini Uingereza Nadine Dorries amesema amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Bi Dorries, mbunge wa kwanza kugundulika na maambukizi, alichukua tahadhari zote baada ya kubaini kuwa ameathirika, na amejiweka karantini nyumbani kwake.

Hali hii imekuja wakati kukiwa na taarifa ya kifo cha mtu wa sita kutokana na virusi vya corona nchini Uingereza ambako kuna visa vya watu 382 kuambukizwa.

Mtu aliyepoteza maisha hivi karibuni ni mzee mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa na changamoto za kiafya.

Bi Dorries, mbunge wa Bedfordshire ya kati, amesema katika taarifa yake kuwa Idara ya afya imeanza kuwafuatilia watu waliokuwa karibu naye, na ofisi yake ya bunge inafuatilia hilo kwa karibu.

Alieleza kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu hali aliyokuwa nayo, lakini akielezea hofu aliyonayo kuhusu mama yake ,84, anayeishi naye ambaye naye ameanza kukohoa siku ya Jumanne.

Haijulikani ni vikao vingapi Bi Dorries amehudhuria Westminster au katika jimbo lake hivi karibuni.

Idara ya afya imesema alianza kuonesha dalili siku ya Alhamisi juma lililopita -alipohudhuria dhifa iliyofanyika Downing Street iliyohodhiwa na Waziri Mkuu Boris Johnson- na akawekwa karantini tangu siku ya Ijumaa.

Daniele Rugani Beki wa kati, wachezaji wa Arsenal wajiweka karantini

Daniele Rugani alishiriki katika mazoezi katika uwanja wa Juventus siku ya Jumanne

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Daniele Rugani alishiriki katika mazoezi katika uwanja wa Juventus siku ya Jumanne

Licha ya baadhi ya mechi kusitishwa, klabu ya Juventus imetangaza kwamba beki wa kati wa Italia Daniele Rugani amekutwa na virusi vya corona.

Klabu hiyo ya ligi ya Serie A imesema kwamba imechukua hatua zote za kumtenga mchezaji huyo zinazohitajika kisheria ikiwemo kuwashirikisha wale ambao waligusana naye

Klabu hiyo imeongezea kwamba Rugani mwenye umri wa miaka 25 kufikia sasa hajaonesha dalili za ugonjwa huo.

Michezo yote nchini Italia imeahirishwa hadi Aprili 3 huku taifa hilo likijiweka katika karantini kutokana na mlipuko huo wa coronavirus.

Rugani ameichezea klabu yake mara saba pekee msimu huu na hakutumika katika mechi ya Juventus dhidi ya Intermilan ambayo klabu hiyo iliibuka na ushindi wa 2-0 katika mechi iliochezwa bila mashabiki siku ya Jumapili.

Mechi ya Inter iliotarajiwa kucheza dhidi ya Getafe katika michuano ya Europa siku ya Alhamisi pia imeahirishwa.

Rugani ameshinda mataji manne ya ligi ya Italia akiichezea Juventus na aliichezea Italia mara saba, mara ya mwisho ikiwa 2018.

Siku ya Jumapili alichapisha picha mtandaoni katika chumba cha maandalizi cha Juve akisherehekea ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Inter pamoja na wachezaji wenzake.

Italia imerekodi visa 12,000 vya maambukizi na vifo 827 kutokana na virusi hivyo.

Wakati huohuo mechi kati ya Arsenal na Manchester City imeahirishwa baada ya kuwepo kwa hofu ya virusi vya corona, huku baadhi ya wachezaji wa Arsenal wakiamua kujitenga baada ya mmiliki wa klabu ya Olympiakos Evangelos Marinakis kupatikana na virusi hivyo.

Arsenal inasema kwamba Marinkis mwenye umri wa miaka 52 alikutana na baadhi ya wachezaji wake wakati Arsenal walipokuwa wenyeji wa mechi na klabu hiyo katika kombe la Europa wiki mbili zilizopita.

Mmiliki wa klabu Olympiakos Evangelos Marinakis

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Mmiliki wa klabu Olympiakos Evangelos Marinakis

Nottingham Forest na mmiliki wa klabu Olympiakos Evangelos Marinakis amepatikana na virusi vya corona.

Marinakis, 52,alikuwa katika mji wa Ground kuhudhuria mechi ya klabu yake dhidi ya Millwall siku ya Ijumaa.

"Bwana Marinakis alipewa matibabu baada ya kupatikana na dalili za kwanza za ugonjwa huo aliporejea nyumbani kutoka Ugiriki,"

"Klabu hiyo sasa inatafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa matibabu na asasi husika za michezo kuhakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa kukabiliana na maambukizi."

Marinakis awali alidokeza kuwa na dalili za coronavirus katika mtandao wake wa Instagram.

Olympiakos itakuwa mwenyeji wa Wolves Alhamisi katika ligi ya Europa, baada ya Uefa kupinga ombi la Wolves la kutaka mechi 16 za mwisho katika mkondo wa kwanza kuahirishwa.